Yaliyonipata fb yamempata mwanajf yoyote?b | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yaliyonipata fb yamempata mwanajf yoyote?b

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by SHIEKA, Dec 29, 2011.

 1. SHIEKA

  SHIEKA JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2011
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 8,124
  Likes Received: 938
  Trophy Points: 280
  Basi bwana. Nikajifungulia kiakaunti changu facebookili nisocialize kama wengine.Unajua tena mambo ya siku hizi, mtu unataka uwemo usibaki nyuma. Siku moja nkatembelea hicho kiakaunt nikakuta ujumbe:"Ntawasiliana na wewe kwenye email yako" halafu akaweka jina 'Mirbel Sanko.
  Na kweli, keshoyake nilipofungua email nikakuta ujumbe kutoka kwa huyo mtu.Alisimulia kisa kireefu na kinene kama joka la anaconda kule amazon. Nisikuchoshe ila kwa kifupi alisimulia kisa hiki: Kwamba yeye ni mkimbizi wa ivory coast anayeishi Senegal.Baba yake, Dr Fredrick Sanko alifariki wakati yeye Mirbel bado anasoma na aliacha kiasi fulani cha fedha kwenye benki huko ivory coast. Nilitajiwa fedha hizo kwamba ni dola za kimarekani 30,000. Na kwamba anachotaka kufanya eti ni kuhamishia hizo fedha kwenye akaunti nyingine nje ya ivory coast. Je, naweza kmpa namba ya akaunti yangu ili aniambie jinsi ya kuhamisha? aliomba na eti deal ikifanikiwa atanikatia asilimia 5 ya hiyo hela! Kufika hapo nikagundua mara moja kwamba huu ni mchezo wa matapeli wa kinigeria (Nigeria 419) wa kulaghai watu.Nikashit hiyo email wala sikujibu.Akaendelea kuniandikia, mimi kimya! Akanitumia picha yake(ni mwanamke) akisema kwamba ameisoma profile yangu kwenye fb na eti amenipenda sana na eti anataka niwe wake wa maisha. Nikazidi kuogopa na kukaa kimya.Sijamsikia tena, kakata mawasiliano namshukuru Mungu.

  Pointi yangu hapa ni kwamba matapeli wa kimataifa wanatumia social networks na pengine forum kama hii kunasa mawindo yao. Mie nshafunzwa hatari na hila zilizo kwenye internet. Wengine je? wana tahadhari hizo? Hilo laweza kabisa kutokea hapa JF yaani mwanachama wetu akanaswa na haya matapeli kwa kutumia vivutio vikali kama nilivyofanyiwa.

  WanaJf, mods, tuwe macho!
   
Loading...