Yaliyonikuta Zanzibar - Rushwa tupu!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yaliyonikuta Zanzibar - Rushwa tupu!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Vakwavwe, Aug 18, 2009.

 1. V

  Vakwavwe JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2009
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nimeshangazwa sana na kiasi kikubwa cha rushwa visiwani hapa....
  mimi ni mtumishi wa kutoka private sector...nipo huku kwa kazi maalumu ya siku 14....nimepewe gari T XXX YYY,basi polisi wamenifanya mradi...kidogo tu wananikamata kwa makosa ma2. moja kwa nini naendesha gari yenye usajili wa Bara jambo ambalo bado linajadiliwa kwa kuwa usajili wa magari pande zote unafanywa na TRA ambayo ni moja. la PILI ni kwa nini natumia leseni ya bara wakati sheria na taratibu za kupata leseni ni sawa na zipo chini ya mamlaka moja yaani wizara ya mambo ya ndani na tRA. Inanisikitisha sana kwa kuwa vitu kama hivi ndo vinairudisha nyuma zanzibar kushupalia mambo yasiyo ya msingi...askari hawa bila woga wanamalizia kwa kusema "NIPE NYAMA YANGU YAISHE' kwa maana ya rushwa...
  jingine,zanzibar wanategemea sana biashara hasa biashara ya vitu chakavu maarufu kama 'USED' wateja wao wakubwa ni watu wa bara....hii inatokana na idadi ndogo ya wakazi wa visiwa hivi....na watu wengine wanaijaza zanzibar ni watalii ambao hawanunui viUSED hivi. sasa basi nilitegemea serikali iwasaidia masoko kwa kuruhusu wabara waje kununua kwa wingi....kinyume chake pale bandarini pametawaliwa na rushwa balaa....kuna mageti ma3 kila moja lina mtu anachukua rushwa...wao wanaita nyama yangu...ni kero. nimenunua baiskeli ya mtoto,nafika pale naombwa rushwa waziwazi kama hivo..kisa sina kibali cha polisi cha kusafirisha baiskeli...ujue nina receipt halali za mannunuzi. pale kuna kituo cha polisi cha kupokea rushwa hawatoi kibali cha kusafirisha kitu...nikaonyeshwa kituo cha malindi,nilipofika pale nikaombwa 10,000/= ya rushwa nikakata tamaa kwa kuwa kule bandarini nilikuwa naombwa buku buku tu,nikaambiwa niende kituo kingine wakati huo boat inakaribia kuondoka. nikarudi bandarini nikaliwa NYAMA three times unaanza gate la kwanza NYAMA,la pili NYAMA hao ni MGAMBO na tatu ni wenyewe POLISI wao wanataka nyama kubwa zaidi....nasikitika kwa kuwa mambo haya ni wazi sana....hivi vyombo vya usalama vipo????mnafikiri mnawakomoa waBARA kumbe mtadoda na MAUSED haya.....
  anyways...najuuuuuuuta kununua libaiskeli hili.
  LAKINI NAANDAA MKAKATI BINAFSI WA KUWAUMBUA Watu hawa pesa yangu haiwezi kuliwa hivihivi..
   
 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  Aug 18, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Hivyo ni baadhi ya vituko vya Zenj!..... Pole sana
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Aug 18, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Teh teh teh unajua znz wanategemea nini kule? Kule njaa tupu basi ndo hivyo wanavyo toka wakazi wa kule.
   
 4. Shishi

  Shishi JF-Expert Member

  #4
  Aug 18, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,244
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135

  Aisee pole sana..hiyo baiskeli ilkuwa ya pesa ngapi naona hizo nyama labda zilikuwa nyingi kushinda hiyo cost ya baiskeli! DuH!!!!!
   
 5. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #5
  Aug 18, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ha, ha,ha- Mkuki kwa nguruwe, Kwa binadamu mchungu. Na huko kwenu si mnatutenda hivyo hivyo. Ukija huko ukitaka kupanda basi tu. Vibaka watakwapua kila kitu kilicho mifukoni mwako hata ile mifuko ya ndani kabisa.
   
 6. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #6
  Aug 18, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Serikali za CCM zinadhoofisha uchumi wa Zanzibar. Unajuwa kiongozi wa juu wa SMZ amechaguliwa Dodoma, hivyo machinjio yake atakuwa dodoma
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Aug 18, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Nyie mmezidi hivi wananchi wanategemea nini kujiingizia kipato kule znz? Karafuu au Nazi? Na mzunguko wa pesa ukoje? Maana nilienda kwa Rajju pale bia wanauza ghari sana ambapo huku bara kile kiwanja kama grocery tu ya sebuleni.
   
 8. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #8
  Aug 18, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,925
  Likes Received: 23,565
  Trophy Points: 280
  Udumu Muungano!!!
   
 9. Kobe

  Kobe JF-Expert Member

  #9
  Aug 18, 2009
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 1,756
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  haha ha ha ha wao wanaamini kila aendaye zenji ni mtalii hivyo unakuwa na pesa na wao wanaona halali kula nyama yako(pesa) basi usiombe kama ungetaka kukodisha hizo private Van duh ungeumia roho jamaa wanataja bei utadhani hiyo pesa inaokotwa, aaah jamaa wanatia simanzi maendeleo hakuna lakini tmaa kwenye pesa ipo kubwa sana.mi nionavyo muungano ukivunjika kule hakutakalika manake sijui watashika wapi.
   
 10. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #10
  Aug 18, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...jifanye expatriate, unakitema 'kidhungu' mwanzo mwisho,..watakuachia tu.
   
 11. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #11
  Aug 18, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...hasa pale police mazizini, au bububu! wanaudhiiii na mapipa yao, mpaka usiku wa manane!
   
 12. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #12
  Aug 18, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  sio huko tu bali hata ukipita Airport za zanzibar na Dar. mambo ni hayo hayo..

  Pole sana
   
 13. dmaujanja1

  dmaujanja1 JF-Expert Member

  #13
  Aug 18, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Fidel80 KwaRaju unapafahamuuuuu du ndiyo maana unapenda kujiXpressssssss!
  hONGO YA bUKU ZENJ kubwa sana ulitakiwa utengeneze chenji hata mia tano kina Hamii wanapokea tu.
  Pole kaka
   
 14. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #14
  Aug 18, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135

  Hilo neno "yangu" limeweka uzito mkubwa sana. Duh!
  Najisikia kucheka
   
 15. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #15
  Aug 18, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Sijui ni uelewa mdogo wa mambo katika jamii yetu au ni ukaidi tu wa kutaka kufungwa.

  Huwezi kuja hapa kulia lia kuhusu rushwa wakati ulitoa rushwa!

  Na wewe ndio hao hao, mtoa rushwa mkubwa, adui wa haki, mzandiki, criminal mkubwa!

  Kahadithie kwingine huo udaku rushwa, sio hapa.
   
 16. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #16
  Aug 18, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kibunango unauhakika gani kama hayo mambo kweli yanafanyika au ndio kuwapaka mavi hao jamaa tu.
   
 17. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #17
  Aug 18, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Nipe NYAMA YANGU YAISHE, kama unadaiwa vile, lol

  Pole sana, huo ndo uzanzibari bana.
   
 18. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #18
  Aug 18, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Hayo yapo na yapo mengi zaidi ya hayo...
   
 19. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #19
  Aug 18, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Zamani ikiitwa kitoweo...
   
 20. V

  Vakwavwe JF-Expert Member

  #20
  Aug 18, 2009
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  thanks for your comments, unajua Bondia mwenye kutumia akili huwa hakimbilii kujibu mapigo baada ya kupokea konde zito...anajipanga kwanza. nimeenda vituo vitatu vya polisi wote wanataka rushwa!!!!isitoshe rushwa inadaiwa wazi kabisa ...nikajua kuwa system nzima ndo ilivyo...ulitaka niwaachie baiskel yangu???...hizo rushwa plus legal transport and tax was more than 50% of the bicycles' price. hivi PCCB ni ya muungano au ZNZ wana yao?mimi nilikuwa nasikia askari wa Kenya ndo wanasema nipe kitu kidogo nikuache...kwa Tanzania hii ni first time kuona na nimeonea huku upande wa pili wa nchi....hao wawakilishi wanawakilisha nini kama watu wanaendesha kila kitu wanavyotaka wao???hakuna wa kukemea hili...?
   
Loading...