Yaliyonikuta kwa mke wa FFU

Yaliyonikuta kwa mke wa FFU

mzee wa kasumba

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
1,440
Reaction score
2,963
Maishani kuna mengi ya kukumbukwa, ila kuna mengine ya kukumbukwa zaidi. Hii ni kutokana na uzito wake

Mke wa mtu sumu

Dada huyu alikuwa na duka jirani na ambapo nilikuwa naishi. SIkuwa na mazoea naye kabisa awali. Lakini kadiri siku zilivokwenda alianza kuleta mazoea kidogo kidogo.

Muda wote sikuwa najua kama dada yule alikuwa na mume, nami sikuuliza kwa sababu hakunivutia kumtongoza.

Mazoea yalizidi kiasi kwamba siku nikibadili njia hulalamika sana na kuwa huwa anamiss kuniona na lile tabasamu langu uchwara.

Watoto wa mtaa wataungana nami kwani wanajua, demu akishaanza kusema kuna muda huwa anakumiss basi moja kwa moja unaona hapa ushakubalika. Basi hata kama mwanamke hukua na mpango wa kumpelekea moto utatafuta njia yoyote ile. Basi nami nikaona hapa bila shaka nimeshaeleweka ngoja nianze kucheba cheba.

Siku hiyo nikamwambia "siter ee",
akaitika "bee"

Nikamwambia kuna kitu natamani sana kukwambia ila najikuta roho inasita, ila usijali siku moja ntakwambia tu wala usijali. Kama utapata muda (siku flani) nitafute nikwambie.
Akasema sasa ntakutafutaje wakati wee namba yako sina? Akasema nipe namba yako. Nikambwia namba tuu hiyo mamy. Akasogeza simu yake nikaandika nambari kisha nikapotea.

Kabla sijafika (kazini) ambako nilikuwa naelekea nikatangamana na ujumbe usemao Namba yangu hiyo MIMI MAMA.....

Nikamwambia ooh asante, kumbe umeolewa? Mh basi sawa.
Akasema mbona umeguna? Nikamwambia basi hata ambacho nilitaka kukwambia nimegairi maana nilijua hujaolewa.

Akasema Ongea tuu kaka, we mtu mzima bana.
Mpaka hapa nikahisi kama mdudu anataka kupasua zizi, maana alivimba ghafla. Nikasema eeebwana mchuchu amejileta mwenyewe. Hapa ni kumaliza tuu

Nikamwambia "bana sister samahani, mimi nakupenda. Afu nimekuelewa sana ujue, lakini nilikuwa naogopa kukwambia kwasababu sikutaka kuingilia mahusiano yako ila nafsi imenishinda nami ni mwanadamu. Kama nimekosea nisamehe bure mpendwa. Lakini mpaka hapa roho yangu ni nyeupeeee kwa kutua mzigo niliokua nimeubeba".

Jibu alilolitoa liliniacha mdomo wazi
Alisema "Hayo mbona ni mambo ya kawaida tu, sasa hilo ndo unaogopa? ha ha ha haaa, usijali. Sasa umenipendea nini mimi labda"

Nilishukuru kuona nimevua samaki bila chambo, basi nikajikuta kiduuuuume.

**************

Siku ziliendelea, lakini mdada yule alikuwa anamjua mwanamke ambaye nilikuwa na mahusiano naye kwa wakati ule. Alikuliza vipi yule ninayekuona naye ni demu wako? NIkamwambia ndio. Sikuona haja ya kumficha kwa sababu naye alisema kuwa ana bwana japo hajamuoa.

Siku moja aliomba tuonane mahala tuzungumze

Siku hiyo tukakutana sehemu tu ya kawaida tukapata kiyepe safi, huku tukipata mawili matatu (mazungumzo). Sikua na amani sana kwa sababu hapakuwa mbali na mtaani maana simjui mumewe anafananaje.

Kumbe mda wote ule jamaa ameshitukia ishu za mke wake kuna mabadiliko flani ameyaona akaanza kufuatilia kimya kimya

ITAENDELEA....................................
 
Yani we ndio pimbi kabisa, yani unaitwa sehemu ambayo unajua kwa asilimia 86 unaenda kupiga mechi halafu eti unajisifia mlikula chips, hivi nyie watoto wa kiume mbona mnatudhalilisha sana sisi WANAUME
Shida mino
 
Yani we ndio pimbi kabisa, yani unaitwa sehemu ambayo unajua kwa asilimia 86 unaenda kupiga mechi halafu eti unajisifia mlikula chips, hivi nyie watoto wa kiume mbona mnatudhalilisha sana sisi WANAUME
Peleka ushamba wako kijijini kwenu huko.. kula chips hakuoneshi wew ni mwanaume au mvulana
 
Yani we ndio pimbi kabisa, yani unaitwa sehemu ambayo unajua kwa asilimia 86 unaenda kupiga mechi halafu eti unajisifia mlikula chips, hivi nyie watoto wa kiume mbona mnatudhalilisha sana sisi WANAUME
Mwanaume unajiita mcheza viduku? Wanao wanajua kama hili ndiyo jina lako au hata watoto huna?
 
Tunaongea na nyie vivulana mnaotegemea kubustiwa na vumbi la kongo, hatuongelei kuhusu watoto wetu wala wazazi wetu ambao hawamo humu
Kama mwanaume unatakiwa uone aibu kujipachika baadhi ya majina. Wewe una tofauti gani na jamaa aliyekua anatumia id ya kike ya gilesi na ya cute love?

Mawazo yako yapo kwenye ngono tu
 
Kama mwanaume unatakiwa uone aibu kujipachika baadhi ya majina. Wewe una tofauti gani na jamaa aliyekua anatumia id ya kike ya gilesi na ya cute love?

Mawazo yako yapo kwenye ngono tu
Ni kitu kizuri sana kama umegundua kuwa mimi ni MWANAUME na sio MTOTO WA KIUME anaetumia vumbi la kongo, imeisha hiyo na tuendelee na mada husika maana inaonekana mmekosa hoja
 
Back
Top Bottom