Yaliyonikuta 2021

Yaliyonikuta 2021

lengo langu lilikua kufanya maisha na sio starehe
Sio kweli.... Na ndio maana unajutia fursa ya mapesa ya dezo dezo..... Mwanamke wa zamani Ana upeo ila pesa Hana.... Sasa hapo kichwa naona kinakuuma, mpya kasepa.

Tafuta pesa kijana. Acha kupenda vya DEZO.
 
Mwishoni mwa mwaka jana muda kama huu nilipata msichana nikafahamiana nae na kufanya nae mapenzi kwa mara ya kwanza na kupata ujauzito.Alinitafuta ili anipe taarifa bahati mbaya sikua hewani kwa siku kadhaa,nakuja pata taarifa tayari ni mwaka mpya 2021 kua ana ujauzito wangu wa wiki kadhaa nikakubali ila sikua na uhakika asilimia zote.Tukapanga siku tuonane tukapima nikajiridhisha ni kweli mjamzito.Siku zikasogea na mapenzi kwake yakaongezeka.

Hatimaye tumbo likawa kubwa(ikatimia miezi 7)akajingua mapacha wakike na kiume bahati mbaya wakafariki kwa muda tofautitofauti nikawa nimepoteza viumbe vyangu nilivyovipenda tokea siku ya kwanza.Baada ya hapo kuna msichana nilifahamiana nae katika harakati zangu mkoani Tabora.Alitokea kunipenda sana na alijitoa kwa kila kitu kwaajili yangu(ana uwezo mkubwa kifedha).Hatukuwahi onana kabla ila alifanya kila kitu kwaajili yangu(nguo chakula,mavazi,etc.).Hatimaye tukaonana nikafanya nae mapenzi bila kutumia kinga kwa siku kadhaa naye akashika ujauzito.

Siku zikasogea na yule mama watoto wa mwanzo aliyejifungua mapacha(kabla ya muda) nikampa tena ujauzito kipindi hicho hicho.Wote wawili wakawa na ujauzito kwa wakati mmoja.Huyu mpya nikawa niko nae sana sambamba ikizingatiwa alikua ananipiga sana kampani nikiwa sina kitu.Tulipanga vitu vingi vya kimaisha ikiwemo kazi na biashara,tulifanya starehe za kila namna.

Siku akaja gundua kuhusu mama wa mwanzo na taarifa zake zote akapata.Akaanza kumsumbua na kumharibu kisaikolojia kua mimi sio mali yake tena hivyo akae mbali na mimi.Ikamuharibu sana yule wa mwanzo kupelekea kuhatarisha ujauzito wake kua hatarini(alipoteza fahamu mara kadhaa).Niliitwa hadi na wazazi wake wajue mustakabali wangu kwa binti yao(aliwaambia kila kitu kuhusu kupata msichana mpya) kama nampenda au nampotezea muda wake tu.Nikakiri nampenda na nitamlinda yeye na ujauzito wake .Nilitumia muda mwingi nikiwa na mpenzi mpya tukifanya starehe na kumsahau wa zamani ingawa wa zamani kimuonekano na kiakili ya maisha yupo vizuri sana.

Siku zikasogea huyu mpya akapata homa kali ikapelekea kupoteza ujauzito wake.Yule wa zamani akapata taarifa na kunipa pole na kusema ye hana tatizo na mimi na yote yaliyotokea ni mipango ya Mungu (ni mti wa dini sana).Huyu mpya akaanza visa na kusema mimi sio mwanaume mwenye msimamo zaidi ya kuendekeza umalaya na uongo uongo hivyo haoni tabu kama tukiishia hapa safari yetu.Tulipanga vitu vingi vya kimaisha lakini hakuna alichotimiza zaidi ya ahadi hewa na kutumia pesa zaidi katika starehe.Nipo katika wakati mgumu sana kwa sasa ikiwemo kukwama kwa mipango yangu mingi ya maisha niliyopanga na huyu mpya ambayo hakuitimiza zaidi ya starehe.

Yule ya mwanzo bado ni mjamzito,ananipenda sana na ana akili sana ya maisha,kanishauri vitu vingi sana toka tufahamiane ila nilimuumiza sana kwa kumpiga tukio la ghafla.Naombeni msaada wenu wa ushauri wenu wana j.f nifanye nini ili niweze kuishi maisha yenye furaha na nitimize malengo yangu na nipige hatua kimaisha!!

Tatizo lako uvivu Na kupenda kulelewa, chukua wazaman, Lea, nenda kafanye vibarua Kwenye majaruba
 
capital inakwama mkuu
Sasa huwezi lalama kuwa umeachwa na mwanamke kisa ya hela zake. Wewe ulipenda hela zake na hilo alitambua nashangaa unalalamika nini, hayo mawazo si bado unayo basi yatumie.

Nina ex wangu aliwahi mlalamikia ex wake kuwa alimshauri kuhusu biashara alafu huyo man baada ya kupata akamuacha. Mi nilimwambia kama unaona mawazo yako yalimfanya atoboe, kwanini nawe usitekeleze ushauri uliompa ukawa na hela kama yeye. Hapo tulizua ugomvi

Hapa unalilia capital wala sio mawazo sijui mapenzi
 
Yote yamepita mzee, kilichopo muoe huyu wa dini na akili za maisha.....

Chondechonde usiwaze wala kumpigia yule mwenye hela eti mrudiane...... Atakupiga na kitu kizito kichwani
 
Mwanaume unapenda mteremko na mserereko wewe.... Yaani unasisitiza kuwa mipango yako mingi haijatimia kutokana na ahadi hewa na starehe za mwanamke mpya.....

Sasa mbona hukumchuna kwa akili?? Haki nacheka Kama mazuri vile??
 
Kwa nilivyoelewa unahitaji mwanamke ambaye yupo njema kiuchumi ndio maana ulivyoachana na huyo mpya imekuuma umeyumba kiuchumi.

Huyo wa zamani unampenda sana shida hana hela ila ndio anakupa furaha ya kweli ndio maana ukashindwa kufanya maamuzi kipindi ulipokua na wote wawili.

Wanaume acheni kupenda mtelezo, vitabu vya dini vimeandika mtakula kwa jasho means wanaume mfanye kazi, mambo ya kudate na mtu kisa ana hela tuachieni sisi jaman(Joke)
Mkuu pambana hela ukizitafuta kwa bidii utazikamata nyingi tu
shos umejua kukomesha lol
 
Sio kweli.... Na ndio maana unajutia fursa ya mapesa ya dezo dezo..... Mwanamke wa zamani Ana upeo ila pesa Hana.... Sasa hapo kichwa naona kinakuuma, mpya kasepa.

Tafuta pesa kijana. Acha kupenda vya DEZO.
 
Marioo ktk ubora wake,
Tafuta pesa kijana wee.
 
Mkifunga shule mnakuwa hamna kazi za kufanya? Homework umemaliza? Leo huendi tuition? nakushauri ungechukua jembe upalilie majani hapo kwenu
 
Wewe ni mjinga na mpumbavu wote tuseme "AMEN"

Kwanza huna sifa ya kuwa baba maana bado una uvulana mwingi, unapenda mtelemko, na huna future yeyote zaid ya kuwaza starehe
future ipo kiunoni mwake.
 
Back
Top Bottom