Yaliyomkuta Rais Bush Irak, yamkuta Rais al Bashir | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yaliyomkuta Rais Bush Irak, yamkuta Rais al Bashir

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Jan 26, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,336
  Likes Received: 22,188
  Trophy Points: 280
  KHARTOUM, Sudan

  MWANAMUME mmoja raia wa hapa ameripotiwa kumrushia kiatu Rais Omar al Bashir akiwa kwenye mkutano katika jengo moja lililopo mjini hapa.

  Walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa hata hivyo Rais al-Bashir alinusurika na askari wa usalama walimkamata mrusha kiatu huyo na kumtia mbaroni ingawa maofisa kutoka ofisi ya Rais al Bashir walikanusha madai ya kiongozi huyo kurushiwa kiatu na badala yake walidai kuwa mhalifu huyo alizuiwa alipokuwa akijaribu kumkaribia Rais huyo.

  Mmoja wa mashuhuda hao ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema kuwa tukio hilo lilotokea jana kwenye ukumbi wa Friendship uliopo mjini hapa ambako kiongozi huyo alikuwa akizungumza na wageni wake.

  Chanzo hicho kimesema baada ya mtuhumiwa kurusha kiatu hicho wanausalama walimkamata na haikufahamika wazi chanzo cha mwanamume huyo kumrushia kiatu Rais huyo.

  Rais Bashir alianza kuitawala Sudan tangu alipotwaa madaraka katika mapinduzi ya kijeshi mwaka 1989 na anatarajiwa kusimama katika kinyangÂ’anyiro cha uchaguzi mkuu wa Aprili mwaka huu Sudan itakapokuwa ikifanya uchaguzi wake mkuu wa kwanza baada ya miaka 24.


  Tukio kama hilo lilitokea Desemba 2008 wakati mwandishi wa habari nchini Irak, Muntazer al-Zaidi, alimrushia kiatu aliyekuwa Rais wa Marekani, George Bush, alipokuwa ziarani mjini Baghdad.
  [​IMG]
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  huyu jinsi ambavyo simpendi ningemrushia hata fuko la mavi sio kiatu...he is killing innocent people in darfur
   
 3. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #3
  Jan 26, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  kampeni za mwaka huu itabidi walinzi wa rais wajuandae mmaana hii piga piga hii..mara berlusconi ,mara mzee mwinyi,mara papa kadandiwa kanzu,...mara jk adandiwa miguu mwanza [kirumba]...mara jk aanguka jangwani,mara jk azimika mwanza [kirumba]..blair apigwa yai viza..,...ni changamoto kwa walinzi wa viongozi...
   
 4. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #4
  Jan 26, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  kazi ipo walinzi wanamitihani kwelikweli
   
Loading...