Wahenga walisema historia hujirudia, yaliyomkuta mtawala wa GALILAYA Mh. Ponsio Pilato ndiyo hayo hayo yamemkuta na mtawala wa wabongo Mh. Jakaya Mrisho Kikwete.
Bahati mbaya kwa Ponsio Pilato hakuwa myahudi ila aliteuliwa tu na Mfalime wa Warumi Mh Kaizari Agustino (Agusto) kwenda Galilaya kutawala wayahudi , mila na desturi za wayahudi maskini ya Mungu alikuwa hazijui yeye alikuwa ni mtawala tu. Ndiyo maana alipopelekewa wafungwa wawili Yesu Kristo toka Nazareti na Baraba toka mjini Yerusalem kwa mjibu wa sheria ya wakati wa Pasaka ili mmoja amwachilie huru, Ponsio Pilato alisoma charge sheet za wote akaona Yesu Kristo Mnazareti hana hata chembe ya hatia ila Baraba alikuwa ni mharifu sugu, alikuwa ni muuwaji, mnyanganyi na mbakaji wa wanawake za watu. Baada ya kuona Yesu Kristo hana hatia Pilato akatafuta njia ya kumwachia na kumwangamiza Baraba, alikuwa na uwezo wa kumwachilia Yesu moja kwa moja bila kutumia njia yoyote ila alijiridhisha njia aliyoibuni ingefanya kazi.
Kwa kuwa Baraba alikuwa ni mharifu sugu kama waharifu sugu ambao kwetu huwa tunajichukulia sheria mkononi ya kuwachoma moto basi Pilato alidhani akiwaambia wayahudi amwachie nani kati ya hao kama sheria ya pasaka inavyosema watasema amwachie Yesu Kristo amsurubishe Baraba kwa kuwa anawasumbua sana , kumbe alijidanganya, hakuamini maskio yake wayahudi wakasema aachiwe Baraba. Kama nilivyosema hapo juu Pilato hakuwa myahudi alikuwa hajui kwamba kwa wayahudi suala la Yesu Kristo kujiita mwana wa mungu na kufanya kazi siku ya sabato ni makosa makubwa sana kuliko ya Baraba kwa hiyo suruhu ni kuuwawa tu. Hesabu za Pilato kumwachia Yesu ndio zikaiishia hapo.
Jakaya Mrisho Kikwete aliwekwa madarakani na wenye pesa, walichangishana wakafanya kila njia haramu na halali wakafaulu kumweka kwenye kiti mtu wao, watu hao wakijiita wana mtandao ni wazi ukiwekwa madarani na watu basi ni lazima ufanye yale wanayotaka, Mh. Kikwete mengi ya waliyotaka afanye yalimshinda kwa kuwa yalikuwa yanaangamiza inchi (rushwa, EPA, Richmundi, mnvua ya mabomu taka Tailand n,k,) Uzalendo ukamzidi akaanza mapema kabisa kujinasua toka kwa wale waliomweka madarakani , Mwanzo kabisa akawakamata akina Basil Mramba, Daniel Yana n,k, pia akawatosa akina Lowassa , Msabaha, Karamagi, Zakia Megji nae akaingia mkumbo huo.
Sasa waliotoswa wakaanza mizengwe wachukue hicho kiti wawo sijui wafanye nini , Kikwete akawa makini baada ya kelele nyingi mtu kama Rostam Aziz yakamshinda akakimbia sasa amebaki Lowassa ni wazi kabisa Lowassa anautaka urais na wakati huo huo Urais hauwezi na Kikwete analijua hilo, sasa Plan A kwa kuwa chombo kikubwa cha maamuzi ndani ya chama kinachotawala ni Halimashauri kuu ya chama chao (yaani NEC) na hatimae kamati kuu yaani (CC) basi hatua ya kwanza ni kuwatosa hawa wanamtandao ambao wanataka kumweka tena mtu wao Lowassa,Mh. Kikwete akabuni mbinu ya kuwatosa wao na wapambe wao kama akina Peter Selukamba, Mery Nagu, Beatrice Sherukindo n,k. kwa kuwa njia yao kubwa ni rushwa mbinu ikawa ujumbe wa NEC upiganiwe wilayani kwani wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya ni zaidi ya 1200, basi kama wao wanajidai wanahela basi wawahonge hao wajumbe wote. Maskini ya mungu kitu ambacho Kikwete hakujua *(kama mwenzie Pilato) wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya asilimia 98 % hawajasoma kwa hiyo hawawezi kutafsiri mbinu au hawakuweza kutafsiri Mbinu ya Mh Kikwete , kwa kutumia wapambe wao wakawanunua kirahisi wajumbe mwisho wa siku wao na wapambe wao wakajikuta wameingia kwenye hicho chombo cha maamuzi kwa hiyo Plan A ya Kikwete ikaishia hapo.
Tofauti na Ponsio Pilato Kikwete amebuni Plan B ambazo ni mbili hizo nina imani atamtosa Lowassa na wapambe wake.
Sasa tusubiri tuone.
EBAEBAN
Tel Aviv.

- Amempendekeza Philipo Mangula awe makamo wa mwenyikiti wa chama kinachotawala ili kusudi wakati ukiwadia wa kuchukua form za kugombea Urais na hatimae kujadiliwa Mangula afanye kazi moja tu ya kukata jina la Lowassa kama walivyokuwa wanakata jina la Malecela.. Mangula kazi hiyo anaweza kabisa kabisa kuifanya kwa macho makavu.
- Wamechelewesha kutaja wajumbe wa kamati kuu, kazi iliyopo hapa ni kupiga darubini ili wapambe wa Lowassa na Lowassa mwenyewe wasiingie katika chombo hiki pia kazi hii Mh. Kikwete anaiweza.
Sasa tusubiri tuone.
EBAEBAN
Tel Aviv.