Yaliyomkuta Ponsio Pilato, yamemkuta na Jakaya Mrisho Kikwete

Hii imetulia
Wahenga walisema historia hujirudia, yaliyomkuta mtawala wa GALILAYA Mh. Ponsio Pilato ndiyo hayo hayo yamemkuta na mtawala wa wabongo Mh. Jakaya Mrisho Kikwete.

Bahati mbaya kwa Ponsio Pilato hakuwa myahudi ila aliteuliwa tu na Mfalime wa Warumi Mh Kaizari Agustino (Agusto) kwenda Galilaya kutawala wayahudi , mila na desturi za wayahudi maskini ya Mungu alikuwa hazijui yeye alikuwa ni mtawala tu. Ndiyo maana alipopelekewa wafungwa wawili Yesu Kristo toka Nazareti na Baraba toka mjini Yerusalem kwa mjibu wa sheria ya wakati wa Pasaka ili mmoja amwachilie huru, Ponsio Pilato alisoma charge sheet za wote akaona Yesu Kristo Mnazareti hana hata chembe ya hatia ila Baraba alikuwa ni mharifu sugu, alikuwa ni muuwaji, mnyanganyi na mbakaji wa wanawake za watu. Baada ya kuona Yesu Kristo hana hatia Pilato akatafuta njia ya kumwachia na kumwangamiza Baraba, alikuwa na uwezo wa kumwachilia Yesu moja kwa moja bila kutumia njia yoyote ila alijiridhisha njia aliyoibuni ingefanya kazi.

Kwa kuwa Baraba alikuwa ni mharifu sugu kama waharifu sugu ambao kwetu huwa tunajichukulia sheria mkononi ya kuwachoma moto basi Pilato alidhani akiwaambia wayahudi amwachie nani kati ya hao kama sheria ya pasaka inavyosema watasema amwachie Yesu Kristo amsurubishe Baraba kwa kuwa anawasumbua sana , kumbe alijidanganya, hakuamini maskio yake wayahudi wakasema aachiwe Baraba. Kama nilivyosema hapo juu Pilato hakuwa myahudi alikuwa hajui kwamba kwa wayahudi suala la Yesu Kristo kujiita mwana wa mungu na kufanya kazi siku ya sabato ni makosa makubwa sana kuliko ya Baraba kwa hiyo suruhu ni kuuwawa tu. Hesabu za Pilato kumwachia Yesu ndio zikaiishia hapo.

Jakaya Mrisho Kikwete aliwekwa madarakani na wenye pesa, walichangishana wakafanya kila njia haramu na halali wakafaulu kumweka kwenye kiti mtu wao, watu hao wakijiita wana mtandao ni wazi ukiwekwa madarani na watu basi ni lazima ufanye yale wanayotaka, Mh. Kikwete mengi ya waliyotaka afanye yalimshinda kwa kuwa yalikuwa yanaangamiza inchi (rushwa, EPA, Richmundi, mnvua ya mabomu taka Tailand n,k,) Uzalendo ukamzidi akaanza mapema kabisa kujinasua toka kwa wale waliomweka madarakani , Mwanzo kabisa akawakamata akina Basil Mramba, Daniel Yana n,k, pia akawatosa akina Lowassa , Msabaha, Karamagi, Zakia Megji nae akaingia mkumbo huo.

Sasa waliotoswa wakaanza mizengwe wachukue hicho kiti wawo sijui wafanye nini , Kikwete akawa makini baada ya kelele nyingi mtu kama Rostam Aziz yakamshinda akakimbia sasa amebaki Lowassa ni wazi kabisa Lowassa anautaka urais na wakati huo huo Urais hauwezi na Kikwete analijua hilo, sasa Plan A kwa kuwa chombo kikubwa cha maamuzi ndani ya chama kinachotawala ni Halimashauri kuu ya chama chao (yaani NEC) na hatimae kamati kuu yaani (CC) basi hatua ya kwanza ni kuwatosa hawa wanamtandao ambao wanataka kumweka tena mtu wao Lowassa,Mh. Kikwete akabuni mbinu ya kuwatosa wao na wapambe wao kama akina Peter Selukamba, Mery Nagu, Beatrice Sherukindo n,k. kwa kuwa njia yao kubwa ni rushwa mbinu ikawa ujumbe wa NEC upiganiwe wilayani kwani wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya ni zaidi ya 1200, basi kama wao wanajidai wanahela basi wawahonge hao wajumbe wote. Maskini ya mungu kitu ambacho Kikwete hakujua *(kama mwenzie Pilato) wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya asilimia 98 % hawajasoma kwa hiyo hawawezi kutafsiri mbinu au hawakuweza kutafsiri Mbinu ya Mh Kikwete , kwa kutumia wapambe wao wakawanunua kirahisi wajumbe mwisho wa siku wao na wapambe wao wakajikuta wameingia kwenye hicho chombo cha maamuzi kwa hiyo Plan A ya Kikwete ikaishia hapo.

Tofauti na Ponsio Pilato Kikwete amebuni Plan B ambazo ni mbili hizo nina imani atamtosa Lowassa na wapambe wake.

  1. Amempendekeza Philipo Mangula awe makamo wa mwenyikiti wa chama kinachotawala ili kusudi wakati ukiwadia wa kuchukua form za kugombea Urais na hatimae kujadiliwa Mangula afanye kazi moja tu ya kukata jina la Lowassa kama walivyokuwa wanakata jina la Malecela.. Mangula kazi hiyo anaweza kabisa kabisa kuifanya kwa macho makavu.
  2. Wamechelewesha kutaja wajumbe wa kamati kuu, kazi iliyopo hapa ni kupiga darubini ili wapambe wa Lowassa na Lowassa mwenyewe wasiingie katika chombo hiki pia kazi hii Mh. Kikwete anaiweza.
Na wale watafutao madaraka kwa nguvu huwa wana mbinu zao kama suala la Faithbird Cox yule wa kwenye kashifa ya Watergate, sitaki kuingia ndani kuhusu hilo ila nina imani wenye akili mmenielewa.

Sasa tusubiri tuone.

EBAEBAN
Tel Aviv.
 
Pontio Pilato na JK sioni kama kuna uwiano.Pontio Pilato alinawa mikono na kuruhusu Wayahudi wafanye vile watavyo kwa Yesu Kisto japo nafsi yake ilimsuta.JK hajakiri kama amepotoshwa na hao akina mtandao.Pilato alikuwa anawakilisha Dola la Rumi ya kale kama mkoloni hakuwa na machungu na Wayahudi,sana sana aliona ni heri kutosa Yesu ili kupunguza ghasia ambazo zingeweza kuongeza ugumu wa kutawala Wayahudi,vile vile kulinda ajira yake vinginevyo Kaisari angempiga chini.
JK ni mwananchi mzawa anaeongoza Watanzania wenzake bila shindikizo la wakoloni bali la watanzania wawe wa mtandao au wengine.Kama Jemedari mkuu na raisi wa Tanzania analo lungu ,mamlaka ya kuchukua maamuzi bila kuyumbishwa na mtu kwani yeye ni kama Kaisari wala sio gavana kama Pilato.Raisi Kikwete amewahi kutamka kuwa uraisi hauna ubia,hivyo sioni kama anayo haja ya kutengeneza zengwe ili kumuadhibu fisadi,wakati yeye ndio kiongozi wa nchi namba mmoja.Mh Lowasa hakataliwi kugombea uongozi,ni haki yake ya msingi,kama atakuwa na mapungufu ni juu ya wananchi wenyewe kuamua kwa busara zao bila shindikizo la mtu au watu au kikundi kwani kura ni ya siri.Lakini hatujakataswa kumchukulia hatua ya kisheria pale ambapo kuna ushahidi wa kujitoshereza.Vinginevyo hatueleweki kumjadili mtu mmoja miaka nenda miaka rudi hapa kibarazani tena ambaye ameishastaafu uwaziri mkuu miaka kibao.Hivi bila Mh Lowasa hakuna Jamii Forum?
 
Pontio Pilato na JK sioni kama kuna uwiano.Pontio Pilato alinawa mikono na kuruhusu Wayahudi wafanye vile watavyo kwa Yesu Kisto japo nafsi yake ilimsuta.JK hajakiri kama amepotoshwa na hao akina mtandao.Pilato alikuwa anawakilisha Dola la Rumi ya kale kama mkoloni hakuwa na machungu na Wayahudi,sana sana aliona ni heri kutosa Yesu ili kupunguza ghasia ambazo zingeweza kuongeza ugumu wa kutawala Wayahudi,vile vile kulinda ajira yake vinginevyo Kaisari angempiga chini.
JK ni mwananchi mzawa anaeongoza Watanzania wenzake bila shindikizo la wakoloni bali la watanzania wawe wa mtandao au wengine.Kama Jemedari mkuu na raisi wa Tanzania analo lungu ,mamlaka ya kuchukua maamuzi bila kuyumbishwa na mtu kwani yeye ni kama Kaisari wala sio gavana kama Pilato.Raisi Kikwete amewahi kutamka kuwa uraisi hauna ubia,hivyo sioni kama anayo haja ya kutengeneza zengwe ili kumuadhibu fisadi,wakati yeye ndio kiongozi wa nchi namba mmoja.Mh Lowasa hakataliwi kugombea uongozi,ni haki yake ya msingi,kama atakuwa na mapungufu ni juu ya wananchi wenyewe kuamua kwa busara zao bila shindikizo la mtu au watu au kikundi kwani kura ni ya siri.Lakini hatujakataswa kumchukulia hatua ya kisheria pale ambapo kuna ushahidi wa kujitoshereza.Vinginevyo hatueleweki kumjadili mtu mmoja miaka nenda miaka rudi hapa kibarazani tena ambaye ameishastaafu uwaziri mkuu miaka kibao.Hivi bila Mh Lowasa hakuna Jamii Forum?

Kwani lazima awe raisi wa nchi hii....?
 
Kwani lazima awe raisi wa nchi hii....?
Uraisi mpaka ujitokeze kugombea,utimize masharti,uchaguliwe na chama husika,ndio ugombee,upigiwe kura ya ndio,kua zihesabiwe na mwisho uchaguliwe,utangazwe mshindi,uapishwe kama Raisi.Bado kuna mchakato wa katiba mpya hatujui hatima yake.Uchaguzi bado mpaka 2015 bado safari ndefu.
 
kama inahusu kuvunjika na kufa kwa ccm ni sawa tuh,na ife tuh ikibid hata leo,,
ccm imeua ndugu zangu wengi sana kwa uzembe wa kutowapa dawa hospitalini,kuwapa dawa fake,kuwalaza chini,kuwanyima elimu,kuwadhulumu na mengineyo yasiyoelezeka,,
ccm mbona inachelewa sana kufa??
 
  • Thanks
Reactions: Ame
[/COLOR]

Nani kakuambia Yuda Eskariote ni msaliti? Kilichomponza huyo YUDA wako ni kule kujiamini sana, kwa sisi tunaopiga dulu za mbali YUDA siyo msaliti hata kidogo ni kule kujiamini kwake kupita kiasi(overconfidence) ndiko kulikomponza Yuda aitwe msaliti mpaka hivi leo hakika hakuwa na nia mbaya kama Mzee Kikwete alivyokuwa hana nia mbaya kwa kubuni Plan B. Ilikuwa hivi, Yuda alikuwa ni mfuasi wa Yesu kwanza alikuwa ni mtoto wa mjini Yerusalem tena alikuwa ni mjanja sana ndio maana akachaguliwa kuwa mtunza fedha wa kikundi cha Yesu. Yuda alikuwa anafuaatana na Yesu kila mahali alikuwa anajionea mwenyewe kwa macho yake ile miujiza mikuu ya Yesu, kufufua watu, vipofu kuona, viziwi kusikia na wenye ukoma kutakata, kwa imani yake na kwa kujiamini kwake katu hakudhani kuna binadamu anaweza kumkamata Yesu, ndio maana wale wayahudi walipomwendea wampe pesa akawaonyeshe Yesu alikubali haraka kwa sababu alijua watashindwa tu kama walivyokuwa wanashindwa siku zote kwa hiyo yeye atachukua pesa za bure, kumbe hakujua ilibidi mtu afe ili neno litimie, Yuda anatufundisha tu tusijiamini sana mfano mtu anakudai hela na ziko bank basi umhahakikishie utamlipa kesho bank zikifunguliwa huwezi jua bank inaweza kuunguwa usiku au watumishi kesho watagoma au bank ikafirisika kama Meridian biao ukashindwa kutimiza ahadi.
Turudi kwenye hoja, hadanganywi mtu hapa, plan B lazima itawatosa hao akina Lowasa wenu , Plan B ni full proof lazima ifanye na haina haja ya kusema mengi.
EBAEBAN
Tel Aviv.

Lakini ujue kuwa Ame ana plan c ambayo itawatosa mafisadi wote huyo mwingine included..Na Plan C inahusiana na plan B yenu ambayo hiyo plan B ndiyo fimbo itagayo gawanya bahari ya Sham ili wana wa ufalme wa pite na ninyi wenye plan B mkjidai kutembea ndani ya bahari kama sisi basi mjue ndilo litakuwa kaburi lenu......Narudia mafisadi mstari umechorwa kati yenu na utawala wa Tanzania hakuna wakuukatiza huo mstari na funguo za Ikulu zipo kwa Ame naye kasha mkabidhi mpakwa mafuta wa bwana kazi kwenu!
 
Kiukweli lowasa ana maamuzi ya haraka kuliko Jmk lakini wote ndio wale wale kwa upande corrupt

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom