Yaliyojiri wakati Rais Magufuli alipokutana na Mabalozi wa Tanzania wanaoiwakilisha taifa nchi za nje

Balozi gani kwenye hicho kilinge angeweza kuuliza alipo Azory Gwanda?

Balozi gani angenyanyua mdomo kusema "tunapata tabu kuitetea nchi huko majuu" kutokana na mambo ya utekaji na ukeketaji wa kucha kwa pliers!

Tusiambukizane ujinga tafadhali.
 
Diplomasia ya kiuchumi 🤣🤣🤣🤣🤣



Mkutano huu ni muhimu sana, Tanzania tunatekeleza diplomasia ya kiuchumi, ila ubalozini tuna waambata wa kijeshi tuu, hatuna waambata wa uchumi!. To be able to move forward, things must change.
P
 
Mkutano huu ni muhimu sana, Tanzania tunatekeleza diplomasia ya kiuchumi, ila ubalozini tuna waambata wa kijeshi tuu, hatuna waambata wa uchumi!. To be able to move forward, things must change.
P

Yap, waambata wa uchumi na biashara ni muhimu, kutafuta wawekezaji na masoko. Kutangaza fursa zilizopo Tanzania.
 
Hongera!
-
Swali, Ni sababu zipi zinapelekea kuwa na mabalozi 40's wakati mataifa yapo 200's?
 
Sekta binafsi bado ambapo ndiyo walipo walipa kodi wakubwa. Mfano mradi wa nyumba za kisasa, Fumba wilaya ya Magharibi tu ndiyo wa Sekta binafsi. Vipi kuvutia uwekezaji ktk viwanda vya kubangua korosho kuongeza thamani na viwanda vya kusindika mazao / soko la uhakika kwa mazao yote ya kilimo, mifugo na uvuvi. Au mabalozi hawatakiwi kuunga mkono juhudi binafsi za wakulima wengi wanyonge na wavuja jasho wa sekta binafsi?

Naona mkazo ni madaraja, reli na barabara . Mikutano ya mabalozi wetu na mwanadiplomasia namba moja (Mh. Rais) na namba 2 (Waziri Mambo ya Nje) inabidi wasikilize maoni yetu pia ili kutanua wigo wa majukumu msingi ya mabalozi wetu nje ya nchi.

Source : Channel ten



Sekta binafsi inabidi isaidiwe, tutoe vikwazo vya biashara, tupunguze urasimu, ukiritimba, rushwa, hata Passport, vibali kama export license iwe unavipata chap chap n.k. Serikali isikilize maoni ya wadau wote.
 
Hongera!
-
Swali, Ni sababu zipi zinapelekea kuwa na mabalozi 40's wakati mataifa yapo 200's?


Nafikiri nia ni kuokoa gharama. Balozi wa UK anaweza kuwakilisha pia Ireland, wa Sweden pia kuwakilisha Norway, Dermark, Iceland,Latvia,

Balozi wa India anaweza pia kuwakilisha Nepal, Mongolia etc.
 
Nafikiri nia ni kuokoa gharama. Balozi wa UK anaweza kuwakilisha pia Ireland, wa Sweden pia kuwakilisha Norway, Dermark, Iceland,Latvia,
Balozi wa India anaweza pia kuwakilisha Nepal, Mongolia etc.
Hivi ikitokea dharura kwenye nchi isiyokuwa na balozi kwa muda huo msaada hutolewa sana sana na Kenya au nchi jirani katika eneo hilo?
 
Sijaelewa kitu hapa. Yaani balozi alete ujenzi wa barabara, kiwanda, daraja nk. Ninaona kama mabalozi hawa wametumwa kwenda kuwa ombaomba kwa niaba ya nchi. Ni hao hao tunaowaita mabeberu siku nyingine na kwamba wasitupangie mambo yetu??? Mbona tunasema vitu hivo tunajenga kwa fedha zetu za ndani??

Imefika wakati tukiri sisi sio nchi tajiri wala hatuwezi kuwa dona kantri - kama balozi anahitajika kuleta miradi ya barabara na madaraja kutoka nchi wanazotuwakilisha.

Tukubali kuwa sisi ni tegemezi na wanafiki!! Inasikitisha!

Kuwekeza sio kuwa omba omba, ni win -win situation. Ni kutangaza fursa, vitu vilivyopo Tanzania. Kuweka mahusiano mazuri na nchi nyingine.

Kwani unafikiri kazi ya balozi ni nini?
 
Yap inategemea na mipango kati ya nchi na nchi. Tuna wawakilishi hadi wazungu wànaoiwakisha Tanzania.
Samahani uniweza nielezea hapa kidogo.

Japo watumiaji wengi wa JamiiForums wanafikiri kila mmoja humu ndani lazima awe mTanzania au African.
 
Miradi miradi miradi.... huyu ni rais au waziri wa miundombinu na usafirishaji?

Kazi ya Rais ni ipi?

Diplomasia, afya, elimu, uwekezaji, biashara, ajira, kutunza amani?kuweka mazingira mazuri ya biashara, kuwalinda wananchi wote, kuinua uchumi wao. No?

Kuna vitu yuko vizuri, mapungufu pia yapo. Nani ni mkamilifu?
 
“Nataka muwe very aggressive, na ukiona mtu anakukwamisha mimi nipo niandikieni uone kama hatakwama yeye, mimi nataka kuona vitu sio maneno maneno” amesisitiza Rais Magufuli.

Hapakuwepo na haja ya kutoa kauli kama hii kwenye hicho kikao, maana hao mabalozi amewachagua mwenyewe na alijiridhisha kwamba wanafaa kabla hajawakabidhi nyadhifa hizo, hivyo misisitizo kama hii kwa upande mwingine inatoa tafsiri ya kwamba ana mashaka na utendaji wao wa kazi.

Halafu anavyosema eti akitokea mtu anayejaribu kuwakwamisha hao mabalozi atakwama yeye, ata deal nao vipi? na je kama ikitokea mtu huyo anayewakwamisha akiwa ni mtu mwenye nyadhifa za juu kwenye nchi husika? mfano labda waziri mkuu wa Japan anaweza akakabiliana nae vipi?

Hii ndio tatizo la kuongozwa na mtu mwenye zero understanding ya masuala ya kidiplomasia hawajui waongee nini na wapi.
 
Ni vipofu tu ndiyo wanapongeza na kusifia kila upuuzi bila ya kutafakari athari kubwa kwa Taifa.
Si vyema kupinga kila jambo, kuna mambo yanafanywa sasa yanafaida na zinaonekana mkuu. Huwezi sema kila kitu hakipo sawa halafu wewe ukawa sawa na kama hulioni hilo basi huenda ndio tatizo lako kuu.
 
Samahani uniweza nielezea hapa kidogo.

Japo watumiaji wengi wa JamiiForums wanafikiri kila mmoja humu ndani lazima awe mTanzania au African.

Unajua tulipopata uhuru tulikuwa hatuna uwezo wa kuwa na wawakilishi kila nchi.

Sehemu zingine tulitumia watu walioishi Tanzania na wenye mapenzi na Tanzania, ingawaje hawakuwa Watanzania (Honorary Ambassadors) Hutuwalipi chochote ila walikuwa kama middlemen.

Mfano hivi USA haina embassy in Iran lakini inaweza kutumia UK embassy kufikisha ujumbe.
 
Kipi bora kwako
Demokrasia au maendeleo?
Wananchi wa kawaida,wanahitaji demokrasia au msendeleo?
Ndugu yangu, demokrasia hats Ulaya imeshindikana!
Ebu tupate maendeleo kwanza, hiyo demokrasia itatukuta njiani

Unajua watu hawajui hakuna demokrasia bila maendeleo.

Kama una njaa utampigia mtu yoyote atayekupa chakula, kama huna elimu, utapiga kula kizembe, bila kufikiria kwa kina sera za kila chama. Mbwembwe, nyimbo, mapambio, kanga, pilau itatosha kuona huyu mtu anakujali.

Kwahiyo ili kupata demokrasia ya ukweli watu kwanzw inabidi wapate basics needs kama chakula, elimu, makazi, afya.

Halafu labda wanaweza kufikiri kwa kina.

Demokrasia inabidi ianze kwanza kuwakomboa watu kiuchumi, kiakili, kielimu, kiafya, hata kiutamaduni, iongeze kwanza uwezo, upeo wao wa kujitambua, kutambua nguvu zao.

Demokrasia iko wapi hapa duniani? Dunia yote inaweza kuamua kitu nchi moja ikapinga (veto).

Africa, bara yote halina sauti kwenye kwenye maamuzi makubwa duniani. South America, India hazina sauti.

Hivi viti vya kudumu kama kweli kuna demokrasia ungewapa walau kimoja Waafrika, Wahindi, Brazil labda kwa South America, na kingine labda to Caribbean.

10 Veto, kwahiyo kwa maslahi ya Afrika, Dunia nzima yangezingatiwa. It would have been better, fair, world system.

USA, kuna tofauti kubwa sana mahakamani, polisi, sheria zinavyowatreat, behave kuhusu maskini na matajiri, weusi na weupe, wanawake na wanaume.

Vitu vyote muhimu watu wachache wale wale wanavidhibiti. Nafasi zote muhimu, vitu muhimu wenye maamuzi ya mwisho ni watu, nchi chache sana zinavidhibiti.

Yemen watoto, (picha chini)watu wanakufa kwa maelfu, njaa imetamalaki, Syria millioni ni wakimbizi , zaidi ya millioni wana ulemavu, Iraq imegawanyika, vipande vipande, libya labda ya miaka 50 itatulia, DRC tumejitahidi ila bado sana (millioni 10 walikufa, dictator wa ukweli walimpa kila support, Mobutu) wizi wa rasilimali zao undaelea.

Wakati huo huo madikteta wa ukweli wanapeta Congo Brazaville, Cameroon, Equtorial Guinea; Saudi Arabia, Oatar, Brunei,etc.

The bottom line is about interest, maintaining power by any means necessary.

They ll leave you alone if do as they tell you. Soft power to nudge if you are cooperating a little bit like bad publicity in the world media. Sanctions, hard power if you don't listen, comply.
Yemen6.jpg
images (1).jpeg
images.jpeg
images (1).jpeg
Yemen6.jpg
 
Mkutano huu ni muhimu sana, Tanzania tunatekeleza diplomasia ya kiuchumi, ila ubalozini tuna waambata wa kijeshi tuu, hatuna waambata wa uchumi!. To be able to move forward, things must change.
P
Inabidi ifike mda tubadilike sasa. Sio kuchua mtu mstaafu na kumuweka awe balozo. Inatakiwa wenye professional za uchumi na biashara wawekwe huko.
 
Inabidi ifike mda tubadilike sasa. Sio kuchua mtu mstaafu na kumuweka awe balozo. Inatakiwa wenye professional za uchumi na biashara wawekwe huko.


Kabisa wawekwe watu makini sana, isiwe kama pension, asante, a favour, kwende kula bata, mvinyo na partying all the time.
 
Duh nimesema nini hapo juu.., ni lini tutaanza kuweka mkazo kwenye kupeleka wawekezaji na sio kuleta wawekezaji ?

Its just the right mentality.., wawekezaji watuletee nini ambacho hatuna na miaka yote hii hatujakipata.., Sisi ni taifa la kuendelea kutegemea wawekezaji, What made them wawekezaji ?

Emancipate yourselves from mental slavery
None but ourselves can free our minds​
serikali inatakiwa kufanya nini ili kupeleka wawekezaji?
Zingatia kuwa wawekezaji wengi ni watu binafsi kama mimi na wewe wenye makampuni yao..
Mimi na wewe tumekwama wapi?
Serikali ifanye nini ili kutengeneza wawekezaji wa kupelekwa nje??
 
Back
Top Bottom