Yaliyojiri wakati Rais John Magufuli akiweka jiwe la msingi katika skuli ya Mwanakwerekwe leo Januari 11, 2020 Zanzibar

Papaa Muu

JF-Expert Member
Nov 6, 2018
234
500
Nawashukuru Wananchi wa Zanzibar kwa Mapokezi makubwa

Ninaipongea Serikali ya Awamu ya Saba kwa Miaka tisa kwa kuiletea Maendeleo Zanzibar

Katika kipindi cha miaka 9 idadi ya wanafunzi imeongezeka katika skuli za Maandalizi kutoka 238 mwaka 2010 nakufikia Wanafunzi 382 kwa mwaka 2018 kwa upande wa Sekondari idadi imefikia Wanafunzi 381 kutoka 299 mwaka 2010

Idadi ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu pia imeongezeka kutoka 767 mwaka 2010 na kufikia Wanafunzi 3,624(2018)

Huduma za afya nazo zimeimarika hasa huduma za kibingwa kwa Magonjwa ya figo na saratani katika Hospitali ya Mnazi Mmoja

Huduma za Usafiri maboresho ya Barabara, Bandari, Manunuzi ya Meli, Ujenzi wa viwanja vya ndege Umeimarisha Uchumi wa Zanzibar

Uchumi unakuwa kwa Asilimia saba Ukichangiwa na Sekta ya Utalii inayochangia asilimia 27 na Kilimo kikichangia asilimia 21.3

Idadi ya watalii kwa mwaka 2018 imefikia laki 520,809 , kutoka Watalii laki 150,000 kwa mwaka 2010

Pato la Taifa limefikia Tilioni 2.874 kwa mwaka 2018 ikiwa sawa naDola za kimarekani 1,024 na kuifanya Zanzibar kukaribia Uchumi wa kati ambao ni sawa na Dola za kimarekani 1040

Skuli ya Mwanakwerekwe imeghalimu shilingi Bilioni 2.628 ambao ni Mkopo wa Dola milioni 35 ukijumuisha na Skuli nyingine hii ikiwa ni zaidi Bilioni 80 kutoka Benki ya Dunia kupitia Mradi wa Kuinua Kiwango cha Elimu Zanzibar

Tuchape kazi tukusanye kodi tulipe madeni haya

Nitashirikiana na Dakta Mohamed Shein na Serikali ya Mapinduzi katika kuhakikisha Mapinduzi Yanadumu na hakuna atakaye yachezea kwakua ndio chanzo cha amani na maendeleo tuliyonayo

Tutunze amani kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom