Kenya 2022 Yaliyojiri Uchaguzi Mkuu wa Kenya: William Ruto ashinda kiti cha Urais, apata 50.49% ya kura

Kenya 2022 General Election
Sidhani. Kenyatta hakuwa anachukiwa kiasi hiki. Wakikuyu ndiyo wamesababisha. Angekuwa ni mkikuyu mwenzao wangempigia kwa wingi. BTW ujue kilichofanya matokeo yawe hivyo ni watu hasa vijana kutojitokeza kwa wingi kupiga kura.
Mkuu, iliyokuwa inachukiwa ni serikali yake na kupanda kwa gharama za maisha, kama ilivyokuwa Tanzania, hakuna mtu anamchukia Samia ila ni hali iliyopo.

Sasa wewe ambaye tunaamini umetuletea maisha magumu leo hii unatuletea mtu na unataka tumuunge mkono umuachie kijiti, huoni kama tutammalizia hasira na tutachagua wa upande wa pili?
Na hao ambao hawakujitokeza kupiga kura pia ni hasira dhidi ya serikali yake, ambayo pona ya Ruto ni ile kuonesha hayupo pamoja nayo.

Uliona hapo mwishoni watu wa Raila wanamlazimisha Uhuru aingilie kati,hapo ndipo walishtuka mtoto wa mjini hayupo nao.

Huu mchezo wa UhuRuto utatumiwa pia na Museveni na kijana wake Kainerugaba.😂
 
Sidhani. Kenyatta hakuwa anachukiwa kiasi hiki. Wakikuyu ndiyo wamesababisha. Angekuwa ni mkikuyu mwenzao wangempigia kwa wingi. BTW ujue kilichofanya matokeo yawe hivyo ni watu hasa vijana kutojitokeza kwa wingi kupiga kura.
Tuliwaambia watu humu Ruto anachukua wakaleta analysis za kitoto.
 
Ruto na Uhuru wamemchezea mchezo mbaya sana Mzee wa watu.
Mzee aliamini sana vya kupewa. Watu wamepandishwa wote ICC halafu waje wagombane na wavunje makubaliano yao hivi tu.

Yani Rais agombane na Naibu wake hadi kufikia kumpa mtu mwingine kazi za Naibu rais na wala asimfanyie figisu kumtoa serikalini? 😂
Raila hakuwa smart tu.
 
hahahaha ndio jibu ambalo linamfanya Uhuru abaki safe na Odinga kuamini hivyo.
Uhuru alitumia nguvu nyingi kumpambania Odinga. Risk iliyokuwepo ni kwamba nguvu zilizotumika zilimuongezea ushawishi Odinga na zingeweza mletea ushindi. Bila kuungwa mkono na state apparatus angepata pungufu ya hapa na au angeibiwa kura.

Hakuna lugha yoyote ya kupindisha, Uhuru alikuwa na Odinga. Kama ungejua mahusiano ya Uhuru na Ruto tangu wanatoka The Hague usingesema haya unayosema
 
Kwamba mkuu unaamini kabisa kwa Afrika yetu hii unaweza kuwa na ugomvi na Rais na ukatoboa?

Kwamba Uhuru angekuwa hataki Wafula atangaze mshindi leo Wafula angefanikiwa kutangaza?

Kama ndivyo basi Uhuru na Jamhuri ya Kenya ni nembo ya utawala bora na darasa kwa Afrika nzima.
Uhuru aliwahi kuwa na kesi ya kuvuruga uchaguzi pale The Hague. Kuwa na kesi ya pili ni risk maana anaondoka madarakani sasa.

Ruto ni mtu tough kakaa kwenye siasa miaka mingi akiwa ngazi za juu. Hata Uhuru angemtoa kwenye chama bado angekuwa tishio kwenye uchaguzi. Labda angemuua kama ambavyo Daniel Arap Moi alifanya kwa wagumu

Wafula Chebukati sio mzembe. Huoni wenzake wakiongozwa na mama waliobebwa kwenye tume na Uhuru walivyojiondoa. Wafula ni mtu mwingine kabisa sio kina Jecha na yule bwege wa "Watanzania wanataka maji, sio blah blah"
 
Mkuu,kwa Afrika yetu hakuna kitu raisi akitaka kufanya anashindwa, akishindwa kisheria basi atakifanya sirini na madhara yatakuwa mabaya zaidi.

Uhuru angeamua hata hao Ruto na Wafula wasingeona huu uchaguzi.
Bado naendelea kuamini na sababu ninazo, UhuRuto kwa mara ya tatu wamemchezea Raila. Huu mchezo wameucheza kisomi sana.
 
Ndio hivyo, Tanzania mambo yakiwa wazi kama Kenya Chama Fulani ndio basi tena. Hizi ni salamu nzuri kwa wapinzani Tanzania
 
Back
Top Bottom