Yaliyojiri: Simba Vs Mbeya City Uwanja wa Taifa VPL 4/3/2017

PROSPER 05

JF-Expert Member
Oct 14, 2013
226
217
Fuatilia Live Update ya Mechi Kati ya Simba Na Mbeya City (Full Time Mbeya city 2 Simba 2)

MPIRA UMEKWISHAA
-Agyei anaokoa vizuri mpira wa kona na kuwa kona tena.Ungeweza kujaa moja kwa moja, inachongwa tena, anaokoa tena Agyei
-Anaingia Semtawa lakini Simba wanaokoa inakuwa konaaa
-Nchimbi anapiga kichwa safi kabisa lakini Agyei
-Zahir yuko chini na City wanaonekana kufurahia sare

-City wanaonekana hawajakata tamaa, Simba halikadhalika lakini umiliki, City wanaonekana kuwa na kasi zaidi
- SUB Raphael Bryson anaenda benchi upande wa City, anaingia Zahoro Pazi
Zimeongezwa Dakika 5
Dk 89, Mavugo anapoteza nafasi nyingine nzuri baada ya pasi safi ya Mo Ibra
Dk 87, Mavugo anaingia, vizuri, mpira unaokolewa na kipa na kona lakini haina madhara kwa City
86 Kichuyaaaa Gooooooooo . Kichuya anaisawazishia Simba kwa Mkwaju maridadi wa Penati.
SUB Dk 85 Kabanda analambwa kadi ya njano kwa kumuagusha Zimbwe
Dk 84 Simba wanapata penaaat baada ya ZImbwe kuagushwa na Kabanda
Dk 80 Gooooooooooo Kenny Aly Mwambungu anawapeleka mbele Mbeya City baada ya Gonga safi ndani ya 18
Dk 76 Simba wanaonekana ni kama waliochoka, upande wa kushoto, Ajibu hakabi wala kuingia ndani ni kama aliyechoka sana. Lakini Semtawa anacheza anavyotaka akiwa anafanya anavyota
Dk 75, Simba wanapata kona baada ya mpira wa Hamadi Juma kuokolewa
Dk 74, Nchimbi anaingia kwa kasi na kuachia mkwaju mkali kabisa, lakini mpira unatoka sentimeta chache pembeni. Ilikuwa hatari
Dk 71, Simba nao wanapoteza nafasi baada ya Mo Ibra kupiga krosi ambayo inamzidi kasi Mavugo
Dk 74, Nchimbi anaingia kwa kasi na kuachia mkwaju mkali kabisa, lakini mpira unatoka sentimeta chache pembeni. Ilikuwa hatari
Dk 71, Simba nao wanapoteza nafasi baada ya Mo Ibra kupiga krosi ambayo inamzidi kasi Mavugo



Dk 70 Raphael anapoteza nafasi nzuri, mpira wake wa kichwa unatoka juu kidogo mwa lango la Simba
Dk 68 sasa, Simba wanaendelea kulishambulia lango la City kama nyuki. Lakini City wanaonekana sasa kuanza kupoteaza muda

DK 65 GOOOOOOO mpira wa adhabu, Ajibu anauchonga kiufundi kabisa na kuandika bao zuri kwa Simba
DK 63 Krosi nzuri ya Kichuya, Mo Ibra na Mkude wanagongana wenyewe
SUB Dk 69, anatoka Ngassa kwa upande wa Mbeya City anaingia Ayoub Semtawa, huyu ni daktari kitaaluma na kati ya wachezaji hatari
DK 63Krosi nzuri ya Kichuya, Mo Ibra na Mkude wanagongana wenyewe
SUB Dk 69, anatoka Ngassa kwa upande wa Mbeya City anaingia Ayoub Semtawa, huyu ni daktari kitaaluma na kati ya wachezaji hatari
Dk 59, Mavugo yeye na lango, baada ya shuti la Mo Ibra kuokolewa, unamkuta Mavugo yeye na lango, anapaishaa buuuuu
Dk 55, krosi maridadi ya Ajibu, inatua kichwani mwa Mavugo lakini anashindwa kulenga lango
SUB Dk 54, Muzamiru anakwenda benchi na nafasi yake inachukuliwa na Mohamed Ibrahim maarufu kama Mo



Dk 52 Kenny Ally naye yuko chini lakini inaonekana kama City wanataka kupunguza makali ya Simba wanaoshambulia mfululizo
Dk 51, nafasi nyingine nzyuri kwa Simba, Ndemla anaachia mkwaju, unaokolewa na kuwa kona, inachongwa, inaokolewa tena kona
Dk 49 Mavugo anabaki yeye na kipa, lakini anashindwa kufunga na mwamuzi anasema tayari aliotea
Dk 48, Simba wanapata kona nyingine, inachongwa na kuokolewa
Dk 47, Simba wanafanya shambulizi kali hapa, Ajibu na Mavugo wanagongeana. Kichuya anaachia shuti kali inaokolewa na kwua kona
Dk 45 Kipindi cha pili kimeanza kwa kasi, Mbeya City wanataka kuongeza bao la pili na kumaliza mchezo, Simba wanataka kusawazisha
MAPUMZIKO
DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 44 sasa, mpira bado unachezwa katikati zaidi, City wakionekana kutaka kuupoza zaidi na Simba wanataka kufunga
Dk 41, Mbeya City wanapata kona na wanaonekana hawana haraka wakitaka kupoteza muda na ikiwezekana kwenda mapumziko na bao moja
Dk 40, Ajibu anamchambua beki mmoja na Mavugo akiwa katika nafasi nzuri, lakini Ajibu anataka kufunga mwenyewe, kipa Owen anaokoa
Dk 40 Ngassa anawachambua vizuri walinzi wa Simba na kumpa Nchimbi, Agyei anaokpa

GOOOOOOO Dk 37, Nchimbi anaukwamisha mpira wavuni kwa mkwaju mkali kabisa baada ya Raphael Alpha kuuacha mpira nyuma na yeye kuuwahiDk 36, Simba kama wanapoteana hasa katika safu ya ulinzi na wanapaswa kuwa makini
Dk 34, Simba wanaichezea nafasi nyingine ya wazi, Hamadi Juma anapunguza na kupiga krosi safi lakini Muzamiru anabutua tuuuuu
Dk 32, Mavugo anaingia vizuri mbele ya Rajab Zahir lakini unaokolewa na kuwa kona. Inachongwa haina madhara kwa City
KADI Dk 29, Kenny Ally analambwa kadi ya njano kwa kushika mpira lakini akaendelea kulalamika
Dk 25, nafasi nzuri kabisa kwa Mbeya City, Nchimbi kashindwa kutulia na kutoa mpira huo


Dk 23, Simba wanapata kona ya pili baada ya mpira aliokuwa nao kichuya kuokolewa. Inachongwa vizuri na kipa Owen Chaimaa anadaka vizuri kabisa
Dk 21, Simba wanapata mpira wa adhabu nje kidogo nje ya lango la Mbeya City lakini pigo la Ndemla halikuwa na jipya
Dk 17, krosi safi ya Shamte na Kenny Ally anaunganisha kichwa safi, unatoka nje kidogo ya lango la Simba. Lilikuwa shambulizi zuri kwa City
Dk 15, krosi safi hapa ya Hamadi, kipa Owen anafanya kazi nyingine nzuri na kuokoa
SUB Dk 13, Mbeya City wanamtoa Sankan Mkandawile aliyeumia na nafasi yake inachukuliwa na John Kabanda
Dk 12, krosi safi ya Mavugo, Kichuya anapiga kichwa lakini kinakuwa laini na kudakwa na Owen


Dk 10, Simba wanaonekana kuendelea kugongena vizuri na kuutawala mchezo, Mbeya City kama wamesinzia hivi
Dk 7, Kotei anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira mguuni mwa Ditram Nchimbi
Dk 5 pasi nzuri ya Ndemla inatua kwa Mavugo lakini ni offside
Dk 4, Zimbwe alikua anaingia vizuri lakini Shamte anatoa na kuwa kona
Dk 3, Simba wanaonekana kuanza kutulia na kuonana kwa pasi za harakaharaka
Dk 1, mechi imeanza taratibu huku kila upande ukionyesha umepania kufanya vizuri

Kwa hisani ya Salehe Jembe Blog
 
Hawa Mbeya City walikuwa na mazingira mazuri ya kushinda game kutokana na mikia wanabweteka na ushindi wa Yanga.
 
Back
Top Bottom