Yaliyojiri: Mkutano wa Mgombea wa CCM, Dr. Magufuli jimboni Chato, Geita - Septemba 20, 2015

MSUKUMA AMCHANA LOWASA:

Mwenyekiti wa CCM Mkoani geita Bw.Joseph Msukuma amemvaa mgombea urais kupitia umoja wa UKAWA, Mhe.Lowasa na wengine waliohamia chadema kwa kusema kuwa anawashukuru kwa kuwa chama kimetua mzigo, hayo aliyasema tarehe 20/09/2015 katika mkutano wa mgombea wa urais kupitia CCM Mhe.JOHN MAGUFULI uliofanyika Mkoani Geita!

Msukuma amesema kuwa wale wote waliondoka CCM walikuwa na mizigo kwa kuwa walikuwa na uchu wa madaraka!Akimuelezea Lowasa,amesema kuwa alikuwa ni rafiki yake mkubwa na siri nyingi juu ya mgombea huyo anazijua.Ameeleza kuwa mgombea wa urais wa CCM anatosha na ndio maana chama kilimbariki na wale wote waliojitoa akil zao hazikuwa timamu!

Aidha alisisitiza kuwa kwa kanda ya ziwa hakuna alie na siri za lowasa kama yeye na kuomba kama kuna anaebisha basi uandaliwe mdahalo maalum ambapo yeye atagharamia kila kitu ili kueleza ukweli.

Je, Lowasa yupo tayari?
Hapa mimi na familia yangu ya watoto 12Magufuri tu!!!!
 
Mkutano wa leo sio tsunami
Wala sio mafuriko

Yaaan hio inaitwa
hakunaga

maana haijapata kutokea tangu uhuru
 

Mke wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth John Magufuli akiwasalimia wananchi wa Chato na kuwaomba ridhaa ya kumchagua mumewe Dkt John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano,kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa wa Oktoba 25 mwaka huu.
Mara bada ya kuhutubia chumba chetu cha habari kilihemewa na simu za wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kuelezea furaha yao sio tu kwa kumuona jukwaani bali pia kwa kuongea kwa kujiamini. Mama Magufuli amekuwa haonekani sana kwa sababu ya kuuguza mgonjwa nyumbani kwao Chato. Wamesema wametiwa moyo sana na haiba ya Mama Magufuli na wameshangazwa kwa uwezo wake mkubwa wa kuongea mbele za watu bila woga na bila kumung'unya maneno.
Mke wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth John Magufuli akiwasalimia wananchi wa Chato na kuwaomba ridhaa ya kumchagua Dkt John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano,kweney uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuwafanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Mke wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth John Magufuli akipeana mkono na Mgombea Ubunge wa jimbo la Chato,Dkt Meedad Kalemani mara baada ya kuwasalimia wananchi wa Chato na kuwaomba ridhaa ya kumchagua Dkt Magufuli kuwa Rais wa awamu ya tano

Wananchi wa Chato wakimshangilia Mama Magufuli kwa shangwe kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa shule ya sekondari Chato mkoani Geita.







 
Back
Top Bottom