Yaliyojiri: Mkutano wa Mgombea wa CCM, Dr. Magufuli jimboni Chato, Geita - Septemba 20, 2015

Lowasa alipokuwa ccm alitukanwa sana na kumwita mchafu, fisadi papa. leo akiwa upinzani amekua msafi, lulu na mtakatifu. hii nayo unaisemeaje? siasa uchwara

Waambie mkuu UKAWA hopeless sana hawa jamaa. Mara waje na barabara za Kenya waseme ni Rwanda, mara picha za Mwigulu akiwa na Slaa na Lipumba kuwa anawanunua kumbe wako kwenye mkutano wa wanasiasa na rais wa Ujerumani alipokuja nchini. Lazima washindwe tu mwaka huu na huyo fisadi wao.
 
Huyu huyu ndo alilazimisha kutua chopa katikati ya watu kule arusha .. shule muhimu sana jamani ... Poleni albino maana matajiri wasiokuwa na elimu ni shidaaa ....

Kwa Msukuma ndio unaweza kujua umuhimu na tofauti ya elimu na hasara ya ujinga.
Ujinga + ... albino = Chopa
 
mwenyekiti wa ccm geita awataka wasukuma na wana kanda ya ziwa kumchaguwa magufuli kwani ni msukuma mwenzao wa kanda ya ziwa , je hii siyo ukanda na ukabila ??

ndo umegundua leo kuhusu ukanda na ukabila? Je upande wapili wa shilingi unauonaje au una makengeza wewe?

Hizi ndo siasa mnazozitaka sikuhizi za kushabikia watu wa kwenu kwa sababu mmejaa tope ndani ya vichwa vyenu kwahiyo vumilia uone mwisho wake.
 
Hakika CCM mnajitekenya na Kucheka wenyewe kwa mtindo huu?

60% ya watu wanaohudhuria mkutano kutazama wasanii kama original commedy,ali kiba,Diamond,Yamotto bend,wema nk,,,
 
Msafara wa mgombea wa urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli ukielekea kwenye uwanja wa michezo Chato maarufu kama Mazaina.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa michezo wa Mazaina Chato tayari kuhutubia wakazi wa Chato.
Umati wa wakazi wa Chato wakiwa wamefurika kwenye viwanja vya mkutano kwa ajili ya kumsikiliza Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Joseph Musukuma na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi na mjumbe wa kamati kuu ya CCM Alhaji Abdallah Bulembo.


Hii ndio meza kuu.
Shilole akitumbuiza kwenye mkutano wa kampeni za CCM Chato
Chege na Temba wakitumbuiza kwenye mkutano wa kampeni za Chato CCM.
Mr.Blue akiwapagaisha wakazi wa Chato kwenye mkutano wa kampeni.


Original Komedi wakitumbuiza wakazi wa Chato kwenye mkutano wa kampeni za CCM.
Joti akipeana mkono na Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli mara baada ya kumaliza kutumbuiza.
Yamoto Band wakitumbuiza kwenye uwanja wa michezo Chato kabla ya kuanza mkutano wa kapeni za CCM.



Khadija Kopa akitumbuiza wakazi wa Chato
Ali Star wa TOT akitumbuiza kwenye jukwaa la CCM Chato wakati wa mkutano wa kampeni za CCM
Fid Q akishusha mistari kwenye jukwaa la kampeni za CCM Chato.
Bushoke akitumbuiza wakazi wa Chato kwenye mkutano wa kampeni za Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
Wakazi wa Chato wakimsikiliza Muwakilishi wa walemavu kwenye mkutano wa kampeni za CCM.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akijinadi na kuwaambia Tanzania mpya itakuwa ya Viwanda.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Chato kwenye mkutano wa kampeni za CCM.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Chato ambapo maelfu ya watu walijitokeza kwa wingi kwenye mkutano.
Umati wa wakazi wa Chato wakimsikiliza Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Maguful
 
Magufuli ndo rais tho nchi itapata misukosuko lakin mwisho wa siku wataelewa tuuuu
 
Hii habari ya jana imechuja. Watu walifuata kuwaona wasanii. CCM Bila ya wasanii ni bure kabisa
 
Magufuli kweli ushashinda, hakuna ubishi kila kona ukipita ni wewe tu, sifa zako tele ndizo zilizokufikisha hapo ulipo.
 
Back
Top Bottom