Yaliyojiri, Matokeo ya maeneo yaliyorudia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa tarehe 21 Disemba, 2014

Wadau..natokea frisha bar tabata.nimefika hapa tabata magengeni vijana wa chadema wamefunga barabara kwa shwangwe.wakifurahia ushindi.nimefunga vioo vyote kwa hofu.hali ni mbaya sana.

Watu kushangilia ushindi ndiyo hali kuwa mbaya? Miccm bana!
 
WATANZANIA WANA ROHO MBAYA. MZEE KIPARA KWA USANII HUU ALIZANI ANGEFIKILIWA JAPO KTK SERIKALI YA MTAA WATANZANIA WAMESEMA TUPA KULE HII MBWA KATILI KWA TEMBO WETU. Duh
Hela zote za kusunguka nchi nzima zingetumika kuboresha sekta ya mifugo. Hiyo ngombe amekonda Sana kutokana lishe hafifu!
 
Kutoka urambo mjini matokeo
ya marudio

mtaa wa stesheni
cuf.....307
ccm....107

mtaa wa block q
cuf ....256
ccm.....223

mtaa wa boma village
chadema ....405
ccm.............97

mtaa wa urambo kati
ccm ....287
cuf......275

mtaa wa majengo ya tabora
cuf...... 407
ccm...... 57

Safi ukawa
 
Kama sikosei uchaguzi pia umerudiwa Temeke Mitaa 10 na Ilala Mitaa mingi zaidi kama 60 hivi. Hakuna mwenye up dates za matokeo ya huko atujuze?
 
Kuna tetesi kuwa mtaa wa Waziri Mkuu Pinda huko Chanika CHADEMA wameshinda. Mwenye taarifa sahihi atuletee!
 
mkuu hiyo ya kusema ccm inakandamiza uislam si kweli , waislam ndio walio nufaika sana na serikali hii. Fuatilia uone tafiti wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya , wakurugenzi ndio kabisa zaidi ya 70% , bodi ya ajira , bodi ya mikopo , bodi ya vyuo vikuu TCU na hata Ghasia yupo pale Tamisemi kwa kufanikisha malengo yao. Waislam wengi walio vyuoni wana mikopo zaidi ya 80% wakati wakristo wengi wanapata mikopo 60%-75% na nyingine wanajiripia wenyewe

anamtania faiza maana wao wanadai kuna mfumo kristo ndo maana anamuuliza
 
Mitaa mingapi ilirudia huko vingunguti?

kata nzima ya vingunguti na maeneo kadhaa ya buguruni
ila nlivyoona ccm watu wameichoka maana nlikua hosp.yani mmama tu wa nyumbani anasema yaani ccm watu tushaichoka na hizo hela walizokula (ESCROW)nkasema kumbe jamani hili saga sio jf tu
 
Katika mwendelezo wa kuwagawia maumivu chama tawala, muungano wa UKAWA umeendelea kukimegua chama kinachokufa cha CCM ambapo katika kata kumi CUF kimefanikiwa kushinda kata nane na chama mwenza katika ukawa yaani CHADEMA kimepata mtaa mmoja sawia na CCM.
kwa matokeo haya kwa sasa chama hiki kikongwe kabisa nchini kinakuwa chama cha upinzani Vinginguti rasmi!!
viva UKAWA!!

Na bado ikiwa watanganyika wameamka hivi itakuwaje kwa Zenj nadiriki kusema mwaka kesho CUF itai-delete ccm Zanzibar completely. Mungu ni mkubwa.
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wakazi wa Mtaa wa Ibungilo B, Kata ya Ibungilo, Wilaya ya Ilemela mkoani hapa, wamekumbwa na hali ya sintofahamu wakati wakijianda kupiga kura ya kumchagua Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, baada mgombea wa nafasi hiyo kupitia CCM kutangazwa mshindi kabla ya wao kupiga kura.

Hali hiyo lisibabisha wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambao walifurika kwenye kituo cha kupigia kura kilichopo Mtaa huo, kupinga matokeo hayo kwa madai kuwa hawajapiga kura iweje matokeo yatangazwe.

Hatua hiyo ilisababisha Polisi kuingilia kati kuwatawanya wafuasi hao kwa kupiga mabomu ya machozi, jambo ambalo lilisababisha wafusi hao kutawanyika sambamba na wananchi waliyojitokeza kupiga kura.

Wakati hayo yakitokea Mbunge wa Ilemela, Highnes Kiwia alimsimika mgombea wa Chadema, Ramadhani Saidi kuwa Mwenyekiti wa Mtaaa huo, kwa madai kwamba ndiye chaguo la wakazi wa Mtaa huo na kwamba hawawezi kuchagulia kiongozi wasiyomtaka.

Kiwia alisema, "Haiwezekani watu wamejitokeza kupiga kura, wanakuta matokeo tayari yamebandikwa, ni jambo la ajabu na lakushangaza watu hawajapiga kura matokeo yanapatikanaje, lazima suala hilo litolewe ufafanuzi wa kina."

Hata hivyo mwandishi wa habari hizi alimtafuta msimamizi wa uchaguzi huo Wilaya ya Ilemela ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wilaya hiyo, Justin Lukaza, na kueleza kwamba matokeo hayo ni sahihi, kwani uchaguzi wa Disemba 14 walishindwa kutangaza matokeo kutokana na tofauti zilizotokea, hivyo leo wameamua kuyatoa.

Akizungumza na mwandishi wa gazeiti hili Katibu wa Chadema tawi la Ibungilo B, Abedi Bulashi alisema kuwa uchaguzi ulifanyika Disemba 14, ulimalizika usiku wa manane, lakini kulitokea kasoro na msimamizi wa uchaguzi huo aliharisha uchaguzi na kupanga kurudiwa leo (jana).

Mmmo ya wananchi yao Daniel Buzuka alisema, "Mimi nilifika asubuhi hapa kituoni kupiga kura, lakini nilishangaa kuona polisi wanakuja na kusema hakuna uchaguzi, huu ni ubabe umetumika na wametunyima haki yetu ya masingi.

Magamba mna kazi kweli safari hii,bado 2015


Chanzo: Mwananchi (Desemba 22,2014)
 
Chadema kufanya vurugu ni kawaida yao kwahiyo hatushangai hata kidogo.
 
Back
Top Bottom