Yaliyojiri kwenye Mkutano wa Lowassa wa kutangaza nia ya kugombea Urais - Arusha

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Wakuu,

Leo ndo ile siku ambayo Edward Lowassa anatangaza nia yake ya kugombea Urais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Mkutano huu umekuwa gumzo katika vyombo vingi vya habari. Mkutano huo unafanyikia katika Jiji la Arusha.

Hivyo basi, Tuendelee kujuzana hapa kinachoendelea katika Uwanja huo wa kumbukumbu wa Sheikh Amri Abeid Karume Arusha, ili hata wale ambao hawana uwezo wa kuona na kusikiliza, wapate nafasi hiyo kupitia hapa.

Vituo vya ITV, Radio one na
East Africa Television (EATV) wapo hewani tayari.

Karibuni.

===========================

Updates;

attachment.php

watu walio hudhulia

=MC wa Shughuli hii ni Ephraim kibonde

=Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Joseph Kasheku (Mzee Msukuma) anaashuka na Helcopter Uwanjani muda huu

=Baada ya Sara kutoka dini ya kiislam na Kikristo, Makada mbali mbali wanatoa salamu.

=Baada ya Kangi Lugola kutoa salamu sasa ni zamu ya Onesmo Olenangoro
=Onesmo Olenangoro anasema Lowassa ni Mwema, Mchapa kazi. Baada ya kuongea anamkaribisha Lowassa.

=Lowassa anasema upigwe wimbo wa sasa kumekucha wa Hayati Komba ambapo amewaambia watu wote waimbe . wacheze na kupiga Makofi.

=Wimbo wa sasa kumekucha haujapigwa baadala yake umepigwa wimbo wa Harambe.

=Lowassa amemuambia DJ amsikilize, anasema kila mmoja asimame dakika moja kumkumbuka Kapt Komba. Kisha DJ apige wimbo wa Sasa Kumekucha. Baada ya Sara DJ kaukosa wimbo. Sasa Lowassa anaendelea kuongea.

=Lowassa anasema kwa Kusoma;

=Leo nimewaita hapa ili kutangaza nia ya kugombea Urais, je mtanipa?

=Mara ya kwa nza niligombea Urais mwaka 1995, mara ya pili ilikua mwaka 2005 lakini nlimuunga mkono Kikwete. na mimi ndo nlikua mwenyekiti wa Kampeni.

=Kilichonifanya nitangaze nia ni hali tete katika nchi yetu.

=Moja ni kisiasa.
Nataka nijenge siasa mpya na kuacha siasa mfilisi ambazo zimejaa chuki wa kila aina.

=Uchumi wa nchi
Vijana wanataka kuona wanapata ajira, Mikopo.


=Wataanzania wanaendelea kuamini kwamba wanaweza pata mabadiliko ndani ya CCM. Nyerere alisema Watanzania wasipopata mabadiliko ndani ya CCm watayatafuta nje ya CCM.

=Uongozi wenye uthubutu, usioogopa kufanya maamuzi magumu

=Mabadiliko yanataka uongozi makini thabiti na usio yumba

=Uongozi wenye ubunifu na upeo mkubwa

=uongozi unaoamini katika shirikisho katika ujenzi

=Uongozi unaozingatia muda

=Angalia, kushangilia kwenu kusimpe sababu ya Mangula Kunishughulikia

=Unapomtafuta Rais ni kutafuta amri Jeshi Mkuu, ni kumtafuta mwenyekiti wa CCM. naamini vigenzo hivyo ninavyo na nkishiriki vita vya Kagera nikiwa kiongozi wa mbele kwenye vita ya Idd Amin. Waulize wengine, walifika Kagera?
Hiyo ndo safari ya matumaini

=DIRA
-Kuimalisha Muungano wetu

-Kushughulikia mambo ya kibaguzi na kikabila

-Kusimamia uchumi

-Kuondokana na sifa mbaya ya Taifa lenye mfumo wa kuombaomba.

-Kujenga mfumo mpya wa Elimu

Hayo nloyaeleza ndio yatakua msingi wangu wa kuongoza nchi.

=Marais waliotangulia wamefanya kazi kubwa sana lakini kuna nafasi ya kufanya zaidi yao

=Nimeamua kugombea ili kupambana na umasikini. tuna Rasilimali nyingi sana

=Uongozi wangu utakua mwanzo wa mchaka mchaka wa Maendeleo.

=Ntaimalisha misingi ya Muungano na kuyaenzi mapinduzi ya Zanzibar

=Kujenga Uzalendo, Uadilifu na Kumaliza rushwa.

=Tumekuwa wajuzi wa kutunga sera bila kuzifanyia kazi. Sera inatungwa Tanzania, Inaenda uganda inahaririwa na kenya na Uganda wanaifanyia kazi. Mimi ntasimamia sera

=Ntadumisha uraia Mwema.

=Ntafanya maamuzi magumu kila inapotakiwa

=Ntaleta mapinduzi ya Viwanda

=Ntakabiriana na Rushwa kwa vitendo sio maneno

=Ntaboresha Masirahi ya Walimu na wafanyakazi wa Sekta ya Umma

=Ntaboresha huduma za afya maji safi na salama.

=Ntawawekea utaratibu mzuri wa Bodaboda, Mama ntilie machinga. Hawatafukuzwa barabarani.

=Kwenye Michezo tumechoka kuwa Kichwa cha mwenda wazimu na washiriki washindwa.

=Kazi yangu ya kwanza itakua kukabiliana na msongamano na ndani ya miezi 12 itakua Historia

=Nauchukia umasikini

=Tuanze pamoja mchakato wa maendeleo. Hii Ndo Safari ya maendeleo.

Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki Afrika Asanteni sana

Toka nimezaliwa sijaonawatu wamejaa namna hii. Asanteni sana.

Watu wanashangilia wakisema Rais..Rais..Rais...!!

Bonyeza hapa Kuisoma Hotuba Edward Ngoyai Lowassa Aliyoisoma

=Josephat Gwajima anasema Lowassa ndiye Joshua wa kutupeleka nchi ya ahadi.

Baada ya hapo anaomba. na Kumtakia kila la heri Lowassa.

=Mzee Kingunge Ngombale–Mwiru anasema;

Nimepewa heshima hii kwa niaba ya wazee wote na watu wanaoitakia mema Nchi ya Tanzania.

=Nimehudhulia mikutano mingi, huu ni wa kipekee, haijawahi kutokea. Inanikumbusha Mikutano ya TANU tukimpokea Nyerere akitokea Newyork

=Nampongeza Lowassa kwa kutangaza nia yake ya kuanzisha mchakato wa kuelekea Ikulu. Lakini pili, nawashukuru sana ninyi nyote sio Arusha peke yake, hapa tumejumuika watanzania, sio bara peke yao wapo Zanzibar pia. Nawashukuru sana.

=Namuunga Mkono Lowassa. Unapozungumzia Rais, unazungumzia Nchi, Unapozungumzia Nchi unazungumzia wananchi.

=Sisi wazee tunaokuja hapa tunaamini huu mchakato unaoanzia hapa unahusu Hatima ya Nchi yetu na Masilahi ya Nchi yetu. na wazee siku zote wanapenda nchi yao iende mbele siku zote kwa usalama na amani. Sasa wako wanaccm wengi ambao nao vilevile watatangaza nia. Na hii ni haki yao kama wanachama wa chama cha mapinduzi na vilevile kama watanzania.

=Lakini kwa kuwa swala la urais ni swala la watu na swala la wananchi, hatima yake lazima wananchi waseme. kwahiyo unapozungumzia vigezo vya wagombea Urais, lazima ulizingatie hilo

=Namshukuru Kikwete, Juzi Dodoma alitamka, katika mchakato wetu tuzingatie kwamba tunaye mtafuta lazima anakubalika ndani ya chama na ya chama. Huo ndo msimamo sahii wa chama tangu TANU na AFRO.

=lakini pia, anayetaka kuwa kiongozi wetu awe na uwezo wa kutuongoza. Lazima tumkabidhi nchi mtu ambaye anajua kuunganisha watu. Awe na uwezo wa kuulea muungano.

= Tunatafuta/wananchi wanatafuta kiongozi ambaye ataweza kukabiliana na tatizo sugu la umasikini wetu. Swala hilindio kubwa kuliko yote. Tazameni nchi yetu. tumejitahidi sana tangu awamu ya kwanza hadi ya sasa na tatizo lipo pale pale. Karibu asilimia 30 ya wananchi wetu wanaishi kwa chini ya dola moja kwa siku. huo ni umasikini wa kutupwa 30% ni watu wapatao mil15.

=Juzi afrika kusini walisema zaidi ya watu 50% wanaishi katika umasikini. anaishi kwa dola moja au tatu wote ni masikini. Jiulize asilimia ngapi wanaishi kwa umasikini.

=Sisi tunaomjua Lowassa na Kazi alizofanya kutatua matatizo katika nchi yetu. Waswahili wanasema Mzigo mzitto mpe mnyamwezi, na mimi nadhani Lowassa ndiye Mnyamwezi wa tatizo letu.

=Katiba yetu inayopendekezwa sura ya pili inasema, Lengo kuu la katiba yetu ni kujenga uchumi wa kisasa kama ndiyo njia kuu ya kuondokana na Umasikini. na kujikita na mapinduzi ya elimu bora na msimo wa Lowassa unajulikana. Mapinduzi ya kilimo ufugaji na uvuvi na ndugu Lowassa hayo ndiyo anayaweza.

=Tunatafuta rais atakaye tuongoza akiwa mwenyekiti wa chama chetu cha CCM. Lowassa anatofauti na wengine kwa sababu ni mtu ambaye amelelwa na chama chetu. Mimi katika nchi hii nmepata heshima kubwa. Nmekuwepo kidogo, nawajua yeye ni wa rika lile la wakina Kinana, Kikwete. Wamepata malezi ya TANU ya Nyerere hadi CCM.
=Nyerere alikua nawaandaa wawe na mafunzo ya kiongozi na kijeshi, wote hao wamepitia. Lowassa ameandaliwa. Hivi karibuni tumeyumbayumba hivi. Nyerere alisema "Mimi nang'atuka, lakini ntaendelea kuamini, bila CCM madhubuti CCM itayumba. Sasa sisi wazee kwa mambo haya ambayo yametokea hivi karibuni tuliingia na wasiwasi. CCM isiyo na Ummoja itasambalatika. Nimelizika na msimamo wa mwenyekiti Kikwete, Msimamo wake ni Murua. Baada ya mikwaluzano ndani ya chama chetu, Yaliyopita si ndwele, tugange yajayo. Tukitaka kuganga yajayo, lazima na ni Muhimu kuwepo mchakato wa Suluhu (reconciliation) wazungumze wapeane mikono. Wakitaka kuwaita wazee wapo. Yupo MZee Mwinyi juzi alikua na miaka 90 lakini bado yupo barabara. Kazi ya wazee ni kusuluhisha. Kuganga yajayo bial Suluhu haya!. Mila zetu na kuitana na kuzungumza.

=Tumeanza safari ya matumaini, lazima twende mpaka kieleweke. Asanteni sana.(anamaliza Mzee Kingunge Ngombale) MC Kibonde anampandisha jukwaani msanii wa kizazi kipya Diamond Platinum. Anasema pia kutakuwepo Dully Sykes Ney wa Mitego. Wanaotumbuza sasa ni Jambo Squad na wimbo wao wa Tukunyema. Sasa hivi kinachofuata ni Burudani.

Asanteni sana kwa kunisoma.

Kwaherini.



 

Attachments

  • lowassa5.jpg
    lowassa5.jpg
    41 KB · Views: 38,293
Last edited by a moderator:
Tukio la lowasa na safari ya matumaini lipo live muda huu EATV&ITV.Leo ndio anatarajia kutangaza nia kuwania kiti cha URAIS.
 
Nikonatazama kuna kamsanii kamoja kapo jukwaani eti kanaoongoza watu kuimba eti LOWASA ndio alijenga chuo kikuu cha dodoma kweli? ina maana lowasa ndio rais ya 2010-2015?

Kweli lowasa ameamua kuwadhihaki marais walioiongoza hii nchi
 
Gwajima alisema Dr.Slaa na Lowasa ni marafiki zake wakubwa pale kawe kwenye mkutano wa Chadema alikuwepo .
 
Nikonatazama kuna kamsanii kamoja kapo jukwaani eti kanaoongoza watu kuimba eti LOWASA ndio alijenga chuo kikuu cha dodoma kweli? ina maana lowasa ndio rais ya 2010-2015?

Kweli lowasa ameamua kuwadhihaki marais walioiongoza hii nchi

Teh Teh dawa ina kuingia tuu..
 
huyu mzee cmwelewi juz alikua mkutano wa mbowe pale tanganyika packer sasa namuona mbele kwenye mkutano wa mh lowasa.

Viongozi wa dini sasa ni aibu tupu, kweli penye uzia tembeza noti
babakomdogo.akitembelea kwenu laxima.atembee.na.mama??
 
Azimio la Arusha II inazaliwa leo: Maadui wakuu watatu wa nchi hii UJINGA, MARADHI na UMASKINI wanakwenda kumalizwa ndani ya miaka 5 ijayo! ... Lowassa atazalisha ajira mpaka za ziada, Huduma za Uhakika ktk ELIMU, AFYA, MAJI, UMEME... Maliasili ya nchi hii itaanza kuwanufaisha Wazawa kwanza...
 
Back
Top Bottom