Yaliyojiri katika Chaguzi Ndogo: Uchaguzi wa ubunge jimbo la Dimani na madiwani Tanzania Bara

Modibo

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
425
700
Leo ndo leo uchaguzi wa ubunge jimbo la Dimani Zanzibar na uchaguzi wa madiwani kata 20 Tanzania bara.

Ni chaguzi zitazotoa mwelekeo na mabadiliko na ukubalikaji wa vyama tangu uchaguzi mkuu wa 2015.

Karibuni tupeane updates na matukio yanayojiri huko.

.......Updates...........

*Uchaguzi wa Ubunge unafanyika kwenye jimbo la Dimani, Wilaya ya Magharibi “B”, Mkoa wa Mjini Magharibi – Zanzibar

Uchaguzi wa madiwani unafanyika kwenye kata Ishirini (20) katika Halmashauri Kumi na Tisa (19) za Tanzania Bara, kata hizo ni.

1. Ngarenanyuki (Meru DC, Arusha),
2. Igombavanu (Mufindi DC, Iringa),
3. Ikweha (Mufindi DC, Iringa),
4. Kiwanja cha Ndege (Morogoro MC, Morogoro),
5. Ihumwa(Dodoma MC, Dodoma),
6. Kijichi (Temeke MC, Dar es Salaam),
7. Kahumulwa (Sengerema DC, Mwanza)
8. Maguu (Mbinga DC, Ruvuma),
9. Ng’hambi (Mpwapwa DC, Dodoma),
10. Kimwani (Muleba DC, Kagera),
11. Kinampundu (Mkalama DC, Singida),
12. Isagehe (Kahama TC, Shinyanga),
13. Kasansa (Mpimbwe DC, Katavi),
14. Duru (Babati DC, Manyara),
15. Malya (Kwimba D.C, Mwanza),
16. Misugusugu (Kibaha TC, Pwani),
17. Mateves (Arusha D.C, Arusha),
18. Nkome (Geita DC, Geita),
19. Lembeni (Mwanga DC, Kilimanjaro) na
20. Tanga (Songea MC, Ruvuma)
--
siyoi koroi, Uchaguzi udiwani Kata ya Ngarenanyuki DED na ccm wapora daftari la wapiga kura.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru Bwana Christopher Kazeri anatembelea vituo akiwa ameambatana na viongozi wa ccm.

Sheria za uchaguzi haziruhusu viongozi wa vyama vya siasa kupiga kambi kwenye vituo vya uchaguzi.

Hii imeweza kutokea Ngarenanyuki tu mkurugenzi wa halmashauri ambaye ni msimamizi wa uchaguzu kutembea na viongozi wa ccm.

mkurugenzi akiwa ameambatana na makada wa ccm wamewanyang'anya mawakala wa vyama daftari lenye majina ya wapiga kura.

Safari ya demokrasia kwa nchi yetu bado sana.
Hii haikubaliki popote.

Tume ya taifa ya uchaguzi kwa mtindo huu huu uchaguzi hauwezi kuwa huru na haki.

--
Francis12, UPDATES MCHAGUZI MDOGO JIMBO LA DIMANI Z'BAR.

Kumetokea mgogoro kati ya mawakala wa CUF na Askari Polisi. Hali hii imepelekea mawakala wa CUF kuondolewa kwa nguvu kwenye vyumba vya kupigia kura na hivyo mawakala wa CCM kubaki peke yao.

Sababu za mgogoro huu ni kama ifuatavyo:

-Mawakala wa CUF amegundua baadhi ya masanduku yamejazwa kura ambazo zimeshapigwa tiki kwa mgombea wa CCM.

-Mawakala wa CUF wamegundua kuwa kuna watu hawamo ndani ya daftari la kupiga kura ila wamekuja kupiga kura na wameruhusiwa kupiga licha ya majina yao kukosekana kwenye daftari.

-Chumba number 6 kituo cha Kibondeni, imegundilikana kwamba masunduku yote yaliyopo yamejazwa kura ambazo zimeshapigwa tayari.

-Wapiga kura wengi jimbo la Dimani ni hewa.

-Police wameanza kupiga watu maeneo ya Fuoni kituo cha Kibondeni baada ya watu hao kudai kuna kura feki kwenye kituo hicho.

-Katika kituo hicho cha Fuoni mabasi yamekua yakisomba watu na kuwaleta kupiga kura. Watu hao si wakazi wa jimbo la Dimani. Picha hapo chini inaonesha moja ya mabasi yanayotumika kusomba watu na kuwapeleka vituoni kupiga kura.


*MABOMU YATAWALA UCHAGUZI WA MARUDIO

*Dereva wa Mbunge Chadema ajeruhiwa, CCM yaongoza Ubunge, udiwani

mtz1UCHAGUZI mdogo wa Jimbo la Dimani, Wilaya ya Magharibi “B”, Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar na ule wa udiwani katika kata 20 Tanzania Bara, umefanyika huku mabomu ya machozi na vurugu vikitawala vituoni.

Kutokana na hali hiyo baadhi ya wananchi walijikuta wakijeruhiwa kwa mabomu na wengine kupigwa na vitu vyenye ncha kali.

Takribani maeneo yote ambapo uchaguzi huo wa marudio ulifanyika jana kuanzia asubuhi mpaka saa 10 jioni vituo vilipofungwa.

Wananchi walikuwa wakijitokeza kwa uchache tofauti na idadi ya watu walioandikishwa kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Kahama

Katika Kata ya Isaghehe Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Jackson Peter ambaye ni dereva wa Mbunge wa Viti Maalimu Chadema, Salome Makamba, alishambuliwa na vijana wasiojulikana na kumkata shingoni na kitu chenye ncha kali.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche (Chadema), alisema dereva huyo alikuwa akiendesha gari aina ya Toyota Land Cruiser yenye namba za usajili T 581 BJB akizungukia vituo vya kupigia kura kwenye kata hiyo, ndipo kundi la vijana lilipozuia gari hilo na kuanza kumshambulia.

“Green Guard wa CCM wameshambulia gari ya mheshimiwa Salome Makamba na kumjeruhi vibaya dereva wake ambae tumempeleka Hospital ya Kahama mpaka sasa hajitambui,” alisema Heche.

Kagera

Katibu Mwenezi wa Jimbo la Muleba Kusini, Hamis Yusuph pamoja katibu wake, Elisha Kabombo (Chadema) wamekamatwa na polisi wakiwa kwenye harakati za kuzungukia vituo vya kupigia kura katika Kata ya Kimwani wilayani Muleba mkoani hapa, huku chanzo cha kukamatwa kwake kikiwa hakijaelezwa.

Taarifa kutoka Kata ya Kimwani kulipokuwa kukifanyika uchaguzi, zilisema viongozi hao walikamatwa wakiwa kwenye harakati za kufuatilia uchaguzi huo katika vituo mbalimbali.

Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kagera Augustine Ollomi hakupatikana jana kuzungumzia hali hiyo, simu yake ya mkononi haikuwa hewani.

Morogoro

kwa upande wa Kata ya Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro, polisi walitawanya watu kwa mabomu katika mitaa ya Lusogo na Ngazengwa hatua iliyochukuliwa baada ya wafuasi wa vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo kuonekana wakiwa kwenye makundi makundi waksubiri.

Katika uchaguzi huo watu waliojitokeza walikuwa wachache tofauti na ilivyozoeleka kwenye chaguzi nyingine.

Arusha

Katika Kata ya Mateves iliyopo katika jimbo la Arumeru Magharibi na Ngarenanyuki-Arumeru Mashariki mkoani Arusha, wananchi waliojitokeza katika vituo vya kupigia kura walikuwa wachache tofauti na ilivyozoeleka katika chaguzi zilizopita.

Katika Kata ya Mateves, upigaji kura ulianza mapema huku kukiwa na idadi ndogo ya wapiga kura.

Akizungumzia hali hiyo mmoja wa wasimamizi wa kituo cha kupigia kura katika kata hiyo ambaye hakuwa tayari kujitambulisha akidai si msemaji, alisema tangu walipofungua kituo chao wananchi walikuwa wakijitokeza ingawa hawakuwa wengi.

Uchaguzi wa Mateves unafanyika baada ya Mahakama kutengua udiwani wa kata hiyo ambapo wagombea waliochuana ni Jeremia Ole Leken (Chadema), Saing’orie Mollel (CCM), Phil Klerruu (NCCR- Mageuzi) na Rashid Daa (CUF).

Na kwa upande wa Kata ya Ngarenanyuki iliyopo Arumeru Mashariki nako hali ya usalama wakati wa zoezi la upigaji kura mpaka mchana usalama na amani viliendelea kutawala katika vituo vingi.

Wakati tukiwa tunakwenda mtamboni taarifa kutoka katika kata hiyo zinaeleza kuwa CCM imefanikiwa kutetea kiti hicho kwa mgombea wake Saing’orie Mollel kuibuka na ushindi dhidi ya wagombea wa vyama vingine.

Dar


Jijini Dar es Salaam pia uchaguzi wa udiwani Kata ya Mtoni Kijichi, waliojitokeza kupiga kura walikuwa wachache ikilinganishwa na uchaguzi uliopita.

Uchaguzi huo unafanyika baada ya aliyekuwa Diwani wa Kata hiyo, Charles Anderson (CCM), kufariki dunia mwaka jana.

Katika Kituo namba nane kilichoko katika ofisi ya Mtendaji wa Mtaa wa Kijichi, wapigakura walioandikishwa walikuwa 475 lakini hadi saa 8:37 mchana waliokuwa wamepiga kura ni 76 tu.

“Mwitikio wa watu ni mdogo sana, mwaka jana muda kama huu (saa 8:37 mchana) ungekuta hapa watu wamejaa, lakini sasa hivi unatuona tunapiga story (tunazungumza),” alisema Ofisa Mtendaji wa Mtaa wa Mtoni Kijichi, Frank Komba.

Uchaguzi Dimani


Katika uchaguzi wa kujaza nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Dimani, wananchi walijitokeza kwa uchache kwenye vituo vingi huku kukiwa na askari wengi waliokuwa wakirandaranda mitaani kwa magari yao.

Katika uchaguzi huo, Chama cha Wananchi (CUF), walilalamika kufanyiwa hujuma kwa mawakala wao kutolewa kwenye vituo vya kupigia kura.

Mkurugenzi wa Uchaguzi CUF, Omar Ali Shehe, alisema kinachofanyika si uchaguzi bali ni ‘utaratibu wa kibabe kwenye kile kinachoitwa demokrasia ya vyama vingi’.

Taarifa hizo za CUF zilisema mawakala sita wa chama hicho na wengine wa vyama vya upinzani, walitolewa nje ya vituo bila sababu za msingi.

CCM


Kwa upande wake Naibu Katibu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alisema chama chao hakihusiki na udanganyifu wowote katika uchaguzi huo.

Alisema mwenendo mzima wa upigaji kura umekuwa huru na wa haki na ndio maana wananchi wanapiga kura bila tatizo .

“Chama chetu kimekua na utaratibu wa kujenga wanachama wake imani na ndiyo maana tunaendelea kuaminiwa kila siku,” alisemai Vuai.

Kauli ya NEC


Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Jaji Hamid Mahmoud Hamid, alisema hakuna mawakala waliotolewa nje ya vituo vya kupigia kura na kwamba taarifa hizo zinazosambazwa ni uzushi.

“Kama kuna mawakala wametolewa nje basi itakua wana makosa na ndio maana huenda ikawa wametolewa. Wapo baadhi ya mawakala nimepewa taarifa walikua wanazungumza na simu kwenye vituo kitu ambacho hawakutakiwa kufanya hivyo,’’ alisema Hamid.

Habari hii imeandaliwa na Na Muhammd Khamis (UoI) Zanzibar , ELIYA MBONEA, Arusha na Nora Damian, Dar

==========

MATOKEO YA AWALI

==========

Jimbo la Dimani Zanzibar

image.jpeg


CCM YASHINDA VITI VYA UDIWANI MUFINDI

Msimamizi wa uchaguzi wa halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ametangaza matokeo ya uchaguzi mdogo wa kata mbili za Ikweha na Igombavanu zote zikiwa jimbo pacha la Mufindi kaskazini, ambapo matokea yanaonesha kuwa chama cha mapinduzi CCM kimefanikiwa kutetea viti vyote viwili katika kata hizo.

Taarifa ya msimamizi wa uchaguzi kupitia kitengo cha habari na mawasilino cha halmshauri ya wilaya ya Mufindi, zinaonesha kuwa, katika kata ya Ikweha jumla ya watu waliokuwa mejiandikisha kupiga kura walikuwa elfu 03 mianane 11, (3811) waliojitokeza kupiga kura ni elfu 02 miatatu na 07, (2307) ambapo mgombea wa CCM Bw.Albeto Chaula amepata kura elfumoja mianne na 05 (1405) sawa na asilimia 61% mgombea wa CDM Bw Ayubu Masika amepta kura mianane na 77(877) sawa na asilimia 38% huku mgombea wa CUF Bw. Meshack Manga akipata kura 25 sawa na asilimia 1%.

Taarifa hiyo imeainisha pia matokeo ya kata ya Igombavanu, ambapo waliojiandikisha kupiga kura walikuwa elfu 03 miambili 83 (3283) wakati kura zilizopigwa zilikuwa elfu 02 na 27(2027) kati ya hizo mgombea wa CCM Bw. Rashid Mkuvasa wamejikusanyia kura elfu moja miambili 83 (1283) sawa na asilimia 63% huku mgombea wa CDM Bw.Scholar Mitimingi amepata kura miasaba na 44( 744) sawa na asilimia 37%.

Katika uchaguzi huo jumla ya kura 64 zimekataliwa ambapo Ikweha ni kura 36 na Igombavanu kura 28. Aidha, zoezi la uchaguzi katika kata zote mbili lilikuwa la amani na utulivu.

Uchaguzi wa kata hizo, uliitishwa na tume ya taifa ya uchaguzi baada ya kufariki kwa waliokuwa madiewani wa kata hizo mbili kupitia chama cha mapinduzi CCM ikiwa ni miezi michache baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

KILICHOIANGUSHA UKAWA UCHAGUZI WA MARUDIO HIKI HAPA


UCHAGUZISIKU moja baada ya kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Dimani visiwani Zanzibar na udiwani katika kata 20 za Tanzania Bara, mengi yameibuka ikiwamo kutajwa kwa sababu ya kuangushwa kwa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) dhidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Wasomi, wanasiasa mbalimbali nchini wamezungumzia hatua ya kushindwa kwa Ukawa, huku baadhi ya vyama vikitaka kufanyika kwa mabadiliko na kuwapo tume huru ya uchaguzi.

Katika uchaguzi huo mdogo, vyama vya upinzani vimegaragazwa vibaya.

Katika Jimbo la Dimani, mgombea wa CCM, Juma Ali Juma aliibuka mshindi kwa kura 4,860 huku mpinzani wake wa CUF, Abdulrazak Khatib Ramadhan akipata kura 1,234.

Wakati CCM ikiibuka na ushindi wa kata 19 za udiwani, Chama cha Demokrasisa na Maendeleo (Chadema), kimefanikiwa kutetea kiti chake katika Kata ya Duru mjini Babati, huku Chama cha Wananchi (CUF), kikiambulia patupu baada ya kushindwa pia kutetea kiti chake cha Kimwani wilayani Muleba mkoani Kagera.

Hata hivyo, wachambuzi wa masuala ya siasa wamesema mara nyingi mshindi wa uchaguzi mdogo huwa ni wa chama kilichokuwa madarakani katika eneo husika, na kwamba vyama vya upinzani havina nguvu vijijini kama ilivyo CCM.

Mtaalamu na mchambuzi wa masuala ya siasa, Profesa Gaudence Mpangala wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCO), alisema vyama vya upinzani vina nguvu mijini kuliko vijijini, hivyo ilikuwa vigumu kwao kushinda uchaguzi huo.

“Hadi sasa CCM ina nguvu sana vijijini na haya ni matokeo ya Baba wa Taifa, Julius Nyerere kukiimarisha chama zaidi kwenye ‘grassroots’ (ngazi za chini) na uhalisia ni kwamba upinzani wana nguvu zaidi mijini japo si miji yote,” alisema Profesa Mpangala.

Alisema ushindi katika uchaguzi mdogo huwa ni wa chama kilichotawala katika eneo husika na kwamba licha ya kwamba CUF ina nguvu Zanzibar, lakini kwa upande wa Unguja CCM ndiyo wana nguvu kwani hata mbunge wa Dimani alikuwa wa chama tawala.

Kutokana na hali hiyo, alisema matokeo hayo hayawezi kutumika kuonyesha kwamba wananchi wanaukubali uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano na badala yake ni matokeo ya mfumo wa siasa uliopo tangu miaka ya nyuma.

Akizungumzia uchache wa wapigakura waliojitokeza kwenye uchaguzi huo, alisema kwa kawaida uchaguzi mdogo huwa hauna hamasa kubwa kama ilivyo kwa Uchaguzi Mkuu.

Dk. Bana na udhaifu


Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Benson Bana, alisema ushindi waliopata CCM ni dhahiri kwamba upinzani umekwisha nguvu.

Alisema ushindi huo ni njia mojawapo ya mwaka 2020 kwa CCM kuwa na njia nyeupe ya kushinda uchaguzi bila upinzani kupata viti.

Dk. Bana alisema CCM bado ina nguvu, wananchi bado wa imani na ni ushahidi tosha Ukawa wameishiwa nguvu.

“Nilitegemea baada ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 Ukawa wangejipanga na kusajili chama kimoja, lakini wameshindwa kufanya hivyo basi wataendelea kugawana kura.

“Tatizo la Ukawa kwa sasa pia ni kushindwa kufanya kazi na matokeo yake wanamkumbatia mtu mmoja aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

“Lowassa kwa sasa ana mvuto yeye ndani ya Ukawa na sio Ukawa kuwa na mvuto na wananchi na mbaya zaidi hawawezi kufanikiwa kutokana na mparaganyiko uliopo kati ya Zanzibar na Tanzania Bara,’’ alisema Dk. Bana.

Dk. Lwaitama

Dk. Azaveli Lwaitama, alisema ni vigumu kusema CCM imeshinda ikiwa hakuna tume huru ya uchaguzi.

Alisema bila tume huru CCM itaendelea kushinda uchaguzi kwani imekuwa ikisaidiwa na dola.

“Katika hali ya kutokuwa na tume huru ya uchaguzi, mtu utaamini vipi kile kinachotangazwa ili ujue kweli kulikuwa na ushindani.

“Kwa hali kama hii ambayo Jeshi la Polisi linaenda kutanda kwenye jimbo la uchaguzi kama ilivyokuwa Dimani, lazima CCM iendelee kutawala, wala hatutafikia walipo wenzetu Kenya ambako chama kikishindwa kinakubali,” alisema Dk. Lwaitama.

UVCCM yatamba


Akizungumzia matokeo hayo, Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Shaka Hamdu Shaka, alisema ushindi walioupata unaonyesha taswira njema kwa chama hicho tawala kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Alisema wamepokea ushindi huo kwa faraja na umeonyesha dhahiri CCM itaendelea kufanya vizuri kwenye kila uchaguzi kwani kwa sasa Watanzania hawajaona chama mbadala wa kushindana nayo.

Kaimu Katibu Mkuu huyo, alisema CCM ni chama makini na Watanzania wanakiamini pamoja na viongozi wake na ndiyo moja ya sababu iliyowafanya kukipa ushindi wa kishindo.

“Hakuna wa kuzuia nguvu ya CCM, tutaendelea kushinda kwa kuwa ni chama chenye demokrasia ya kweli na kimefanya uchaguzi huo kwenye uhuru, amani na ndiyo maana hata wananchi wanakikubali. Na hiyo ni ishara tosha kwamba mwaka 2020 wataisoma namba kweli kweli,’’ alisema Shaka.

Tundu Lissu

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), jana alizungumzia uchaguzi huo kupitia andiko lake na kusema matokeo hayo hayakishangazi chama, na kwamba hawana sababu ya kushangilia wala kuomboleza kwani imekuwa ni kawaida kushindwa kwenye uchaguzi mdogo.

Alisema imekuwa ngumu kushinda uchaguzi mdogo na kwamba historia inaonesha kuwa licha ya kushindwa kwenye uchaguzi huo, lakini hufanya vizuri zaidi kwenye Uchaguzi Mkuu unaofuatia.

Lissu alisema hawajapoteza kitu katika uchaguzi mdogo kwani hawajafanikiwa kuchukua kata za CCM na wala wao kunyang’anywa za kwao.

“Uchaguzi mdogo wa ubunge au udiwani ni mgumu sana kushinda katika mazingira halisi ya nchi yetu. Mifano michache inathibitisha ukweli huu. Katika ‘election cycle’ (mzunguko wa uchaguzi) ya 2005-2010 tulishinda Jimbo la Tarime, lakini tukapigwa Biharamulo Magharibi na Busanda.

“Tarime lilikuwa jimbo letu tangu Uchaguzi Mkuu wa 2005, Busanda lilikuwa la CCM na Biharamulo Magharibi lilikuwa la TLP.

“Sikumbuki vizuri kama tulishinda kata hata moja katika mzunguko wa uchaguzi wa kipindi hicho,” alisema Lissu na kuongeza:

“Hatujanyang’anywa iliyokuwa yetu (kata/jimbo), hatujanyakua zilizokuwa zao. Hata hivyo, funzo kubwa zaidi la historia ya uchaguzi huu ni kwamba licha ya kupigwa kwenye uchaguzi mdogo, tumeendelea kufanya vizuri zaidi katika kila Uchaguzi Mkuu uliofuatia kipigo cha uchaguzi mdogo,” alisema Lissu.

Mtatiro na mgogoro

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa CUF ambaye hatambuliwi na Msajili wa Vyama vya Siasa, Julius Mtatiro, hakutofautiana sana kimtazamo na Lissu.

Alisema kuwa huwa ngumu kwa upinzani kushinda huku akimtupia lawama Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba, kuivuruga Ukawa.

Alisema haoni uhusiano kati ya matokeo hayo ya uchaguzi mdogo na utendaji wa Serikali, kwani imekuwa kawaida CCM kushinda kwenye uchaguzi mdogo kutokana na kutumia nguvu nyingi za rasilimali na dola.

Alibainisha kuwa kulikuwa na uwezekano wa upinzani kushinda kata saba kama ungeungana, huku akikitaka Chama cha ACT-Wazalendo kufikiria kujiunga Ukawa.

CCM kufunguka leo


MTANZANIA ilipomtafuta Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole kuzungumzia uchaguzi huo, alisema asingeweza kuzungumza na badala yake chama hicho kitazungumza leo.

“Ilikuwa tuzungumze leo (jana), lakini tumeona ni vema kwanza tumpe nafasi Rais Dk. John Magufuli na ugeni wake (Rais wa Uturuki),” alisema.

Vijana CUF

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Jumuia ya Vijana wa Chama cha Wananchi (JUVICUF), Hamidu Bobali, alisema kuwa sasa umefika wakati wa Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage kujitafakari kwa yaliyotokea.

Alisema katika zama za demokrasia haiingii akilini katika uchaguzi mdogo Jimbo la Dimani, kusiwepo na kura hata moja iliyoharibika.

Alisema kwa sasa vita iliyopo ni kubwa ya vyama vya upinzani, hivyo vinapaswa kuelekeza nguvu zake katika kudai tume huru ya uchaguzi na Katiba mpya.

Bobali ambaye pia ni Mbunge wa Mchinga, alisema bila kuwa na tume huru ya uchaguzi, CCM ni ngumu kuiondoa madarakani kwa kuwa tayari imejitengenezea ushindi kabla hata ya kuingia katika masanduku ya kura na kupiga kura.

“JUVICUF tunapenda kuutangazia umma kuwa ni wazi sasa vita kubwa ya vyama vya upinzani inapaswa ielekezwe katika kudai Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, katika hili JUVICUF kutoka sasa tutakuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha tume huru inapatikana,” alisema Bobali.

Aliongeza kuwa mawakala wao walitolewa nje kutokana na msimamizi wa uchaguzi kutumia daftari jingine kinyume na lile ambalo lilitolewa na Tume ya Uchaguzi kwa mawakala wote.

Akizungumzia uchaguzi wa madiwani, alikiri udhaifu kutokea kutokana na mgogoro unaoendelea ndani ya chama hicho.

Bobali alisema kuwa CUF ilikuwa na uwezekano wa kushinda kata zaidi ya nne ambazo ni Kimwani ambayo walikuwa wakiitetea, Kiwanja cha Ndege, Nkome na Malya.

Chanzo: Mtanzania
 
Mkuu hebu tuwekee kata zinzofanya uchaguzi wa madiwani nchini ili iwe rahisi kufuatilia kwa karibu.
 
Habari wakuu,

Leo ndio chaguzi ndogo za udiwani, zinafanyika baadhi ya maeneo mbali mbali hapa nchini hivyo tujuzane yanayoendelea kwenye maeneo husika yanayofanya uchaguzi bila kusahahau uchaguz wa DimaniZanzibar.
 
Mkuu yupo tayari kutoa executive order. Poilis wapotayar kutii, tume imetia macho kwa mshangao
 
UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE JIMBO LA DIMANI - ZANZIBAR NA MADIWANI KATIKA
KATA ISHIRINI (20) KWENYE HALMASHAURI KUMI NA TISA (19) ZA TANZANIA BARA TAREHE
22 JANUARI, 2017


Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawatangazia
wananchi wote wa Jimbo la Dimani, Wilaya ya Magharibi “B”, Mkoa wa Mjini
Magharibi – Zanzibar na Kata Ishirini (20) katika Halmashauri Kumi na Tisa (19)
za Tanzania Bara kuwa Uchaguzi Mdogo wa Ubunge wa Jimbo hilo na Madiwani katika
Kata hizo utafanyika siku ya Jumapili tarehe 22/01/2017. Kata hizo na
Halmashauri na Mikoa kwenye mabano ni Ngarenanyuki (Meru DC, Arusha), Igombavanu
na Ikweha (Mufindi DC, Iringa), Kiwanja cha Ndege (Morogoro MC, Morogoro), Ihumwa
(Dodoma MC, Dodoma), Kijichi (Temeke MC, Dar es Salaam), Kahumulwa (Sengerema
DC, Mwanza) Maguu (Mbinga DC, Ruvuma), Ng’hambi (Mpwapwa DC, Dodoma), Kimwani (Muleba
DC, Kagera), Kinampundu (Mkalama DC, Singida), Isagehe (Kahama TC, Shinyanga),
Kasansa (Mpimbwe DC, Katavi), Duru (Babati DC, Manyara), Malya (Kwimba D.C, Mwanza), Misugusugu
(Kibaha TC, Pwani), Mateves (Arusha D.C, Arusha), Nkome (Geita DC, Geita),
Lembeni (Mwanga DC, Kilimanjaro) na Tanga (Songea MC, Ruvuma) na utaratibu utakuwa kama ifuatavyo:-
 
Kata 20 zinazorudia uchaguzi ni;
1. Ngarenanyuki (Meru DC, Arusha),
2. Igombavanu (Mufindi DC, Iringa),
3. Ikweha (Mufindi DC, Iringa),
4. Kiwanja cha Ndege (Morogoro MC, Morogoro),
5. Ihumwa(Dodoma MC, Dodoma),
6. Kijichi (Temeke MC, Dar es Salaam),
7. Kahumulwa (Sengerema DC, Mwanza)
8. Maguu (Mbinga DC, Ruvuma),
9. Ng’hambi (Mpwapwa DC, Dodoma),
10. Kimwani (Muleba DC, Kagera),
11. Kinampundu (Mkalama DC, Singida),
12. Isagehe (Kahama TC, Shinyanga),
13. Kasansa (Mpimbwe DC, Katavi),
14. Duru (Babati DC, Manyara),
15. Malya (Kwimba D.C, Mwanza),
16. Misugusugu (Kibaha TC, Pwani),
17. Mateves (Arusha D.C, Arusha),
18. Nkome (Geita DC, Geita),
19. Lembeni (Mwanga DC, Kilimanjaro) na
20. Tanga (Songea MC, Ruvuma)
 
Wakuu leo ndiyo Ile siku ya kujua kama rais Magufuli ama anapendwa ama Tayari raia washamchoka. Tupia hapa kinachojiri katika zoezi la upigaji kura na matokeo, na vipi mwitikio wa wananchi
 
Uchaguzi wa Jimbo la dimani hadi sasa ni machafuko matupu, mawakala wa cuf wametolewa kwenye vyumba vya kupiga kura kwa sababu ya KUGUNDUA na KUHOJI mambo yafuatayo:

Wamegundua baadhi ya masanduku yamejazwa kura ambazo zimeshatiwa tiki kwa mbunge wa ccm

Wamegundua kuwa kuna watu hawamo ndani ya daftari la kupiga kura ila wamekuja kupiga kura na walipo pinga MAWAKALA WETU, (kaa Mujib wa Sheria na Kanuni za Sheria za Uchaguzi) JESHI LA POLISI waliwakunja na kuwatoa Nje

Chumba number 6 imegundilikana kwamba masunduku yote yamejazwa kura

MAPANDIKIZI NI MENGI YAKILINDWA NA KUSINDIKIZWA NA JESHI LA POLISI.

Mazombi waanza kupiga watu maeneo ya fuoni kituo cha kibondeni
 
Anaandika Nizzoh Afrika Mwanaharakati

Kumetokea mgogoro kati ya mawakala wa CUF na Askari Polisi. Hali hii imepelekea mawakala wa CUF kuondolewa kwa nguvu kwenye vyumba vya kupigia kura na hivyo mawakala wa CCM kubaki peke yao.

Sababu za mgogoro huu ni kama ifuatavyo:

-Mawakala wa CUF amegundua baadhi ya masanduku yamejazwa kura ambazo zimeshapigwa tiki kwa mgombea wa CCM.

-Mawakala wa CUF wamegundua kuwa kuna watu hawamo ndani ya daftari la kupiga kura ila wamekuja kupiga kura na wameruhusiwa kupiga licha ya majina yao kukosekana kwenye daftari.

-Chumba number 6 kituo cha Kibondeni, imegundilikana kwamba masunduku yote yaliyopo yamejazwa kura ambazo zimeshapigwa tayari.

-Wapiga kura wengi jimbo la Dimani ni hewa.

-Police wameanza kupiga watu maeneo ya Fuoni kituo cha Kibondeni baada ya watu hao kudai kuna kura feki kwenye kituo hicho.!
 
Back
Top Bottom