Yaliyojiri: Kesi ya Mh. Lissu ya 'Dikteta Uchwara' - Agosti 28, 2017

Wakuu nipo mahakamani Mbele ya mheshimiwa Godfrey Mwambapa. Tunasikiliza Kesi ya Mheshimwa Tundu Lissu inayohusu Udikteta Uchwara. Nipo na Mr. Maxence Melo nafikiri naye ana kesi leo hapa Mahakamani.

Nitawajuza zaidi kinachojiri.

Tuko na shahidi fundi mwashi anataja maneno halafu anayakana...

======

UPDATES:

Wakuu, leo kunakesi inaendelea ya Mwanasheria wa CHADEMA na rais wa TLS Mheshimiwa Tundu Lissu.

Leo kwenye hii kesi amekuja shahidi mmoja wa Upande wa Jamhuri aitwaye Timoth Albert Enekea, ana mika 44 na ni Mkristo.

Shahidi baada ya kula kiapo mbele ya Mahakama, moja kwa moja anaanza kuulizwa Maswali.

Wakili wa Serikali anamuuliza Shahidi;.

Wakili Tutajie unajishughulisha na nini na tuambie ilimu yako.

SHAHIDI: Mimi najishughulisha na Shuguli za za ujenzi na fundi uashi. Shughuli nazifanyia maeneo mbalimbali na hii kazi nmeifanya kwa miaka ishirini.

Elemu ni darasa la saba ila Kuna wazungu walikuja kutoa msaada kwaajili ya kuwaendeleza vijana kazi za ufundi. Nami nlikiwa mmoja wa hao vijana.

Wakili wa Serikali: Tarehe 28/6/2016 ulikiwa wapi?

SHAHIDI: Nlikuwa hapa mahakamani kumdhamini mfanyakazi mwenzangu, hapa mahakama ya kisutu dar es salaaam

Wakili wa Serikali: Lengo la kumdhamini lilifikaje kwako, ulifanikiwa kumdhamini?

SHAHIDI: Majira ya saa tano nilifanikiwa kumdhamini

Wakili wa Serikali: Baada ya kufanikiwa kumdhamini nini kiliendelea?

SHAHIDI: Baada ya kufika nje tukawa tunajadiliana nje ya mahakama na nliyekuja kumdhamini nikimwambia kwamba hii kesi haiwezi kukudhuru, baada ya hapo nikaona umati mkubwa wa wananchi, wakiwa na wanandishi wa habari akiwemo Tundu Lissu ambaye alikuwa anaongea. Kauli za Tundu Lissu alizokuwa akizitoa mimi mwenyewe sikupendezwa na zile kauli.

Wakili wa Serikali: Maneno gani uliyoyasikia?

SHAHIDI: Maneno nliyoyasikia japo sio kwa ufasaha ni Rais Magufuli ni rais uchwara na rais dikteta, watanzania wenzangu tusipokuwa makini tunaingia kwenye giza nene, Hatupaswi kumuunga mkono.Baada ya kusikia maneno hayo Sikujisikia vizuri kusikia maneno hayo, kwakweli mimi nlisogea pembeni, sikupenda kuendelea kusikiliza.

Wakili wa Serikali: Je ukimuona Tundu Lissu unaweza kumtambua?

SHAHIDI: Ndio(ameenda na kumshika bega.. Huyu hapa)

Wakili wa Serikali amemaliza kumuuliza Maswali, anayefuata kumuuliz maswali ni Peter Kibatala. Peter Kibatala ni Wakili anaye mtetea Tundu Lissu kwenye hii Kesi.

Kibatala: Mwenyekiti wako wa kata anaitwa nani?

SHAHIDI: Hakuna ninayemfahamu

Kibatala: Kiongozi gani wa CCM unayemfahamu..

SHAHIDI: Hakuna
KIbatala: Unaishi wapi?

Shahidi: Naishi Goba Kinzudi

Kibatala: Kiongozi wa Serikali ya mtaa wako anaitwa nani?

SHAHIDI: Tangu nihamie kule hakuna ninayemfahamu, nmekaa sasa mwaka mmoja na zaidi

Kibatala: Wakati unamdhamini huyi ndugu yako ulikuwa unaishi wapi?

SHAHIDI: Kinzudi

Kibatala: Wakati haya maneno yanatamkwa, kiongozi wako wa mtaa alikuwa anaitwa nani?

SHAHIDI: Sikumbuki Jina.

Kibatala: Ulivyokuja kumdhamini mtu, uliulizwa maswali kuhusu serikali za mataa?

SHAHIDI: Walisema dhamana ipo wazi nikapeleka barua zangu nikamdhamini

Kibatala: Ulipokuja kumdhamini Huyo ndugu yako, Mliingia chumba kipi cha mahakama?

SHAHIDI: Sikuingia, nilimpa wakala wa Mahakama barua akapeleka

Kibatala: Huyo Ndugu yako Uliyekuja kumdhamini anaitwa nani?

SHAHIDI: Jonas Bunaya, aliibiwa kazini kwake.

Kibatala: Kesi yake inaendelea au imekwisha?

SHAHIDI: Ilishaisha na Jonas Bunaya ameshafariki. Tulikuja kureport hapa Mahakamani kuhusu Kufariki kwake.

Kibatala: Mlilipoti kwa hakimu gani?

HAHIDI: Tulirepoti kwa Kalani. Baada ya hapo tukaambiwa tuende taarifa imefika.

Kibatala: Mdhamini wa hiyo kesi ulikuwa wewe peke yako au kuna wengine?

SHAHIDI: Kulikuwa na wengine wawili, Mtu mmoja walichukua mtu wa kujitegemea na mwingine walimchukua hapa.

Kibatala: Bunaya alikuwa anaishi wapi?

SHAHIDI: Mbezi beach, Baharini.. Upande wa bahari

Kibatala: Viongozi wa mtaa wa mshitakiwa walikuwa wakina nani?

SHAHIDI: Hassan Faraji Ngonyani.

Kibatala: Huyo Kalani unayemtaja haoa mara kwa mara ni nani? Tukimleta hapa unaweza kumtambua?

SHAHIDI: Simkumbuki jina wala sura ya Kalani.

Kibatala: Siku Ulipomuona Lissu akiongea hayo maneno ilikuwa lini na tarehe gani?

SHAHIDI: Ni muda mrefu sikumbuki

Kibatala: Uliyemdhamini, kesi yake ilitajwa lini tena?

SHAHIDI: Sina kumbukumbu, kesi ni ya muda mrefu.

Kibatala: Siku ya tukio kama kweli lilitokea, angalia mahakama yote hii, Lissu alikuwa na watu wengine kati ya hawa walio hapa au alikuwa peke yake?

SHAHIDI: Nlimuona yeye kasimama kwenye jopo la watu.. Nlikuwa na haraka zangu nlimuona Lissu. Sikukalili mtu yoyote,Siwezi kukumbuka mtu..watu walikuwa wengi.

Kibatala: Wakati Lissu anaondoka mahakamani ulimuona?

SHAHIDI: Nlimuacha hapa akiongea mimi nliondoka.

Kibatala: Bunaya anamke?

SHAHIDI: Ndio ila naye ameshafariki kabla ya Bunaya.

Kibatala: Bunaya alikuwa na watoto, wangapi na wanaitwaje? Mwambie hakimu awa watoto wana umri gani?

SHAHIDI: Wapo wawili wakubwa tu wana familia zao.Ila namkumbuka mmoja jina anaitwa Seme Bunaya

Kibatala: Ulipoona polisi wanakuja sehemu Lissu alipokuwa anaongea ukaondoka, mwambie hakimu Polisi walikupataje wakati uliondoka?

SHAHIDI: Tulipokuwa na maeneo ya mahakama na wenzangu polisi wakaja wakasema tuna shida na nyinyi. Alikuja mtu kavaa kiraia

Kibatala: Huyo aliyekufuata unamfahamu jina au cheo?

Hapana: Hapana

Kibatala: Alikuchukua wewe peke yako?

SHAHIDI: Alinichukua na mtu nisiyemfahamu

Kibatala: Wakati unachukuliwa Bunaya Uliyekuja kumdhamini alikuwa wapi?

SHAHIDI: Bunaya alikuwa ameshatangulia na mkewe.

Hakimu(Mimi umeniacha, ulisema mke wake ndo alianza kufariki?)

Shahidi: Mke wa marehemu yupo, aliyekufa ni mama yake mzazi.

Kibatala: Uliyekuja kumdhamini hapa, ana mke hana mke?

SHAHIDI: Anaye mke

Kibatala: Hiyo siku ambayo huikumbuki tarehe yake ambapo ulikuja kumdhamini Buna, je mkewe alikuwepo?

SHAHIDI: Hakuwepo

KIbatala: Mama mzazi wa Bunaya, alikuwepo mahakamani au hakuwepo?

SHAHIDI: Mama wa mshitakiwa mahakamani alikuwepo ndo aliondoka na mwanaye. Wakati tunaoingia ndani yeye hakuwepo alikuwa amekaa nje.

Kibatala: Mwambie mheshimiwa hakimu kesi namba ya mheshimiwa Bunaya

SHAHIDI: Sikumbuki namba ya kesi, ni siku nyingi.

Kibatala: Huyo kalani alikuwa mwanamme au mwanamke?

SHAHIDI: Mwanamke

Kibatala: Umesema wewe ni mjenzi, shughuli zako wafanyia wapi?

SHAHIDI: Nafanyia Tegeta, Kawe au sehemu yoyote penye kazi.

Kibatala: Mtajie mheshimiwa hakimu majina matano ya watu uliowajengea nyumba

SHAHIDI: Kandurus Fussi anaishi Kawe nlimjengea nyumba ni mwanajeshi mstaafu, Christina Mgasa nlimjengea nyumba, Shayo wa my fair..

Kibatala: Twende kwenye siku ya tukio, Lissu alivaa nguo za aina gani?

SHAHIDI: Sikumbuki

Kibatala: Siku hiyo aliyokuwa amevaa miwani au alikuwa hajavaa?

SHAHIDI: Alivaa miwani..miwani ni jadi yake.

Kibatala: Ulikuwaje naye wakati anaongea? yaani mlikuwa naye umbali wa hatu kama ngapi?

SHAHIDI: Hatua kama tano

Kibatala: Kuna maneno mengine ambayo Lissu aliongea siku hiyo?
SHAHIDI: Mimi nliondoka

Kibatala: Toka anaanza kuongea wewe ulikuwa pale?

SHAHIDI: Ndio

Kibatala: Alifika na kuanza kuongea mambo ya uchwara?

SHAHIDI: Ndio.

Kibatala: Uliandikisha maelezo yako Polisi?

SHAHIDI: Ndio

Kibatala: Unamkumbuka afisa wa polisi aliyekuhoji?

SHAHIDI: Nikipindi kirefu...tulichukuliwa tukaambiwa kaa hapa sema nini kilichotokea, baada ya hapo wakasema wataniita wakinihitaji wakati wowote.

Kibatala: Na huyu mwingine mliyechukuliwa naye aliandikisha maelezo?

SHAHIDI: Ndio

Kibatala: Nani alijua umesafiri?

SHAHIDI: Nlipigiwa simu Polisi central, waliniuliza uko wapi nikajibu nmesafiri, Walinambia ukifika tu pindi utakaporudi, niende kurepoti polisi, ndo leo nikaenda.

Kibatala: Kama umefika Polisi kweli, hiyo mapokezi ipoje, Umeongea na nani kwenye chumba namba ngapi?

SHAHIDI: Kuna geti pale mlangoni, Polisi nliyeongea naye ni mwanaume, chumba sikikumbuki.

Kibatala: Lissu wakati anaongea siku hiyo ya Tukio hapa Mahakani Kisutu, kasimama wapi na alikuwa anaongea ameeleka upande upande upi? alikuwa anatazama barabara, mahakama, mwembe au?

SHAHIDI: Alikuwa ametazama getini na Alikiwa njia ya tano ya parking.

Kibatala: Mtu akija hapa mahakamani wakasema alikuwa karibu na bendera, watakuwa waongo?
(swali limekataliwa na hakimu)

Kibatala: Je ulisikia mwenyewe kwa masikio yako Lissu akitamka maneno rais Magufuli?

SHAHIDI: Ndio

Kibatala: Uliwaalifu hawa Polisi ulisikia neno Magufuli?

SHAHIDI: Ndio

Kibatala anamuomba hakimu au Upande wa Waleta Mashitaka wampe Hati ya Mashitaka ya hii Kesi.Wakili wa Serikali anampa Kibata Hati ya Mashitaka. Baada ya kuiangalia Kibatala anaendelea na Maswali.

Kibatala: Muambie mheshimiwa hakimu kama kuna neno rais Magufuli humu, sema kama unaliona(anampa Hati ya Mashitaka shahidi atafute kama kuna neno rais Magufuli). Unaliona neno rais Magufuli?

SHAHIDI: Halikuandikwa.

Kibatala: Kwenye ushahidi wako ulisema Lissu alisema rais dikiteta Je hayo maneno yapo?

SHAHIDI: Yapo

Kibatala: Umepewa Hati ya Mashitaka usome,(amepewa asome) onesha neno Rais Dikteta

Shahidi: Haijaandikwa.

Kibatala: Je maneno hatupaswi kumuunga mkono yapo?

Shahidi: Hawakuyaandika.

Kibatala: Je haya maneno yaliyoandikwa kwenye Hati ya Mashitaka ndo uliyoyasikia wewe au ni tofauti na yale Uliyoyasikia?

Shahidi: Haya ndo yaliyoandikwa kwenye cherge sheet ndiyo nliyoyasikia.

Kibatala: Hapa tuna set mbili za maneno ambayo hayaoani, Kumbukumbu yako sasa, maneno sahihi uliyoyasema kwa hakimu au haya yaliyopo kwenye hati ya mashitaka? Yapi sahihi?

Shahidi: Ni haya ya kwenye hati ya mashitaka, sio nliyomwambia hakimu awali.

Kibatala: Naomba umwambie mheshimiwa hakimu Serikali iliyokuwa anaitaja hapa ni Serikali ipi, aliitaja?

Shahidi: Kwa mjibu wa matamshi yake Serikali ni hii ya Tanzania, hakuna Serikali nyingine.

Kibatala: Je kwenye hati ya Mahitaka wapi imeandikwa Serikali ya Tanzania?

Shahidi: Alizungumzia Serikali ya Tanzania sio nchi nyingine kama hayapo hapo mimi sijui.

Kibatala: Alisema ipingwe kwa namna gani, watu kuandamana au kupigwa kwa mabomu kama walivyofanya kwenye Ofisi ya wanasheria?

Shahidi: Yeye ndo anaweza kujua alikuwa na maana gani

Kibatala: Ujinga unamanisha nini?

Shahidi: dharau.

Kibatala: Ni sahihi kwamba ujinga ni kutofahamu kitu fulani?

Shihidi: Ni ufahamu wa mtu

Kibatala: Julius K. Nyerere alisema maadui wakubwa wa maendeleo ni nini?

Shahidi: Ujinga, umasikini na Maradhi

Kibatala: Nyerere ulimuelewaje?

SHAHIDI: Siwezi kujua kwenye utawala wake alikuwa analenga nini.

kibatala: Wewe unasema maneno yalikukera, huyu unayemsema kaitwa Dikteta, kule Tanga alisema Mawaziri wake ni Wapumbavu Je ni kweli je hayo maneno yake hayajakukera?

SHAHIDI: Siwezi jua

Kibatala: Ni kweli kwamba kuna watu walifukuzwa kwa kufoji vyetu na viongozi kuondolewa madarakani tangu Lissu atamke hivyo unavyosema?

Shihidi: mimi sifuatilii maisha ya mtu.

Kibatala: Serikali ya kidikteta inamaanisha nini?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Hata Dikteta uchwara huwezi kujua maana yake si ndio?

Shihidi: Mimi si mtaalam wa lugha

KIbatala: Je Lissu anatoka chama kimoja na Magufuli?

SHAHIDI: Mi sio mwanasiasa siwezi kujua.

Kibatala: Ulishawahi kusikia rais Magufuli akipinga haya maneno ya Dikteta Uchwara?

Shahidi: sifuatilii mambo ya siasa

Kibatala: Ulishawahi kusikia Benjamin Mkapa akisema wananchi wa nchi hii ni wapumbavu?

Shihidi: Sijawahi

Kibatala: Tuchukulie Lissu alitamka haya maneno na haujui chochote kuhusu matamsha ya Mkapa na Magufuli ya Wapumbavu wala hayajakukera, imekuwaje hii ya Lissu imekukera? Nini kimekukeleketa?

SHAHIDI: Hizi habari haziendani na mwenendo wa nchi yetu ndo maana nliposikia anayataja nikatoka sehemu ya tukio

Kibatala: Ulisikia unachochewa kufanya nini?

Shahidi: Ni matamshi yalikuwa yanatoka.. Hajanichochea mimi alikuwa anazungumzia nchi. Hawezi kunichochea.

Kibatala: Mdhamini mwenzako alisema alichochewa kufanya ninina Lissu?

SHAHIDI: Siwezi kujua kila mtu alikuwa kwenye chumba chake?

Kibatala: Je ungekuwa unafahamu Lissu ni kiongozi wa chadema au kiongozi wa upinzani, je ni kosa kuipinga Serikali iliyoko madarakani.

SHAHIDI: Sijui chochote, hayo mambo ni taratibu za Kiserikali

Kibatala: Mtaani kwako umesema zamani ulikuwa ukiongozwa na Kiongozi ila kwa sasa ameangushwa, Huyo mwenyekiti aliyeangushwa alikiwa wa chama gani?

SHAHIDI: Alikuwa wa CCM aliangushwa na CHADEMA kwenye mtaa ninao kaa.

KIbatala: Je huyo wa CHADEMA alimshambulia huyo wa CCM?

Shahidi: Nmeshakwambia mimi usiniulize mambo ya siasa.

Kibatala: Ulikiwepo wakati wa kampeni? Mimi nipo hapa kwaajili ya kukuuliza maswali, Usinipangie swali la kukuuliza

Shahidi: sikuwepo

Kibatala: Huyu mwenyekiti wa CHADEMA anampenda watu wote?

Shihidi: Siwezi jua sababu natoka asubuhi narudi usiku

Kibatala: Je unalidhika na utendaji kazi wake?

SHAHIDI: Kiongozi ni kiongozi mradi anafuata taratibu za nchi.

Kibatala: Wewe unapanda bodaboda, usafiri wa bodaboda unatumia?

SHAHIDI: Ndio

Kibatala: Uliwahi kusikia Magufuli akisema bodaboda zinazopita Kwenye barabara ya mwendo kasi zing'olewe matairi?

SHAHIDI: Sikuwahi kumsikia

Kibatala: Je ni sahihi mtu akikosea Utaratibu matairi yanyofolewe?

Wakili wa Serikali amekataa swali

Shahidi: Hiyo ni kazi ya trafiki sio mimi.

Kibatala: Hao polisi walioanza kusogea eneo la tukio walikuwa wametokea eneo gani, waliovaa uniform walikuwa wangapi?

SHAHIDI: Sijui walipotokea, waliovaa uniform walikuwa wanne. Lissu alikuwa kamaliza kuongea, Watu walitawanyika, Lissu alitawanyika akaelekea kwenye gari yake.

Kibatala: Ulijuaje ni ni gari yake, Gari yake ilikuwa imepark wapi?

SHAHIDI: Nliona ameingia kwenye gari nikajua ndo yake.

Kibatala: Ilikuwa imepark wapi?

SHAHIDI: Sikuona anaingia kwenye gari gani ila alielekea kwenye magari yalipopark.

Kibatala: Gari ya Lissu ilikuwa rangi gani?

SHAHIDI: Sikutaja gari.

Kibatala: Ukiachilia mbali polisi na wandishi wa habari, ni nini kingine unakumbuka kilitokea au kilikuwepo?

Shahidi: Sikuona chochote

Kibatala amemaliza kumhoji na kusema kwamba hana swali lingine.

Wakili wa Serikali anaomba kuuliza tena Swali moja.

Wakili wa Serikali: Yale maneno uliyoyataja ya "Rais Magufuli ni rais dikteta, dikteta uchwara, Watanzania wenzangu tusipokuwa makini tunaingia kwenye giza nene. hatupaswi kumuunga mkono", ulisikia akiyatamka nani?

Shahidi: Tundu Lissu

Maswali yameisha, Kesi kusikilizwa tena Tarehe 4/9.

Ushahidi wa kubumba huu hautawasaidia chochote waendesha mashtaka wa serikali mwisho wa siku wataangukia pua na Tundu Lissu ataibuka kidedea.
 
Mzoefu kama huyu eti hayumo kwenye timu ya majadiliano! Iko miruma na miosoro!

Tukishindwa ndio utasikia Lisu lisu lisu.
Hapo hakuna sheria wala utaalam wowote. Kibatala alikuwa akigonga meza za Kisutu tu. Shahidi alijibu vizuri ingawa ni raia wa kawaida tu.
 
  • Shabbash...! Lissu na Kibatala walikwenda Mahakamani Kisutu tena wakati jana tu Lissu mwenyewe akiungwa mkono na Kibatala &Co. alitoa tamko kwa mawakili wote nchini kususia kwenda mahakamani leo 28/8 na kesho 29/8 ikiwa ni njia ya kulaani kushambuliwa kwa kampuni ya mawakili ya IMMMA? Ama kweli wajinga ndio waliwao!
 
  • Shabbash...! Lissu na Kibatala walikwenda Mahakamani Kisutu tena wakati jana tu Lissu mwenyewe akiungwa mkono na Kibatala &Co. alitoa tamko kwa mawakili wote nchini kususia kwenda mahakamani leo 28/8 na kesho 29/8 ikiwa ni njia ya kulaani kushambuliwa kwa kampuni ya mawakili ya IMMMA? Ama kweli wajinga ndio waliwao!
Aseeh! Mgomo ni jumanne na jumatano ,Leo jumatatu kuwa mpore kiongozi. Sorry wewe ni Sophia?

To accomplish much you must first lose everything..
 
Hapo hakuna sheria wala utaalam wowote. Kibatala alikuwa akigonga meza za Kisutu tu. Shahidi alijibu vizuri ingawa ni raia wa kawaida tu.
"hakuchochewa na chochote ila alichukia na kuondoka"

Ameua shitaka la uchochezi.
 
Hahahahaha hawa mashaidi wananivunja mbavu, "Mke wa marehemu alitangulia kufariki halafu tena aliongozana na mkewe wakitoka mahakamani "Tena ni mama wa marehemu ndio alitangulia kufariki sio mkewe "

Kazi kweli kweli hata mwenyekiti wa mtaa anao ishi hamjui ila kaenda kumuwekea mtu mdhamana
 
"hakuchochewa na chochote ila alichukia na kuondoka"

Ameua shitaka la uchochezi.
Kukubali kutoa ushahidi dhidi ya perpetrator ni dhahiri kuwa alikerekwa. Hiyo ndio anatomy ya mashitaka. Watu wakihudhika wanaweza ku-react kwabnamna ambayo in-create political and social discord.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom