Ndo umeandika nn sasa
Hakuna mtu aliyetegemea kama siku ya leo Dr. Magufuli angepata watu katika uwanja wa Sheik Amri Abeid Arusha. Hata yeye mwenyewe Magufuli hakuamini alichokiona leo. Watu walikuwa wengi sana hasa ikizingatiwa kuwa Arusha ni ngome ya CHADEMA. Mbaya zaidi, vijana waliokuwa wamevalia sare za CCM walikuwa wengi mno. Mimi mwenyewe leo nilikuwa Arusha na nikasema lazima niende nikashuhudie nini kitatokea huko. Sikuamini kabisa!
Kumekuwa na upotoshaji mkubwa sana kuhusu wana CCM wa Arusha. Tumewasikia Mara nyingi sana UKAWA wakisema eti Arusha CCM imekufa, hapana, Arusha CCM iko hai tena iko imara sana. Nilichogundua WanaCCM wa Arusha sio watu wa kupiga kelele na kujionesha barabarani. Leo vijana wa CHADEMA walipigwa na butwaa hasa walipoona vijana wenzao kwa maelfu wakiwa wamevalia mavazi ya CCM.
Mimi ni mwanaCCM ambae sikai Arusha lakini leo nilifurahi sana tena sana kwa nilichokiona. Kuna kila dalili, jimbo la Arusha mjini linarudi mikononi mwa CCM. Nilikuwa nimekaa na wenyeji wa mji huu pale uwanjani, na wengi wao walisema CHADEMA ilishinda Ubunge Arusha sababu wazee wengi wa CCM walichukizwa na aina ya mtu waliyepewa wakati ule ndio maana wengi wao hawakupiga kura. Sasa hivi wanasema wamechukizwa zaidi na Lema sababu ameifanya Arusha kuwa ni ya maandamano na vurugu na mabomu kitu ambacho wanajuta. Wakazi wengi wa Arusha wameapa kumchagua Philemon Molel {MONABAN} kuwa Mbunge wao.
Nafahamu fika kuwa mshindi wa urais anapatikana kwa kupigiwa kura, lakini ukweli utabakia pale pale kuwa Magufuli ana nafasi kubwa sana ya kuingia Ikulu na ninaweza kusema mpaka sasa ni kama Magufuli amemaliza Kampeni na leo amefunga kazi Arusha mjini. Hata yeye mwenyewe leo baada ya kuona umati uliojaa uwanjani alisema sasa basi, yeye ameshakuwa rais tayari. Mimi pia nasema nikiwa kama mwana CCM kwa nilichokiona leo Arusha ambayo ni ngome ya CHADEMA, basi hakuna ubishi, Magufuli ndio rais mpya wa Tanzania.
#HapaKaziTu CHAGUA MAGUFULI.
Magufuli chaguo la Watanzania wote.
Thubutu yako, sisi ndiyo A Towners wazee wa Dili.Nani hapendi kula na vipofu?
Hakunaga CCM huku A Town kwa taarifa yako chaliangu, ukitaka kuamini muulize Batillda na Felix Mrema wanatujua vema, wewe waja leo na kurudi kesho huwezi pata ukweli.Zaidi njoo kijiwe utatukuta tunepeana mrejesho wa kazi.
Sasa wakivimba wakapasuka kura watampigiaje au nayo ipo kwenye ilani ya chama
Piga hesabu 15000 mara idadi ya watu waliofika, kisha zidisha na wengine mikoa mingine ambayo inasemekana watu walinunuliwa, kisha shirikisha ubongo wako! Je inawezekana?
Tuombe Mungu atupe uzima tarehe 25 sio mbali utapata jibu.
Arusha wamekubali kazi na wanataka kazi tu!
"Picha hizo si halisi"
hapa kazi tu. utabiri wa kuhani mkuu wa chadema gwajima et al ni mizungu tu oct 25 tunachagua mtu muadilifu na mchapa kazi magufuli. hapa ni kazi tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuiuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu.Pipoooooooooooooooooz ✌✌✌✌✌✌✌✌✌✌
Watu kweli mnashangaza na ni wepesi wa kusahau kweli kweli. Magufuli alipozindua kampeni Jangwani Dar mkapagawa mara oh kwa tulichokiona Jangwani leo Magufuli ni Raisi. Hazikupita siku saba Lowassa akatinga Jangwani na loo mkanyamazishwa kama vile mmemwagiwa maji baridi.
Magufuli akafika Mbeya na kwa mhemuko mkasahau ya Dar es Salaam hadi siku Lowassa alipotua Mbeya mkawa kimyaaa!
Magufuli akafika Tanga mkapagawa tena hadi Lowassa alipotua huko na kuwanyamazisha. Kama vile hamna kumbukumbu leo mmeanza tena baada ta Magufuli kufika Arusha...
Mmeshindwa kabisa kuona tofauti iliyopo kati ya mafuriko na gharika, unazi umewapofua; mnayo macho lakini hamuoni, mnayo masikio lakini hamsikii. Basi hamna tena namna, subirini kipigo cha Oktoba 25!