Yaliyojiri Ikulu: Mazungumzo kati ya Viongozi wa dini nchini na Rais Magufuli

Baadhi ya Viongozi wa dini wa karne Hii ni wa hovyo hamstahili kusimama mbele ya altare ya Mungu nyie ni wanafiki mlipata nafasi adhimu ya kuongea na rais mkaitumia vibaya nampongeza Yule mchungaji aliyeongelea dwmokrasia na wengine Kama walikuwepo waliotusemea wananchi ila Wale walioenda kusifu pale Kama uvccm mjue mmetuudhi Sana nyie ni wanafiki na hatutegemei Yale matamko yenu ya pasaka!!!
 
No more kubet? Hope baada ya lile swali ikulu kubeti kutapigwa ban sio kitambo.
IMG-20190124-WA0005.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baadhi ya Viongozi wa dini wa karne Hii ni wa hovyo hamstahili kusimama mbele ya altare ya Mungu nyie ni wanafiki mlipata nafasi adhimu ya kuongea na rais mkaitumia vibaya nampongeza Yule mchungaji aliyeongelea dwmokrasia na wengine Kama walikuwepo waliotusemea wananchi ila Wale walioenda kusifu pale Kama uvccm mjue mmetuudhi Sana nyie ni wanafiki na hatutegemei Yale matamko yenu ya pasaka!!!

Ulitaka waende kupinga kila jambo kama Bavicha na Bawacha?
 
Aisee, ala wametangusha sana, wamekuwa woote branch of CCM..... wanashindwa kuongerea bomoa bomoa, mtaani njaa hamna pesa, magari ya mwendokasi wanavyo tutesa

Dah
 
Ni vizuri Kiongozi wa nchi anapokuwa anakutana na wananchi wake kama hivi ili kujua changamoto na kuweza kupokea mawanzo...........hongera Dkt Magufuli tunajua nia yako ni njema tu.
 
Mchungaji Msigwa ni kiongozi wa Kanisa moja la walokole pale Iringa mjini lakini pia ndiye mbunge wa Iringa mjini.
Jana nilijaribu kuwaangalia viongozi wa dini waliohudhuria kupitia luninga lakini sikumuona baba mchungaji Msigwa ingawa palikuwepo wachungaji, maaskofu na mashehe kutoka sehemu zote za Tu.

Je mchungaji Msigwa hakupata mwaliko, alikuwa na udhuru au Kanisa lake ni miongoni mwa yale makanisa madogo madogo yasiyofahamika sana?

Ahsanteni
Maendeleo hayana vyama!
 
Rais kasema sawa kabisa. Mbona nchi nyininge zana vyama vingi hatuoni maandamano kila kukicha. Hakika Watanzaia ile miaka ya 90 tulikuwa sahihi. Tulikuwa bado hatujawa elimu ya Vyama vingi tulidhani vyama vingi ni mapambano. Yaani chama Pinzani ni kupinga kiiiila kitu tulichemsha. Haya unfortunately Vyama vya Upinzani vinadhani Demokrasia ni HOLELA no maaan! Basi huko USA si ungekuta watu wanatembea bila nguo!
 
Hivi kwa akili yako unadhani viongozi wa Dini na wewe nani ana akili zaidi ya mwingine , Tafadhali sana usiwadharau wamesoma sana huenda zaidi ya hata sie na wanajua mengi sana hata zaidi ya sie .Wanajua na kuona pia . Wanajua uzushi na ukweli tusiwafundishe samahani sana.
Bila shaka yo yote akili yako ni ndogo sana kulinganisha na viongozi wa dini na ndiyo sababu unawaabudu kama Miungu!!
 
Mchungaji Msigwa ni kiongozi wa Kanisa moja la walokole pale Iringa mjini lakini pia ndiye mbunge wa Iringa mjini.
Jana nilijaribu kuwaangalia viongozi wa dini waliohudhuria kupitia luninga lakini sikumuona baba mchungaji Msigwa ingawa palikuwepo wachungaji, maaskofu na mashehe kutoka sehemu zote za Tu.

Je mchungaji Msigwa hakupata mwaliko, alikuwa na udhuru au Kanisa lake ni miongoni mwa yale makanisa madogo madogo yasiyofahamika sana?

Ahsanteni
Maendeleo hayana vyama!

Kwa namna moja ama nyingine mikutano miwili aliyofanya mheshimiwa Rais mwezi huu wa kwanza ilikuwa ni ya mafanikio makubwa kwa maslahi ya Taifa la TANZANIA,

Nimependa mkutano aliofanya na wadau wa madini na pia mkutano aliofanya na viongozi wa dini niliamini ya kwamba nia ilikuwa ni njema kwa Taifa na watanzania kwa ujumla

na kama ilivyokuwa kwa watu wa sekta ya madini hata viongozi wa dini siyo rahisi kwamba angeweza kualika wahusika wote nchi nzima kwa asilimia mia moja pamoja na kwamba wapo pia walioalikwa nao wakashindwa kuhudhuria kwa sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wao ama wengine kwa kutokuupa umuhimu unaostahilli katika mikutano hiyo.

Na sidhani kama itakuwa vyema kuanzia kutafuta ni nani ambaye hakuhudhuria na kwa nini kwa sababu kufanya hivyo tutakuwa hatujisaidii sisi wenyewe na pia hatuisaidii jamii ya watanzania zaidi ya kwamba tutakuwa pia hatuna na wala hatuoni nia nzuri ya kilichofanyika

Ni vizuri tungekuwa na hoja ya kuchambua changamoto na mambo yaliyowakilishwa kwa Rais kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tunashauri kwa sehemu yale ambayo Raisi aliambiwa na hao pengine wadau wa madini ama viongozi wa dini na na kwa namna hiyo tutakuwa tumeitendea nchi haki

Sidhani kama ingekusaidia kwa lolote ukifahamu kwamba ni nani na kwa sababu gani hakuhudhuria yule uliyemdhania ama uliyekuwa unapenda awepo,maana wewe unamfahamu huyo umpendae na mtu mwingine naye anamfahamu wa kwake na tena hamfahamu huyo wa kwako kama na wewe usivyomfahamu huyo wa kwake.
Naomba tuchambue hoja zilizojitokeza kwenye mikutano ile .
 
Msgwa ni kiongozi wa dini au dhehebu lipi? Kwa maelezo tuliopewa, walioalikwa siyo kila mchungaji/padre/katekista/shehe nk. Waliitwa viongozi wanaoongoza dini au madhehebu yao. Wengi waliofika ni viongozi wenyewe wenye huduma zao kama vile akina Kakobe, Mwingira, Gwajima, nk, au wawakilishi waliotumwa na viongozi wanaoongoza madhehebu mfano Bakwata, RC, KKKT, nk.

Mchungaji Msigwa sijawahi kuisikia huduma yake inayojitegemea. Labda swahi hili lingemhusu mama Lwakatare ambaye ni mbunge na ana huduma yake anayoiongoza.
 
Ni jana tu viongozi wa dini walikutana na Rais ikulu, kwa mwaliko wa Rais. Viongozi hawa wa dini wanaishi na watanzania, kwa fikra za watu wengi, ni kuwa viongozi hawa wa dini wanayajua matatizo ya waumini wao kwa undani.

Waumini wengi walitarajia kuwa matatizo na madhira yao mengi yangelifikia sikio la Mh. Rais kwa kupitia wao. Nina imani Mh. Rais aliwaalika viongozi akiwa na dhamira ya kusikia mapungufu yaliyopo kwenye utawala wake ili aweze kuyafanyia kazi.

Waumini wengi walivunjika moyo pale ambapo viongozi wao wengi wa dinia walipoonekana kuitumia nafasi waliyopewa, kuacha kutoa maoni kuhusiana na matatizo ya waumini wao, na zaidi wakaitumia nafasi hiyo kutafuta recognition kwa Rais.

Wengine wakatumia nafasi hiyo kuelezea jinsi wao walivyo muhimu katika uongozi wa nchi.

Baadhi walienda mbali zaidi na kutamka kuwa Rais alikuwa amechelewa mno kuwaalila, alitakiwa awaalike wakati alipochukua madaraka ili wapange kwa pamoja namna ya kuongoza nchi!

Kwa maoni yangu, mahusiano ya viongozi wa dini kwa serikali yanaishia kwenye kushauri na kuonya. Na pia ni jambo jema kukiwepo mahusiano mazuri kati ya serikali na taasisi za dini lakini siyo kutengeneza urafiki wa kuongoza nchi.

Viongozi wa dini wana majukwaa yao mahekaluni, misikitini na makanisani ambako wanaweza kuwahubiria waumini wao, wakiwemo watawala na watumishi wa serikali. Huko wanaweza kuonya, wanaweza kukemea, wanaweza kushauri, na kusiwepo wa kuwaingilia. Kualikwa na Rais kwaajili kusikia maoni yao, ni matakwa ya Rais, na siyo wajibu.

Viongozi wa dini wasitafute urafiki na watawala wala wasitafute kuwa sehemu ya watawala. Kama watakuwa marafiki wa watawala au watajiingiza kwenye serikali, watapoteza ihalali wao wa kukemea, kushauri na kuonya.

Zaidi ya kutafuta recognition, viongozi wa dini walitumia muda wao mwingi kupongeza juhudi na mambo mema anayofanya Rais. Kupongeza siyo jambo baya kama kuna jambo jema linafanywa. Lakini kupongeza tu bila kushauri kwenye kasoro, hasa zile kubwa, nadhani hata Rais mwenyewe hatakuwa amefaidika chochote toka kwenye hekima ya hawa viongozi wa dini maana siamini kama Rais aliwaalika kwa nia ya kumpongeza.

Kinachoshangaza zaidi, ni viongozi hawa hawa wa dini, ndio wanaotoa kasoro nyingi za utawala wa Mh. Rais Magufuli wakiwa mbali naye. Ni hawa hawa ndio wanaoandika nyaraka kali kali dhidi ya serikali na watawala. Lakini baada ya kuitwa wanachoweza kutamka ni pongezi tu! Tunachojiuliza, yale malalamiko kwenye nyaraka ilikuwa ni tuhuma za uwongo au chuki ya kitotambulika kuwa na wao ni muhimu? Au wanashindwa kunena KWELI kwa sababu ya woga mbele ya mtawala? Au viongpzi hawa ni wanafiki, wanatamka uale wanayodhani aliywewaalika atapenda kusikia? Au pengine yawezekana yale malalamiko ya kwenye nyaraka yalikwishafanyiwa kazi yote?

Kama viongozi wa dini ni waoga, ni nani atakuwa jasiri?

Kama viongozi wa dini ni wanafiki, wanawafundisha nini waumini wao? Rais atawaheshimu vipi viongozi wanafiki?

Au viongozi wa dini wanawashutumu watawala kwa vile watawala hawataki kuonesha kuwa viongozi wa dini ni muhimu sana katika kuongoza nchi?

Au viongozi wa dini hawakujua Rais alikuwa amewaitia nini, pamoja na ukweli kuwa aliwaeleza mwanzoni mwa mkutano wao?

Viongozi wa dini tumewasikia. Tutawadharau kama baada ya kutoka ikulu ndimi zenu zikanena tofauti na tulovyowasikia mkinena mlipokuwa mbele ya Mh Rais.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom