Yaliyojiri Ikulu: Mazungumzo kati ya Viongozi wa dini nchini na Rais Magufuli

Kuelekea 2020 ikulu imetumia karata yake vzr kuwaita viongozi wa dini na kuwasikiliza, huu ni mtego mzuri wa kuwagombanisha viongozi wa dini na vyama vya upinzani.
Kwa maoni yng mi naona ni bora viongozi wa upinzani wakakaa kimya na kuliacha hili lipite kuliko kuanza kuliongelea kwa hasira, kejeli na dharau kitu ambacho ndio shabaha iliyokusudiwa kuwatenganisha viongozi wa dini na vyama vya upinzani ili kuvunja umoja na mshikamano baina yao kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020.
Divide and rule inafanya kazi mpk misikitini na kanisani.

Maendeleo hayana chama
Sio kivile mkuu, wana lao moyoni. Ipo shida kubwa mfano wadau sector afya,elimu. Unyanyapaa wa wazi. Hali za waumini wengi ni duni,same sadaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanafki sana Mimi nilishakata mguu na sitokuja kwenda kwao
Kama ni ibada nishaipata yangu mwenyewe

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilikuwa namuamini sana Kakobe. Nilikuwa namuona anasimamia anachokiamini bila kutetereka.
Kababaishwa kidogo tu, kajisalimisha haraka kwa mtu yule yule ambaye alitutangazia kuwa anapaswa kwenda kutubu kwa dhambi zake alizozifanya! Badala yake, kaenda kutubu yeye kwake! HONGERA KWAKE BASHITE!
 
Wale wote wako kwa ajili ya matumbo yao
Walitaka tunushiana msuli na serikali wkt wao wenyewe Wana misala kibao....serikali ilijua udhaifu wao wapi pa kuwashika mwishowe wenyewe wakawa wapole
Ukitaka kuwa mkosoaji mwanaharakati yabidi uwe clean

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kivile mkuu, wana lao moyoni. Ipo shida kubwa mfano wadau sector afya,elimu. Unyanyapaa wa wazi. Hali za waumini wengi ni duni,same sadaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakubaliana na hilo mkuu, hata viongozi wa dini kwa namna moja ama nyingine hilo wamelizungumzia sana kwenye hicho kikao.
Wewe ushajiuliza kwa nini viongozi hao waalikwe 2019 na sio 2017 au 2018?
Mkuu amini nakwambia kualikwa kwao ni miongoni mwa mkakati wa kuelekea 2020.
Na mbaya zaidi ukishaingia ndani ya jumba jeupe kamwe hauwezi kukosoa utaishia kusifia tu hata kama unalo dukuduku lako moyoni kama unabisha muulize Edward Lowasa maana hata yeye alishaingia mule.

Maendeleo hayana chama
 
Kuelekea 2020 ikulu imetumia karata yake vzr kuwaita viongozi wa dini na kuwasikiliza, huu ni mtego mzuri wa kuwagombanisha viongozi wa dini na vyama vya upinzani.
Kwa maoni yng mi naona ni bora viongozi wa upinzani wakakaa kimya na kuliacha hili lipite kuliko kuanza kuliongelea kwa hasira, kejeli na dharau kitu ambacho ndio shabaha iliyokusudiwa kuwatenganisha viongozi wa dini na vyama vya upinzani ili kuvunja umoja na mshikamano baina yao kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020.
Divide and rule inafanya kazi mpk misikitini na kanisani.

Maendeleo hayana chama
Facts mkuu.

Ila sijamuona wakujua kama ni trap kwao ni Msigwa au Lema?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikuwa namuamini sana Kakobe. Nilikuwa namuona anasimamia anachokiamini bila kutetereka.
Kababaishwa kidogo tu, kajisalimisha haraka kwa mtu yule yule ambaye alitutangazia kuwa anapaswa kwenda kutubu kwa dhambi zake alizozifanya! Badala yake, kaenda kutubu yeye kwake! HONGERA KWAKE BASHITE!
Toba ya mtu ni siri yake na roho yake na Mungu wake. Kamwe hatusikii matangazo na tafrija baada ya mtu kutubu. Suala la kutubu ni kuwaachia wahusika wenyewe.

Mtazamo wangu ni kuwa serikali inataka kuji-brand tena kama sikivu. Hata hili la muswada wa vyama vya siasa huenda lisipitishwe kwa kuwa imeshaonekana wazi watanzania walio wengi hawajaunga mkono mswada huo. Hata ndani ya CCM, huu muswada umeleta ukakasi.

Tusubiri tuone mwelekeo wa mwaka huu. Ila bado ni mapema mno kutoa hukumu. Huenda kwa viongizi wa dini kukaa na serikali na kuifunda ni ishara njema kuwa uelekeo wa serikali ni kukaa na wahusika na kushauriana ili kupata matunda yaliyo bora kwa taifa. Tusubiri tuone.
 
Mimi binafsi,napenda kumpongeza Rais kwa kuzikumbusha taasisi za dini katika kulipa kodi na kufanya majukumu yao ipaswavyo.Viongozi wakuu wa dini hapa nchini wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kujenga Taifa kupitia taasisi walizozijenga wakiwa na lengo la kumkomboa mnyonge Kiimani,Kifikra,Afya n.k na sio kutazama matoleo tu! bali pia kusimamia matumizi sahihi ya hayo matoleo kama wanavyotuhubiria.
Katika hali halisi baadhi ya taasisi za kidini zimekuwa na Administration na vyanzo vya fedha karibu nchi nzima, na zina nguvu kubwa na waumini wake baadhi ni viongozi wa kubwa hapa nchini ambayo tunategemea wazingatie matumizi sahihi ya rasli mali,kujali utu,Kuwa mstari wa mbele katika maendeleo..
Rais alionesha kuwaheshimu viongozi wa dini,aliwatania kidogo wakacheka na kufurahi,kisha walikwenda kupata chakula kwa pamoja..
 
Hoja za Maji, demokrasia, mirathi, barabara, elimu,korosho, madini, umaskini mikoa ya kusini nk yalisema na viongoi wa dini kama wawakilishi wa wananchi na Rais kasema amechukua yote isipokuwa lile la demokrasia amefafanua kwamba kila Mbunge afanye mikutano jimboni kwake kana Polepole na Bashiru ("Wabunge")

Sasa swali kwenu: je kutokana na mkutano huo kuwa na ufanisi tena kwa muda mfupi wa siku moja. kuna haja gani kuwa na Bunge linalokaa miei mingi ambalo pia linatuhumiwa kuwa dhaifu?
 
Viongozi wa dini walishindwa kujikita katika hoja ya msingi ya serikali kuheshimu utawala wa sheria na kukemea uvunjifu wa katiba unaofanywa na viongozi wa serikali!

Hawakupaswa kuzungumzia kazi za serikali ambazo ni wajibu wake kuwatekelezea wananchi!
 
inawezekana walifanya hivyo baada ya kuona Bunge linaloisimamia serikali ni dhaifu
 
mleta mada uwa unanifurahisha sana, yaani unahoji na.kujijibu mwenyewe kama una majibu mfukoni hivyo unataka yapate kibali
 
1548323658965.png

Rais wa Tanzania Mhe Dtk.John Magufuli amewataka watanzania kupuuza uzushi unaozushwa na baadhi ya watu kuwa hapa nchini hakuna demokrasia na kusema kuwa demokrasia siyo kufanya maandamano bali ni watu kufanya kazi.
 
Viongozi wa dini walishindwa kujikita katika hoja ya msingi ya serikali kuheshimu utawala wa sheria na kukemea uvunjifu wa katiba unaofanywa na viongozi wa serikali!

Hawakupaswa kuzungumzia kazi za serikali ambazo ni wajibu wake kuwatekelezea wananchi!
Hivi kwa akili yako unadhani viongozi wa Dini na wewe nani ana akili zaidi ya mwingine , Tafadhali sana usiwadharau wamesoma sana huenda zaidi ya hata sie na wanajua mengi sana hata zaidi ya sie .Wanajua na kuona pia . Wanajua uzushi na ukweli tusiwafundishe samahani sana.
 
Hii tafsiri yake mpya ameiokota pori gani ? ama kwa hakika Kikwete alichoifanyia nchi hii wee acha tu !
 
Back
Top Bottom