Yaliyojiri Bungeni Dodoma leo Tarehe 13 Mei, 2015

Yaliyojiri Bungeni Dodoma leo Tarehe 13 Mei, 2015

Toka Jana nimeshuhudia Wabunge wakongwe wa CCM wakionyesha mashaka yao kuwa haitaendelea kutawala nchi hii ... UKAWA now or never ...
 
aisee ccm mwaka huu lazima waangukie pua,kwa hayo madudu wanayoyafanya hakuna kijana atakaekichagua labda vikongwe
 
Toka Jana nimeshuhudia Wabunge wakongwe wa CCM wakionyesha mashaka yao kuwa haitaendelea kutawala nchi hii ... UKAWA now or never ...
Tafadhari funguka hujaeleweka.
Fafanua kiasi kwamba hata ambaye hajawashuhudia wabunge hao anaweza kupata picha kwa jinsi gani wanakiri chama chao hakitaweza tena kuitawala nchi hii.
Wameonyesha dalili zipi? Mahala gani? Wanetamkaje? n.k
 
Kibajahi naona yupo kwa ajili ya kufurahisha bunge
Ingekuwa enzi za ufalme angefaa kumchekesha mfalme
 
Wadau, amani iwe kwenu. Hakika jema lazima litukuzwe na siku zote ukweli hujitenga kwenye unafiki. Huyu Mbunge wa Kasulu Vijijini, Agripina Zaituni Buyogera ameisifu Serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuufungua Mkoa wa Kigoma na kuunganisha na mikoa mingine. Anasema kuwa Kigoma ilitengwa na awamu zilizotangulia ila awamu ya nne mambo yamekuwa mazuri. Kwamba, baada ya ujenzi wa daraja la Malagarasi, kigoma sasa kuchele. Pia ameipongeza serikali kwa kupeleka miradi mikubwa ya maji kwenye vijiji vya Kasangesi, Nyarugusu na Rungwe Mpya.

Pamoja na pongezi hizo, Buyogera ameiomba serikali sikivu ya CCM kukamilisha ujenzi wa barabara ya Kidakwe hadi Nyakanazi ili kufungua fursa zaidi za mkoa wa Kigoma. Aidha, anaiomba pia serikali kukamilisha miradi hiyo ya maji kwani wananchi wanaisubiri kwa hamu kubwa sana.

Ukweli Uwazi.
Asiyeona mazuri ya ccm basi huyo ni zuzu
 
Bunge limegeuka kijiwe cha kupigia kampeni.
 
Akili ya msigwa ni sawa na wabunge 20,,wachanganye mawazo bado wanaweza wasimfikie.... Msigwa jembe.... Anajua anachozungumza.. Deni la kila mtanzania.. Ni 846000..Kutoka 440000,,,du watatuuua ccm
 
Nimemsikiliza Manyanya mpaka anatia huruma...
Anasema bajeti iandaliwe kwa kuangalia nchi ili serikali ya chama chochote isipate shida ya kuwahudumia wananchi.
Hana uhakika kama ccm itakuwepo.
UKAWA mpango mzima October.
 
Back
Top Bottom