Yalikua maamuzi magumu ila ya busara

Yalikua maamuzi magumu ila ya busara

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,425
Familia hii ilikua ya jirani zetu, walibahatika kupatawatoto watatu, mama na baba wote walikua wafanyakazi wa serikali. Nyumba waliyokuwa wanaishi waliijenga wenyewe.

Kutokana na majukumu ya kazi za baba na mama, waliajiri dereva wa kupeleka watoto shule asubuhi na kuwarudisha, walikuwa pia na dada wa kazi.

Mama alipata nafasi ya kwenda Australia kusomea shahada ya uzamili, wakati huo huo dada akatoa notice ya kuacha kazi.

Katika kutafuta mtu wa kazi, akatokea mama wa miaka 30+ anatafuta kazi za ndani, mama akaona kwasababu yeye anasafiri, huyu atakua mtu muafaka wa kulea watoto.

Baada ya mama kuondoka, upweke ulimsonga sana baba, akawa akitoka kazini anapitia bar kupata kinywaji. Ssa akirudi nyumbani, mfanyakazi anakuja na kanga moja kumwekea baba chakula.

Tena anamsubiri amalize kula ili aondoe vyombo. Baba kama mwanaume, akaanza kutamani, basi sikumoja akajaribu kama amesahau hivi, akamgusa dada makalio, ilikua kosa, dada akalegea kabisa.

Baada ya hapo tena ikawa mzee anajilia kwa ulaini kabisa kama ameoa. Baada ya miezi kama mitano hivi dada akapata homa, akatibiwa akapata nafuu, lakini homa zikawa hazimuendei mbali.

Baba akaamua akapimwe HIV, majibu yaliporudi dada alikua mwathirika. Kumbe huko alikotoka alifiwa na mume, watoto alimuachia mama yake ili yeye akatafute kazi.

Baba alichanganyikiwa, aliamua kutafuta dada mwingine, ila huyu alishindwa kumuondoa, akawa anamhudumia mpaka hali ilipozidi kuwa mbaya ndiyo akamrudisha kijijini kwao. Baba alipima akajikuta na yeye ameathirika. Aliendelea kulea watoto wake mpaka mke wake aliporudi.

Mama aliporudi, baba alimkalisha mke wake na kumueleza kisa chote, alimwambia mke wangu pamoja na kuwa ninatumia dawa lakini ni vyema tusikutane.

Nisingependa tufe wote tuwaache watoto bila wazazi. Baada ya hapo waliendelea kuishi mama akiwa analala na binti zake.Pamoja na kuwa baba alitumia dawa za ukimwi lakini msongo wa mawazo ulichangia kifo chake.
 
nilikuwa na appoitnment na mchepuko mida ya saa 3, sasa baada ya kusoma mada yako imenitisha, ila ngoja niagize ya bardiiiiii nisahau halafu niende tu.

Kama umeamua kwenda basi ukumbuke kuvaa combat.
 
nilikuwa na appoitnment na mchepuko mida ya saa 3, sasa baada ya kusoma mada yako imenitisha, ila ngoja niagize ya bardiiiiii nisahau halafu niende tu.

hahahahaha.... nikimiss kucheka huwa nakuja JF...
 
huu ugonjwa umewekwa mahali pabaya sana aisee...
 
Hii kitu sijui ikoje unagonga mchepuko unanogewaaa !ukikumbuka ngoma unasema sirudii tena!nikionana naye hata kwenye daladala nashuka..........wiki tu ukikumbuka mautamu anayokupa unampigia simu. Hakika duniani tupo kwenye mtihani wa maisha!!!!!!
 
mmh bibi safari wa the citizen tv alielezea hayo yote leo jioni. mmmh
 
Hii kituu.. Hehee, it moves mountains and dries oceans..
 
ila wanandoa kuwa mbali mbali hata dar-moro ni kutiana majaribuni jamani! Ni kwa kuwa tu hatujui kusoma alama ila kitendo cha housegirl wa siku zote kuaga wakati mama anataka kwenda ulaya kilikuwa ni ishara kuwa mama atafakari upya swala zima la kuondoka na kuacha familia. Mama ndo mlinzi wa familia atii. Unapataje usingizi ukifikiria umeacha wanao na "stranger"? Kuna fursa ambazo huwa naamini zinapatikana zaidi ya mara moja. Shule na scholarship ni mbiliwapo. Hivi unafikiri huyu baba ingekuwa ndo kaenda huko ughaibuni mama angebabaika kiasi cha kunywa bia kupunguza upweke? Unaachaje familia na mtu ambaye hujachukua muda wako kumchunguza na kuridhika nae? Wengine muongeleeni baba, wengine housegir. Mimi nimechagua kumuongelea mama.
 
Kama umeamua kwenda basi ukumbuke kuvaa combat.

Kombati inategemea mimi kunabwana alikuwa na demu watu wakamweleza demu nimwathirika jamaa akaonyesha kondomu. Baada ya mda kupita tukiwa darasani na nje inapopigwa story za HIV jamaa anakosa raha kabisa kumbana vizuri akakiri hakutumia kwakuwa demu aligoma hii nihatari
 
Aliyeenda Australia alikaa muda gani...
 
ila wanandoa kuwa mbali mbali hata dar-moro ni kutiana majaribuni jamani! Ni kwa kuwa tu hatujui kusoma alama ila kitendo cha housegirl wa siku zote kuaga wakati mama anataka kwenda ulaya kilikuwa ni ishara kuwa mama atafakari upya swala zima la kuondoka na kuacha familia. Mama ndo mlinzi wa familia atii. Unapataje usingizi ukifikiria umeacha wanao na "stranger"? Kuna fursa ambazo huwa naamini zinapatikana zaidi ya mara moja. Shule na scholarship ni mbiliwapo. Hivi unafikiri huyu baba ingekuwa ndo kaenda huko ughaibuni mama angebabaika kiasi cha kunywa bia kupunguza upweke? Unaachaje familia na mtu ambaye hujachukua muda wako kumchunguza na kuridhika nae? Wengine muongeleeni baba, wengine housegir. Mimi nimechagua kumuongelea mama.

Mama aliamua kwenda kusoma pia kwasababu ya kuimarisha kipato cha familia. Katika hatua za mwisho za safari hakuwa na muda ya kutafakari consequences. Hata hivyo alimuamini mume wake.
 
Back
Top Bottom