Yale yale ya mwaka 70

Yale yale ya mwaka 70

Mafweza ze don

Senior Member
Joined
Feb 9, 2013
Posts
148
Reaction score
182
Habari zenu wana JF,

Bila kupoteza wakati ningependa moja kwa moja niende kwenye swala linalo nisumbua kwa wakati huu nikihitaji ushauri na msaada wa mawazo kutoka.

Kuna binti ambaye ni mpenzi wangu ila mpaka sasa siamini kama ni wangu tena nmekua nae kwenye mahusiano kw mda wa miezi 7 sasa na kwamuda wote huo nilijitahidi kumfanyia kila anacho taka bila kujali chochote kabla yakua nae kwanza alisha nitoleaga nje kama miaka 4 iliopita.

Lakini mwisho wake nlifanikiwa kuteka moyo wake na nikasema i'll never let her goo but sasa naona kauli yangu inanizidi nguvu yeye anakaa kwake na mimi kwangu ila siku hizi kila ikifika mda wa saa mbili usiku nikimpigia mara asipoke kama jana ndo kabisa hadi akaizima lakini ikifika saa nne anakua available.

Sasa jana akaniambia simu ilikua on labda tatizo ni network nikimbana vizuri anakujaa juu anakua mkali na ananikatia simu na uwezo wakuonana nae sina sababu tumetengana kidogo mikoa ila ni kikazi namipango yetu ilikua ni kufunga ndoa baada ya muda kidogo ila ndo hivo mrembo ameanza kubadilika.

Jambo hili laniumiza kichwa sana naombeni ushauri wenu ndugu zangu

HUYU MTU ANANIA NJEMA KWELI NA MIMI?
 
hana nia njema na wewe kabisa yaan haswa haswa hao mitandao ya simu haiwzekan mtandao usipatikane kabisa kwa masaa mawili hebu fanya kumnunulia line ya mtandao mwengine kabisa haya makampuni ya simu yana shida sana aisee
 
Wewe unamzimia kimapenzi, na yeye kaamua kukuzimia "simu"!
 
Keshapata bwana mkuu...fanya yako achana naye huyoo
 
hata ,buyu uliana kama mchicha kusoma hujui basi hata kutazama picha napo?
 
Ana nia njema kabisa na wewe, anataka uwahi kufa ili uepukane na matatizo ya dunia hii, je hiyo sio nia njema? Anakupenda
 
wanawake wengi wanaoishi maisha ya kujitegemea kabla ya kuolewa ni wahuni sana, wanapigwa sana game za fasta na marafiki zao wa kiume wanaowatembelea.
 
Anayezungusha mimi ndiye huwa nampenda,sipendi Maharage ya Mbeya
wanakuzungusha ndiyo maana unakuta demu amekusoma vya kutosha halafu anaaanza kuangalia nitafaidi nini kwako akiona amana ndiyo kukubali kukwepa kero na kuanzisha timbiri after makubaliano... mtazamo tu
 
Habari zenu wana JF,

Bila kupoteza wakati ningependa moja kwa moja niende kwenye swala linalo nisumbua kwa wakati huu nikihitaji ushauri na msaada wa mawazo kutoka.

Kuna binti ambaye ni mpenzi wangu ila mpaka sasa siamini kama ni wangu tena nmekua nae kwenye mahusiano kw mda wa miezi 7 sasa na kwamuda wote huo nilijitahidi kumfanyia kila anacho taka bila kujali chochote kabla yakua nae kwanza alisha nitoleaga nje kama miaka 4 iliopita.

Lakini mwisho wake nlifanikiwa kuteka moyo wake na nikasema i'll never let her goo but sasa naona kauli yangu inanizidi nguvu yeye anakaa kwake na mimi kwangu ila siku hizi kila ikifika mda wa saa mbili usiku nikimpigia mara asipoke kama jana ndo kabisa hadi akaizima lakini ikifika saa nne anakua available.

Sasa jana akaniambia simu ilikua on labda tatizo ni network nikimbana vizuri anakujaa juu anakua mkali na ananikatia simu na uwezo wakuonana nae sina sababu tumetengana kidogo mikoa ila ni kikazi namipango yetu ilikua ni kufunga ndoa baada ya muda kidogo ila ndo hivo mrembo ameanza kubadilika.

Jambo hili laniumiza kichwa sana naombeni ushauri wenu ndugu zangu

HUYU MTU ANANIA NJEMA KWELI NA MIMI?

Dah aisee we tafuta mwingine tu kaka
 
Me hata sielewi unataka ushauriwe nini hapo ilihali kila kitu kiko open.
 
una umri gani??? ......mhm ngoja nipite mpaka ufike muda wa nyie kwenda chuo...
 
ni kujiendekeza tu coz before her you had a life, mtu umekutana naye ukubwani akusumbue akili
 
Back
Top Bottom