Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,895
- 2,777
Nimekaa nikawaza kidogo na kujiuliza hili swali. Yawezekana yaliyonisababishia kuwaza haya nimeyapitia jana, juzi, miezi kadhaa, ama miaka kadhaa nyuma.
mapenzi ya wawili waliokutana kwa bahati. Waliotafutana kwa mikiki na visiki vingi hadi wakawa pamoja. Nazungumzia yale mapenzi yaliyokuwa machanga enzi hizo. Yapo? Yako wapi sasa? Yale mapenzi ya kulishana kama njiwa. Ya kuwaziana mema mwanzo mwisho. Ya kuhofia kuachana. Ya kugandana kama kumbikumbi.
Hivi huyo uliye naye ndiye yule aliyekufanya kukosana na wazazi wakati fulani?
Ndiye yule aliyekufanya roho ipae ukimwona?
Ndiye yule aliyekufanya roho ipasuke ukisikia jina lake?
Ndiye yule aliyekusababishia kuwa mnadhifu wakati wote?
Ndiye yule aliyekujazia tabasamu usoni na moyoni wakati wote?
Ndiye yule aliyekupa ganzi ya hisia usisikie wala kuona?
Ndiye yule ambaye harufu ya manukato yake ilikutikisa kwa mahaba?
Ndiye yule miezi/miaka michache nyuma mlipeana ahadi zisizotekelezeka?
Ndiye yule ambaye mlikaa enzi hizo mkapanga familia yenu iweje? Imekuwa?
Ndiye yule? kama ndiye yule una kheri. Kama siye, kabadilika nini? Nini kimembadili? Wakati fulani tunatamani kurudisha wakati nyuma japo tuonje tone la yale tuliyopitia katika ulimwengu wa mapenzi. Inashindikana. Kwa nini inashindikana? Chanzo cha kushindikana ni nani? Kuna jambo au mambo yaliyochangia nyie kufikia hali mliyo nayo (kuachana ama kuwa na uhusiano wa mashaka). Pengine unajua sababu. Pengine mnashangaa kwa nini mmefika hapo.
Ulishawahi kumuuliza, 'hivi kwa nini tumefika hapa, mpenzi wangu?' Kwa nini hili litufikishe hapa? Nimebadilika nini? Sikuvutii tena? Siamshi hisia zako kama awali? Nini kimesababisha tufikie hapa? Ni watoto? Ni ndugu? Ni ukapa? Kuna msaidizi wangu huko nje? Ni nini basi? Yako wapi yale mapenzi? au ni utu uzima?
Kwa nini tuishi kwa mazoea?
Kwa nini faraja yangu iwe watoto pekee? Kwa nini isiwe wewe tena?
Kwa nini faraja yangu iwe marafiki zangu?
Kwa nini faraja yangu iwe pombe?
Kwa nini faraja yangu iwe ni kuchelewa kurudi nyumbani?
Kwa nini faraja yangu iwe hawara?
Kwa nini faraja yangu isiwe wewe tena?
Najua mpo mnaokumbana na haya. Hitimisho la simulizi hii ni wewe kuchukua hatua kwa kadiri inavyostahili, ukiakisi katika wakati uliopita. Kipidi kile mnakesha kwenye mbalamwezi mkiimbiana mashairi mazuri na kulisha ndimi. Leo zimekuwa chungu? Muulize, je, unakumbuka?