Yako wapi matawi ya CCM London na Washington DC?

environmental

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
1,054
137
Ndoto nyingi za waliozoea kupata mapande katika keki ya taifa ilikuwa kujikomba kwa CCM walifungua matawi ya ccm miji Mikubwa Duniani ikiwa ni kama chanzo cha kujionyesha kwama wanafanya shughuli za kichama. leo hii na madudi yote ya CCM sijui wamejificha wapi , mhamasiko wao umepungua kwa kasi ya ajabu. Sijui mwana CCM jasiri aniambie anajivunia nini na chama Chake? Wengi waliamini ili upate ubunge ni vema uingie CCM lakini wawaulize majeruhi wa CCM kama Lawrence Masha. mageuzi tanzania ilikuwa safari ndefu lakini imewezekana wako walio simamia hilo mda mrefu na wala hawajawahi kununulika, kuna waliofika bei kama Lamwai, Kaborou, Makongoro. Ila ukweli ni kuwa kama haya mageuzi yanakuuma wewe utakuwa mnyonya damu,
 
Mwenzao Le Mutuz Baharia Big show amefungua matawi kibao lakini akashindwa ku replicate mambo ya NYC akaishia kutembeza rushwa watu wameramba fedha wakamnyima kura asirudie tena na EALA ataisikia bombani
 
Hahahahhhaha Le Mutuz kashakoma. matawi yamegeuka genge la kahawa huko yaliko!
 
Yuko kiongozi mmoja tawi la London nilikutana naye Bongo akasema ameachana na mambo ya ccm maana amegundua ni ubabaishaji tu.... sijui kama bado anadunda mbele au hii ya William imewaogopesha??
 
Le mutuz, baharia, Big show, Field Marshal, Willy, Le grand mutuz, Papa NYC,
Huyu angekuwa Mkongoman hakika tungeona mengi.
Kina Patcho Mwamba a.k.a tajiri wanacheza tu.
 
Mkuu jfforjamii ni kweli mageuzi yamepitia safari ndefu na yenye maumivu makali lakini yamefika! Hawa jamaa waliofungua matawi nje ilikua kuganga njaa,ni kama baadhi ya watendaji wa ngazi ya juu serikalini walipokua wanakaribia ama kustaafu wanaenda kugombea ubunge kupitia CCM wakijua watapita tu! Sasa wajaribu 2015 waone moto utakao wawakia.
 
Hawa ccm London wamekuwa ccm Reading nadhani na wa Washington DC na NY walianzisha matawi kwa kutafuta ulaji. Walidhani kwamba watapata nafasi ya kwenda kugombea ubunge Tanzania. Wengine waliojaribu wakatoswa na ccm wamekata tamaa. Lakini hata matawi yote yalianzishwa kama njia nyingine ya ufisadi make matawi hayako katiba ya ccm na hata kisheria hayakidhi za nchi Uingereza na marekani yaani kuwa na tawi la kisiasa katika nchi ya kigeni. Matawi haya hayawezi kusajiriwa kisheria. Lakini pia matawi haya hayajulikani yana-belong wapi? i.e mkoa, wilaya, kata, tawi etc. Ama hayana uwakilishi wowote katika vikao vya wilaya, mkoa au taifa kama vile NEC, EC etc. Cha zaidi haifahamiki kiwango cha kadi ya ccm nje ya nchi kilipangwa na nani make hakimo katika katiba ya ccm? Kadi ya ccm tanzania inalipiwa kwa Tshs 300 na ada ya Ths 100 kwa mwezi lakini nje ya nchi kuanzia £12 hii ni aina nyingine ya wizi na hata hela inayopatikana haijulikani inatumiwaje make hakuna vikao vya kusoma mapato na matumizi. Saa nyingine akina Jamal Malinzi ndio walikuwa wanafadhili matawi haya. Sasa sijui kwa sasa kama Nape anawamegea fungu!!
 
uchaguzi 2015 utakuwa kinyang'anyiro cha nguvu sana hasa majimboni wananchi wamehamasika kiasi cha kutosha ila cha ajabu Dar na Dom watakuwa wamwisho kwenye haya mageuzi.

Mkuu jfforjamii ni kweli mageuzi yamepitia safari ndefu na yenye maumivu makali lakini yamefika! Hawa jamaa waliofungua matawi nje ilikua kuganga njaa,ni kama baadhi ya watendaji wa ngazi ya juu serikalini walipokua wanakaribia ama kustaafu wanaenda kugombea ubunge kupitia CCM wakijua watapita tu! Sasa wajaribu 2015 waone moto utakao wawakia.
 
uchaguzi 2015 utakuwa kinyang'anyiro cha nguvu sana hasa majimboni wananchi wamehamasika kiasi cha kutosha ila cha ajabu Dar na Dom watakuwa wamwisho kwenye haya mageuzi.
Hii Millard miwilu ni kama haina wenyeji, swhemu kubwa ya wakaziwake ni wageni, wenyeji wa mikoa hawahasoma wamekimbilia vijia maendeleo
 
Wana JF najiuliza yale matawi ya CCM yaliyoko ughaibuni yako wapi katika hiki kipindi ambacho chama chenyewe kinaonekana kiko gizani? Msimamo wao katika masuala ya rushwa zinazoendelea huko nyumbani ni upi au hawa wanachama ni opportunist tu wanasubiri kudaka wanachodondoshewa na watawala na watafuna uchumi wa Tanzania??! Nafikiri kama kweli wana dhamira ya dhati na mapendo ya dhati kwa nchi yetu wangekuwa wanatoa matamko walau kukemea au kuunga mkono sera zinazoendelea huko nyumbani. Humu JF hawa jamaa wapo watuambie msimamo wao??
 
hili ni swala muhimu sana naona linakkwepa kujadiliwa
 
Huu ndio ulikuwa upuuzi wa mwanzo mwisho. wewe unaanzisha tawi la CCM ughaibuni ili iweje? Utafikiri mpigania uhuru wakati uhuru unao.
Amini usiamini, hii ni aibu sana na badala ya kuisaidia CCM, ufunguzi huu wa matawi umefanya CCM ichukiwe na wengi huko ughaibuni fanyenyi utafiti wenu polepole muone.

Nape pigeni marufuku mambo ya hivi. Anayetaka kuwa Kiongozi, njoo kijiweni huku shirikiana na wenzako huku Bongo matawi yako kibao ambayo hayana mwelekeo.
 
Wapi William @ NY....okoa Jahazi!watu wameshaanza kupiga vikombe!
 
Kwa mwenendo wa mambo ya ccm sidhani kama kwa mtu mwenxe uchungu na Tz anaweza kushirikina nao ama kuwa nao tena, labda wanaoweza kuwa nao tena ni wale wenye maslahi yao binafsi na kuinyonya Tz tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom