Baada ya kuimaliza NCCR, Marando sasa aanza na CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baada ya kuimaliza NCCR, Marando sasa aanza na CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TandaleOne, Jul 27, 2012.

 1. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2012
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,617
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  JUMAMOSI iliyopita, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mabere Marando alinukuliwa akiwatetea wabunge wa chama hicho John Mnyika na Tundu Lissu, kwa kusema hawakutishia kumuua Mbunge wa Iramba Magharibi mkoani Singida kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Nchemba.

  Marando ambaye pia ni wakili wa kujitegemea na afisa wa zamani wa Idara ya Usalama wa Taifa (NSS), alisema siyo kweli kwamba wabunge hao walimtumia Nchemba meseji zenye ujumbe wa mauaji dhidi yake, vinginevyo aache kukifuatafuata chama chao katika harakati zake za kutaka kutawala mwaka 2015.

  Alisema badala yake, meseji hizo zimetumwa kwa mbunge huyo na mtoto wa kigogo wa CCM anayemiliki mtambo wa kuingilia mawasiliano ya watu kwa mbinu za kijasusi, lakini akashindwa kumtaja jina wala kuzungumza chochote juu yake.

  Huku akijitambulisha kuwa ni Kiongozi wa Idara ya Usalama na Upelelezi ya Chadema, alisema mtambo huo umenunuliwa nchini Israel, na kwamba umetumika kuandaa maneno na kuingilia mawasiliano ya simu za wabunge hao.

  “Nchini Israel kuna kampuni mbili; Verinty na Nice Systems, hizi zimegundua mtambo wenye uwezo wa kuingilia mawasiliano ya watu kwenye mitandao yao iwe intaneti au simu”, alisema.

  Nilibahatika kumfahamu vizuri Marando alipokuwa Katibu Mkuu wa chama cha NCCR – Mageuzi kati ya mwaka 1995 – 1999, wakati huo nikiwa mwandishi wa habari wa magazeti kadhaa nchini, hivyo nina mengi ninayoweza kuyaainisha juu yake ingawa sitaki kufanya hivyo katika makala hii kwa sababu siyo mahali pake.

  Ninachotaka kusema ni kwamba kama ni taaluma ya ushushushu aliyonayo basi amehitimu kwa mafanikio sana. Ana uwezo wa kumwibulia tuhuma mtu yeyote na kuziweka wazi hata mbele ya halaiki, akazungumza kwa makini na uhakika mdomoni mwake, lakini ukifuatilia baadaye unagundua bila mashaka yoyote kuwa ni uzushi.

  Ujuzi wake huo niliweza kuujua vizuri kati ya mwaka 1997 – 1999 alipokuwa akigombana kwa nguvu kubwa na Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR – Mageuzi, wakati huo, yule ambaye hivi sasa ni Mwenyekiti wa Taifa wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema.

  Lakini kwa vile naye ni shushushu na amewahi kuwa mpaka Afisa Usalama wa Taifa wa Wilaya (DSO) kule Kahama mkoani Shinyanga, fitina za Marando kisiasa kwa Mrema ziligonga mwamba hadi akakimbia yeye mwenyewe kutoka Makao Makuu ya NCCR – Mageuzi, Manzese Argentina jijini Dar es Salaam.

  Ukimwacha Mrema, viongozi wengine waliowahi kupandikiziwa chuki katika chama hicho na Ofisi ya Katibu Mkuu chini ya Marando ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Taifa wa Kitengo cha Vijana, Msafiri Metemelwa ambaye hivi sasa ni Mkurugenzi wa Taifa wa Kampeni na Uchaguzi wa Chadema na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Prince Bagenda.

  Wakati ambapo Mtemelwa alizushiwa kwamba anaongoza kikundi cha kigaidi cha Black Mamba ili kuwadhuru viongozi wanaompinga Mrema katika upande wa kwanza, Bagenda katika upande wa pili aling’olewa kutoka Kamati Kuu ya Chama, lengo likiwa ni kupunguza nguvu za mbunge huyo wa sasa wa Vunjo katika chombo hicho cha uongozi wa kisiasa.

  Inawezekana Mtemelwa na Marando katika kipindi hiki hawavutani wala kugombania tena jambo lolote la kisiasa na uongozi wakiwa wote Chadema, lakini mwanasiasa huyo kamwe hawezi kusahau yaliyomkuta ikiwemo kufukuzwa kwenye vikao muhimu vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya NCCR – Mageuzi, vyote vikifanyika kwa vurugu za kijinga kwenye Ukumbi wa Raskazone Hotel mjini Tanga kuanzia Mei 21, 1997.

  Mwingine ambaye hawezi kusahau vurugu za Marando za kisiasa ukiwemo uzushi, uongo na fitina kwa wapinzani wake ni pamoja na Harold Jaffu, Mjumbe wa Kamati Kuu ya NCCR – Mageuzi aliyekuja kuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho na hatimaye TLP chini ya Mrema baada ya Bagenda kuachia nafasi hiyo.

  Wengine ni pamoja na Thomas Ngawaiya aliyewahi kuwa Katibu Mwenezi wa Taifa wa NCCR – Mageuzi na TLP, Hamduni Marcel aliyekuwa Mkurugenzi wa Taifa wa Kampeni na Uchaguzi wa NCCR – Mageuzi iliyokimbiwa na kina Marando na Cosmas Chenyenge, yule ambaye naye alikuwa Mwenyekiti wa vyama hivyo kwa nyakati tofauti wa Mkoa wa Mwanza.

  Hao wote na wengineo wanamjua vizuri Marando kuwa kwenye siasa ni mzushi kiasi gani, mfitini wa daraja gani na rafiki namna gani, yule ambaye ana sura na rangi tofauti na yupo radhi na tayari wakati wowote na mahali popote kusema vyovyote, kuanzisha chochote na kung’ang’ania jambo lolote ili mradi tu anakidhi matakwa yake ya muda huo bila kujali kutatokea nini baadaye.

  Kama ni kazi ya kutengeneza maneno mezani, kuyamwaga hadharani na kufanana na ukweli basi Marando amefuzu. Aliweza kumfitini Mrema na kila kiongozi aliyekuwa akimuunga mkono walipokuwa wote NCCR – Mageuzi, lakini dhambi hiyo ilikwenda naye sambamba hadi chama hicho kikasambaratika kama kishada kilichokwenda harijojo!

  Kilikufa kama kibudu hadi mwenyewe akapoteza mvuto hata kwa wanachama, marafiki na viongozi aliokimbia nao kutoka Manzese Argentina, wakahamia Kisutu ambako walifungua ofisi mpya ya Makao Makuu ya NCCR – Mageuzi huku wakikomba ruzuku yote ya chama.

  Ushahidi wa suala hili ni pale alipotaka kurudi tena kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR – Mageuzi kupitia uchaguzi mkuu wa chama hicho wa mwaka 1999. Katika zoezi hilo ambalo lilifanyika kwenye Ukumbi wa Chuo cha Bandari, Tandika jijini Dar es Salaam, Marando na aliyekuwa rafiki yake wa karibu, Dk. Masumbuko Lamwai walitupiliwa mbali na nafasi hiyo ikachukuliwa na James Mbatia ambaye bado anaendelea nayo hadi sasa.

  Katika kutaka kwake kuwatetea Mnyika na Lissu kwamba hawahusiki na vitisho vya mauaji dhidi ya Nchemba, hakika shushushu huyo wa zamani wa serikali anajaribu kutwanga maji kwenye kinu, kazi ambayo kwa vyovyote siku ya mwisho itakuja iwe tasa.

  Anajaribu kuogelea kwenye bahari yenye kina kirefu cha maji huku mawimbi makali na tena usiku wa manane yakimpiga usoni. Anataka kuwaokoa kutoka kwenye korongo lenye giza nene, lile ambalo bila kutumia umeme hata akikesha anamulika kwa tochi ya betri 10 hawezi kuona mlango wa kuweza kuwatolea.

  Kama alivyoshindwa kumng’oa Mrema kutoka katika uongozi wa juu wa NCCR – Mageuzi, akajaribu kumvuruga mpaka kisaikolojia wakiwa kwenye kikao cha NEC kule Tanga, lakini akakimbia yeye mwenyewe usiku wa manane, akahamishia ofisi uchochoroni kutoka Makao Makuu yaliyoandikishwa kisheria; hakika hata juhudi hizi za kutaka kuwaokoa kina Mnyika na Tundu Lissu nazo zitakwama.

  Anataka kuitumia nafasi hiyo kusaka umaarufu kwa kudai kuwa ametumia ushushushu wake akiwa ni Kiongozi wa Idara ya Intelijensia ya Chadema, akazichunguza tuhuma hizo kwa siku tatu tu na kugundua kwamba kuna mtoto wa kigogo wa CCM anayemiliki mtambo wa kufanyia ujasusi dhidi ya watu wengine.

  Sitaki kuaminishwa uongo na kielelezo siyo kutaja majina ya makampuni yanayotengeneza mitambo hiyo kwa sababu hata kompyuta inafahamika wapi zinatengenezwa duniani, halafu hata Marando mwenyewe anazijua ni kampuni gani zinatengeneza na kuuza ndege za aina zote za Gulf Stream, Air Bus, Boeing, Fokker Friendship, Twin Otter na kadhalika, hivyo anaweza pia kusema chochote akitaka kuibua uzushi wowote kwa kutumia makapmuni hayo kama kigezo cha kuhalalishia uongo wake.

  Kama hawadanganyi Watanzania basi atutajie majina kamili ya mtoto huyo wa kigogo wa CCM aliyenunua mtambo huo, aseme ilikuwa lini kwa maana ya tarehe, mwezi na mwaka gani, saa ngapi na atuonyeshe pia risiti ya mauzo hayo na ikiwezekana atuambie hata jina la afisa aliyehusika katika kuuza mtambo huo kule Israel.

  Ataje mtoto huyo wa kigogo wa CCM aliondoka Tanzania tarehe ngapi, mwezi gani, mwaka gani na alitumia usafiri gani kama ni wa anga au meli na shirika lake, linamilikiwa na nani na kutoka nchi gani, alianzia wapi safari yake, saa ngapi, alipitia wapi na Israel alifika muda gani.

  Aseme alifikia uwanja upi wa ndege au bandari gani nchini humo, akaishi huko kwa muda gani akiwa hoteli gani kabla ya kurudi Tanzania. Ataje pia usafiri aliotumia kwa safari hiyo na takwimu nyingine zote kwa wasafiri wa kigeni wanaokwenda na kutoka nchi nyingine.

  Bila kufanya hivyo atakuwa anajaribu tena kurudia kazi iliyomshinda kwa Mrema, halafu akashindwa pia kurejea madarakani kama Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR – Mageuzi kwa awamu ya pili. Akagaragazwa vibaya na Mbatia hadi akatimka kutoka chama hicho na kujisalimisha mwenyewe Chadema.

  Endapo amebobea katika uzushi wa kisiasa, majungu na fitina zake sasa namuomba asidhani Watanzania wote ni zezeta wa kufikiri au kutafakari vichwani mwao. Inabidi atafute namna mpya inayoweza kuwaokoa Mnyika na Tundu Lissu kama anataka aendelee kuaminiwa kuwa Kiongozi wa Idara ya Intelijensia ya Chadema.

  Kubaki ameng’ang’ania uongo huo hatimaye ataaibika na kama alivyosema Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Nape Nnauye, shushushu huyo ni mzushi aliyewahi kumsingizia hata yeye, lakini alipombana akaomba radhi kwa maandishi kuwa alishinikizwa kufanya hivyo…“Hata haijapita angalau miezi mitano tu hivi anatoa uzushi mwingine”, anasema.

  Huyo ndiye Mabere Marando, Katibu Mkuu wa zamani wa NCCR – Mageuzi aliyeongoza harakati za kukimaliza kisiasa chama hicho kuanzia mwaka 1997 – 1999, yule ambaye sasa anatetea uozo utakaoisambaratisha Chadema kwa kutumia uzushi mwingine!
   
 2. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Mkuu naona umeandaa Insha ndefu kwaajili ya kumfurahisha aliyekutuma hatuna muda ya kusoma labda convert kwenye audio uweke kwenye Youtube usambaze TBC na Redio Tanzania Bila kusahau Redio Uhuru
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Nilijua tu Marando alikuwa anazusha ,katika ile meza ukimuangalia Dr.Slaa alikuwa ana wasiwasi sana na yale aliokuwa akizungumzia Marando.
  Mwandishi amewaonya CDM wawe waangalifu na huyo jamaa la sivyo anaweza akawazamisha na kuwaacha kwenye mataa baada ya kumaliza kazi iliyomleta hapo.
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kwa kuona jina la Mleta mada na Title yenyewe nimeona ni uzushi ns uswazi.
   
 5. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #5
  Jul 27, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Huu si muda wa porojo tena, watanzania wanataka ukweli na si propaganda...

  Swali langu dogo ni kwamba kama wewe wakatio huo ulikuwa unamwona marando ni mbaya maanake ulikuwa CCM, kama wewe hata leo unamwona marando mbaya hata kama kasema vibaya maana yake wewe ni CCM.

  Haijalishi utaandika nini, kuhusu kiongozi wa upinzani basi bado wewe ni unatetea ufisadi huu uliokithiri ndani ya nchi yetu kwa mizizi ya kulindwa sana na kwa gharama zozote na wana CCM kama wewe..

  Maelezo mengi lakini mwishowe unataka eti amtaje huyo mtoto wa kigogog wa CCM so what wakati hata waliomteka Dr Ulimboka wametajwa badala yake wamefichwa, walioiba fedha za Epa wametajwa lakini hadi leo wapo uraiani wanakula raha,

  Huo ni unafiki wenu tushawazoea, au unataka kuhakikisha kama ni wewe au la????
  Hakuna mtakachokifanya ndani ya TZ hii tusiijue, labda vikao mkafanyie mwezini.
   
 6. M

  Molemo JF-Expert Member

  #6
  Jul 27, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Umejionyesha umasikini wako wa kufikiri kwa kupoteza muda wako kuandika upumbavu kama huu.
   
 7. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #7
  Jul 27, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Watu wengine mna muda wa kuchezea..
   
 8. Nkamu

  Nkamu JF-Expert Member

  #8
  Jul 27, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 206
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mimi nimesoma kama tamthilia nzuri sana! Sijui itaendelea lini!?
   
 9. m

  manucho JF-Expert Member

  #9
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 3,410
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Wajinga wengine bana, kaanzishe gazeti lako huko tandale, hivi bi nyau yupo?
   
 10. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #10
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160

  Kwa jinsi ulivyoandika habari ndefu bila shaka Vasco da Gama dhaifu anaweza kukuajiri ukawa muandika spichi zake za wale wazee wasiojijua wa dar CCM
   
 11. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #11
  Jul 27, 2012
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,617
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Irrelevant fact to the fact on issue...,uko completely OP...!
   
 12. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #12
  Jul 27, 2012
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,617
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  wakiwa ni sehemu ya TANZANIA tena ndio wajenzi wa msingi imara wa TAIFA hili, nitajisikia faraja kuandika speech kwa ajili yao.
   
 13. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #13
  Jul 27, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Mkuu muda umefika tuwahi kabla vitu havijapoa nahamu na tambi na Magimbi kichizi
   
 14. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #14
  Jul 27, 2012
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,617
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Bi nyau Haishi Tandale..,hilo jina sijawahi kulisikia hapa kwa TUMBO...!
   
 15. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #15
  Jul 27, 2012
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,617
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Itaendelea siku MARANDO atakopouthibitishia UMMA kuwa amesema uongo...!
   
 16. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #16
  Jul 27, 2012
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,617
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Unaweza kujilazimisha kufikiri zaidi ya hapo.,uko mbali sana na 'ufahamu'
   
 17. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #17
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Sasa CCM tatizo lenu nini kama chadema ikizama...
   
 18. m

  manucho JF-Expert Member

  #18
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 3,410
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ndiyo line moja hiyo kwa mtogole mpaka unatokea mapipa, kama bi nyau hujawahi kumsikia vp kwa tumbo harufu imeisha siku hizi
   
 19. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #19
  Jul 27, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,017
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  dah! JF ni great thinker mkuu,hoja yako ni dhaifu sana na haina mashiko....kafturu afu ujipange upya,We never know labda njaa inakusumbua:wave:
   
 20. m

  manucho JF-Expert Member

  #20
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 3,410
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Uwanja wa fisi vp, bado libeneke linaendeleaga kama zamani zile nyama za kidizain niajeniaje zipo bado? Mkesha nini vp upo
   
Loading...