Yajue Maujanja ya Computer hapa(should see this): No 1

Hapa ngoja nimwage maujanja kidogo ninayoyafahamu, najua wengi mnafahamu lakini kwa wale wasiojua basi tukumbushane hapa. Ni maujanja ujanja tu. Haya tuanze sasa.

1. Kuongeza spidi ya intaneti.
Kama unatumia broadband(BB) connection nyumbani na unatumia window XP kama OS, na unahisi kwamba BB spidi yako ni ndogo, sasa hapa unaweza kuongeza spidi up to 20%. Kivipi?
-Hakikisha umelog in kama administrator -Anza kwenye Start-> Run -> gpedit.msc, bonyeza OK.
-Nenda kwenye Computer Configuration -> Administrative Templates -> Network -> QoS packet Scheduler.
-Kwa upande wa kulia utakuta hii option Limit Reservable bandwidth
-Ingia hapo na bofya 'Enabled'...kwenye value(nadhani inakuwa 20)...badilisha,weka 0(zero).
-Apply then bofya OK..
.Kushney.

2. Kupata XP key kutoka kwenye CD yake.

Hapa huna haja ya kuhangaika kutafuta product key za XP wakati unataka kuistall OS kwenye system yako.
Cha kufanya: Fungua(explore) CD yako, halafu fungua folder I386. Baada ya hapo fungua file limeandikwa UNATTEND.TXT, Scroll mpaka chini kule kuna utaona uhuni wa watu wa Microsoft ulipolalia. You have done it.
Kushney

3. Hii inaitwa "EXTREMELY FAST BOOTUP"

Hapa kama computer yako inachukua muda mrefu kuwaka, basi njia hii ni dakika sufuri tu, kitu kishawaka.
Kivipi...fuatana nami hapa:
-Kwanza iwezeshe hibernation.
-Nenda kwenye control Panel
-Chagua Power option
-halafu enable hibernation(tia tick hapa),
-Baada ya hapo,fanya hivi, nenda kwenye start->turnoffcomputer button->Bofya shift halafu then on hibernate
Press shift button after you click 'Turn Off Computer' in start menu.
Kushney.

4. Kubadilisha jina la Recircle bin.
-Kwa hali ya kawaida huwezi ku-rename hili folder. Ila kwa maujanja haya unaweza kulifuta hilo neno na kuandika neno lingine lolote utakalo.
Kivipi?Fuatana nami hapa:
Fungua command box hivi: start->run->hapa andika regedit HKEY_CLASSES_ROOT/CLSID/{645FF040-5081-101B-9F08-00AA002F954E} na badilisha jina la "Recycle Bin" kwenda kwa jina lolote unalotaka (hakikisha usiandike quotes yoyote kwenye hilo jina).
Kushney.

Kwa leo tuishie hapa...hili somo litaendelea siku nyingine(Part 2,3,4,5...nk).
Jumapili Njema
1qs8et.gif
2u7ow7c.gif
 
Back
Top Bottom