Jinsi ya kufanya computer yako ikiwaka ikuite jina lako

mjumbe wa bwana

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
5,188
6,011
MUONGOZO WA KUFANYA ILI COMPUTER YAKO DESKTOP AU LAPTOP IKUITE JINA PINDI UNAPOIWASHA (IKUKARIBISHE).

Habari za weekend wana IT..? Naamini kila mmoja angependa kuona pc au computer yake ikimuita Jina Lake (Kumkaribisha) pindi anapoiwasha, kama unapenda mm pia ni mmoja wa watu hao.

Lakini sio kazi rahisi kufanya hili, ila kama unataka kufanikisha hilo fuata hatua hizi nitakazotoa ili kuweza kuicomand computer YAKO Kubwa au pc IKUITE JINA lako pindi tu inapowaka.

1. Nenda sehemu ya kusearch na uandike notepad au njia rahisi bonyeza Windows button na R kwa pamoja then andika notepad then ENTER.

2. hatua ya pili ikifunguka notepad, unatakiwa kucopy code maalum na uzipaste Kwenye hiyo notepad uliyoifungua. Code zenyewe ni:

Dim speaks, speech
Speaks="Welcome to your PC, username"
Set speech=CreateObject("sapi.spvoice")
Speech.speak speaks

Hizo ndio code unatakiwa kuzicopy kama zilivyo nilivyoweka, Kisha hapo Kwenye username futa then andika Jina lako unataka pc ikukaribishe pindi inapowaka... Wale wenye majina ya kingereza kama John, paul, Anna, Kelvin.nk watafurahia sana.

Maana sio kila jina linatamkwa inavyotakikana pindi ukifanikiwa kufanya hili.. Wale wenzangu na mm sasa...!!! Natania, but majina mengine ni ya kibantu(kitamaduni) au ya ukoo. Hvyo ukiicomand computer yako itaita vile inataka, maana maneno yalliyolengwa kutumika humu ni ya kingereza.

Ndio utamkwa vizuri.. Mfano mm niliweka Hello Mr but likatamkwa vizuri, unaweza kuicomand computer ianze kuita kiswahili paia.. Utaondoa neno "WELCOME TO YOUR PC" THEN unaweza kuandika "KARIBU SANA AU KARIBU.." Then itafuatia na kukukaribisha . So inaweza kuanza kukuita kwa kiswahili au kingereza. Mf Karibu Sana John. Or welcome to your Pc john..

3.Hatua ya Tatu unatakiwa uende katika sehemu iliyoandikwa FILE, sehemu hii ipo juu kushoto katika notepad.. Then chagua SAVE AS.

4. ikifunguka itakuletea kama kijisehemu ambacho utatakiwa kusave file lako sehemu hii utaandika WELCOME.vbs then Kwenye "save as type" chagua All Files Kisha bonyeza save Kisha funga hiyo notepad.... Ila kumbuka hilo file utakuwa unalisave wapi maana litahitajika.... Ila watumiaji wengi wa window 7 file hili utalikuta katika documents..... Na hapa niwakumbushe tu watumiaji wa window 7 kuwa microsoft wameshasitisha kutoa new updates, na mipangilio mipya ya window 7. Kwa sasa watumiaji wa window 7 wanaweza kutopata window 7 genuine.. Yaaani window 7 inaenda kupitwa na wakati kama zilizokuwa zamani mfano xp, nk. Kuna jamaa aliniletea pc yake, yenye window 7, Akadai inaleta sana ujumbe kuwa anatakiwa kuiupgrade kwenda window ten au updates. Nikamwambia anatakiwa kuibadili tu, maana window 10 na ubuntu ndio nzuri sana, hususan kwa ulinzi.. Ngoja tuachane na window ili tuendelee na makala yetu..

5. Hatua inayofuata nenda ulikosave hilo file litakuwa na alama ya S.. Kisha licopy alafu nenda local disc c:/documents and setting /all users/start menu /programs/start up na Uta paste Hilo file hapo katika start up (hii ni kwa wale wanaotumia Windows XP). Sidhani kama wapo humu, ila kama wapo basi nimewapa faida, maana nalenga kila mtu ajue, ila kama kuna mtu anatumia windows Xp, mpaka karne hii.. ni zamani.
Kwa wanaotumia Windows 7&8&8.1 na win 10 kama mm nenda local disc c then users.

(username),Appdata/Roaming /Microsoft /Windows /start menu /programs /start up then paste file ulilocopy hapo. Hapo Kwenye user utakuta Jina lako na public, achana na public Ingia hapo ktk Jina lako uliloweka wakati unaweka window. Ila cha muhimu kingine kuwa wanaotumia window 7 hawataiona AppData, hivyo watatakiwa kwenda Kwenye sehemu ya kusearch nakuandika hidden files folder na wachague show hidden folders the watabonyeza apply then OK na File La AppData litaonekana.

6. Kisha nenda Kwenye control panel then "sound and devices" then "sound" then Kwenye sound scheme chagua "no sound" Kisha apply na bonyeza ok, hapo utakuwa umemaliza Kisha restart computer yako ili ikukaribishe kama utakuwa umefuata Hatua zote vizuri.

Ukifanikiwa basi usiste kuja kutoa mrejesho hapa, ili nijue na kama kutakuwa na changamoto yoyote, basi kama kawaida yetu wana IT tutaelekezana wala msijari..

ISHI KITEKNOLOJIA.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom