Kahumbi Lumola
JF-Expert Member
- Mar 3, 2012
- 359
- 2,569
Mimi ni Waziri Mkuu wa serikali ya wanafunzi DIT, Lumola Steven Maziku KAHUMBI. leo nataka nichangie maoni yangu kwa uchache kuhusu TAHLISO yetu, kisha nitaweka wazi mimi nipo katika kundi gani.
TAHLISO ina makundi mawili;
1. kundi la wanaojihusisha na siasa za nchi na 2. kundi ambalo siasa mwiko kwenye TAHLISO ila ni maslahi ya wanafunzi tu.
Nitaanza na kundi la pili ambalo mimi nipo katika kundi hilo. kundi hili hatuna agenda yoyote inayohusu siasa za kinchi NGUVU na AKILI zetu tumezielekeza kwenye eneo moja tu nalo si jingine ila ni la KUDAI MASLAHI ya wanafunzi wote wa TAASISI ZA ELIMU YA JUU nchini na hatupo tayari kuona maslahi rasmi ya wanafunzi yanachezewa iwe na serikali kuu kwa ujumla au iwe wizara fulani au bodi fulani au mtu yeyote yule. kazi yetu ni moja tu na agenda yetu ni wanafunzi.
MSIMAMO WETU WA KUNDI LETU. Kama serikali itatimiza mambo ya wanafunzi ndani ya muda kama taratibu zinavyoelekeza basi wataifanya TAHLISO iwe kama haipo kwasababu hatutakuwa na la kutufanya tutoke tuseme au tuandamane n.k. njia nzuri na njema ya kudhibiti kundi hili, serikali ikikaa kupanga mipango yake basi wanafunzi vyuo vikuu wawe ni wa kwanza.
KUNDI LA PILI. hili ni kundi la WASAKA TONGE, walafi ambao wanafikiri maisha mazuri yanapatikana kwa njia ya kujipendekeza kwa wenye nacho na wenye vyeo. kundi hili halijawahi na halitakuja kuwahi hata mara moja kutoka mbele kusimamia maslahi ya wanafunzi. ukiwaona wametoka basi ujue kuna mgombea urais ameongezeka wamekuja kumuunga mkono, hiyo ndio kazi yao. kwahiyo kwa MUHUTASARI kundi hili ni kundi linalojihusisha na siasa. Ninalichukia sana hilo kundi na MwenyeeziMUNGU atalilaani kundi hilo baya tena wao pamoja na washirika wao.
MATATIZO VYUO VIKUU.
hatukatazwi kufanya siasa lakini kuitumia TAHLISO kama mwavuli ni Dhambi isiyosameheka, mafikirio na ajenda za kisiasa tukazifanye vyama vyetu vya siasa tukumbuke sisi kama wasomi hatupaswi kuwa na haraka ya maisha hii nchi ni ya kwetu baina yetu leo ndio kuna Rais wa mwaka 2030 tena huenda nikawa ni mimi au mwingine yoyote pia baina yetu ndio kuna usalama wa taifa, maaskari, wakurugenzi, wabunge mawaziri n.k. hakuna atakayekuja kushika nafasi hizo ila ni sisi vijana wenzangu wasomi tusitumike ila tufanye kama sisi tujisaidie sisi na Taifa letu kwa ujumla.