Yahya Jammeh ametangaza kuunda Serikali upya

Good People

JF-Expert Member
Aug 6, 2016
945
1,819
Ndugu Yahya Jammeh ambaye ni kiongozi wa waasi ameapa kuunda serikali yake upya baada ya baraza la mawaziri kupuputika kwa kujiuzulu.

Rais Barrow amewashukuru watu watu wa Gambia kwa kutimiza jukumu la Kidemokrasia

Jana ilikua ni Siku ya Kwanza taangu Mwaka 1994 Yahaya Jammeh kulala bila Cheo cha Urais. Kiongozi huyo wa waasi anatarajiwa kung'olewa Mchana wa Leo.
 
Kwani keshasema ni kiongozi wa waasi? Mbona hana anaowaongoza? Mkuu wa majeshi kasema hawezi kuuwa wanajeshi wake kwa sababu za kisiasa. Sasa kiongozi wa waasi gani huyo?
 
Urais mtamu jmn, naona jamaa anataka kufia madarakani
 
Swali la kujiuliza ni je hawa wanaoshadadia kumuondoa jammeh wanaipenda sana gambia au wanamaslahi yao ambayo jammeh aliyaburuza mkiani.
 
Ndugu Yahya Jammeh ambaye ni kiongozi wa waasi ameapa kuunda serikali yake upya baada ya baraza la mawaziri kupuputika kwa kujiuzulu.

Rais Barrow amewashukuru watu watu wa Gambia kwa kutimiza jukumu la Kidemokrasia

Jana ilikua ni Siku ya Kwanza taangu Mwaka 1994 Yahaya Jammeh kulala bila Cheo cha Urais. Kiongozi huyo wa waasi anatarajiwa kung'olewa Mchana wa Leo.
Nimeficha sana na kukaa na siri moyoni lakini leo nimeona bora niseme tu,
Ukweli kila nikisoma hizi habari za huyu Jammeh moja kwa moja mawazo yananipeleka pale ng'ambo kwa wenzetu na ndugu zetu wale walioko kule baharini upande wa Mashariki. Kila nikijaribu kukwepa hisia hizo za kina Mwalimu Seif zisinijie najikuta napata napata wakati gumu sana kuziondoa.

Yaani mtu akinitajia Adam Barrow tu basi Mwalim huyu hapa ananijia kwenye fikra, Na akitajwa Yya Jameh basi ananijia yule Jamaa aliekuwepo kabla nimejiuliza hata ni kwanini sijapata jibu aisee
 
Swali la kujiuliza ni je hawa wanaoshadadia kumuondoa jammeh wanaipenda sana gambia au wanamaslahi yao ambayo jammeh aliyaburuza mkiani.
Yaani ni sawa na wewe ulivyoshangalia Trump kushinda urais,transformation ni muhimu na kila MTU ni mzalendo kwa upande wake ,yaani nchi zote 13 ziwe na maslahi na taifa Dogo ilo mkuu kuqeni seriously
 
Swali la kujiuliza ni je hawa wanaoshadadia kumuondoa jammeh wanaipenda sana gambia au wanamaslahi yao ambayo jammeh aliyaburuza mkiani.

Jameh amefanya crimes nyingi gambia. Some utaona.

Hakuna wanaoshadadia kumwondoa Jameh. Huyu jamaa alishaondolewa na sanduku la kura. Yeye ndiye umwulize haya maswali.

Kwa nini anang'ang'ania madaraka wkati wananchi hawamtaki?
 
Swali la kujiuliza ni je hawa wanaoshadadia kumuondoa jammeh wanaipenda sana gambia au wanamaslahi yao ambayo jammeh aliyaburuza mkiani.
Jammeh ni mshenzi tu mpenda madaraka .ECOWAS hawana maslahi zaidi ya kumlazimisha Jammeh kukubali matokeo ambayo swali aliyakubali.
Alipewa nafasi ya kukubali akajifanya mjanja sasa mpaka mkewe kamgeuka.
 
Swali la kujiuliza ni je hawa wanaoshadadia kumuondoa jammeh wanaipenda sana gambia au wanamaslahi yao ambayo jammeh aliyaburuza mkiani.

Wanawapenda sana Wagambia.
Wanaheshimu sana maoni yao waliyoyatoa kwenye sanduku la Kura.
Wanawasaidia kumchomoa Joka lililojificha Ikulu.
 
Chonde Tanzania lazima kumpokea shujaa Jammeh. Anastahili tuzo . Kufuta uchaguzi siyo kazi ndogo.
 
Swali la kujiuliza ni je hawa wanaoshadadia kumuondoa jammeh wanaipenda sana gambia au wanamaslahi yao ambayo jammeh aliyaburuza mkiani.
Sio watu fulani bali ni katiba ndiyo inasema uchaguzi ukiitishwa mwenye kura nyingi ndiye rais, na ndicho kilitokea.
Jammeh angeacha mazingaombwe na kuitangaza Gambia nchi ya kifalme kama UK basi wala asingesumbuliwa lakini aliamua kutengeneza demokrasia bandia wenye akili zao wakaigeuza na matokeo yake yeye akabaki kuwa rais bandia!
 
Back
Top Bottom