Bususwa
JF-Expert Member
- Sep 30, 2021
- 429
- 1,011
Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pole na majukumu mazito ya ujenzi wa taifa letu! Mh Rais wetu kwanza nakupa hongera sana kwamba hua unapita pita hapa Jamii Forum kusoma maoni ya wananchi wako,yale mazuri hua unayafanyia kazi na mengine hua unayaboresha na huo ndiyo uongozi thabiti!
Mh Rais wetu mimi nikijana mdogo sana mwenye malengo makubwa mbele ya safari zangu za utafutaji wa maisha!
Mh Rais wetu, mwaka 2021 nilinunua kiwanja hapa Dodoma eneo la Nala Chihoni kwa hawa jamaa wanaoitwa Land Network, sababu ni kampuni kubwa niliwaamini sana, nililipa pesa bila ya kwenda kuangalia viwanja vikoje!
Kumbe vile viwanja kwanza havijafanyiwa usafi, ni kwamba hawa jamaa walinunua pori kubwa,wakaanza kulipima kwa kukata viwanja vipande vipande, lakini hawajafanya chochote hadi leo hii ukienda huko huwezi kukiona kiwanja chako zaidi yakuona pori tu
Mh Rais wetu, nikaenda ofisini kwao kuomba wanipeleke kwenye kiwanja changu, nilipofika nikakuta ni pori kweli unaweza kuta hata kuna Simba au tembo kabisa kwenye hilo pori, huo ni mwaka 2021 kipindi hicho nimemaliza kulipa gharama za kiwanja na mambo mengine, nikauliza mtakuja lini kufanya usafi yaani kufyeka hili pori ili niweze kukijua kiwanja changu?? Wakasema mitambo kama Motor Grader wameagiza kutoka Nje ya Tanzania,kwa hiyo ikifika tu watafanya usafi na mimi nitaonyweshwa kiwanja changu sehemu kilipo!
Mh Rais wetu tangu kipindi hicho cha mwaka 2021, mitambo imekuja mwaka 2022 mwishoni, nikaenda tena pale, nilikutana na wenzangu na wenyewe kero ni kama yangu, wamelipa pesa kwenye viwanja,lakini hadi leo hawajui hata viwanja vyao viko wapi! Mitambo yakufanya usafi imekuja lakini nasikia wanakodisha kwa wakandarasi wa ujenzi wa barabara na sisi hawaendi tena kufanyia kazi yetu
Mh Rais wetu kila mtu hua anamipango yake, toka 2021 hadi leo, kama ningekua najua kiwanja kiko wapi,ningekua nishaanza na ujenzi lakini hadi leo nipo nipo tu, hadi nawaza nijipange tu upya ninunue kiwanja kingine tu!
Mh Rais wetu hawa jamaa wamekua wahuni, na wanatoa majibu mepesi sana kwenye jambo la msingi!
Ombi langu kwako,kama utapita hapa au wasaidizi wako watapita hapa! Basi naomba Waziri wa Ardhi,Mkurugenzi wa Jiji Dodoma na Land Network wape amri ili waweze kulifanyia kazk ombi letu! Wanatukwamisha pakubwa sana hawa jamaa
Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app