Yah: Uyoga, Vipepeo na Midoli Bunge la Watanzania

Hivyo hata kama TBC watapata mtu ambae yupo makini na kutengeza chombo hicho cha "Bungeni Live" kiwe na mvuto hata kwa wale wanaokupa fedha za kujiendesha badala la kushughulika na Star Times kuuza vitu vingine kama simu, hio inakuwa huitaji bilioni 4 kuendesha live broadcasting..
Thank you!

1. Hakina watu makini kuanzia TBC hadi wizarani. Inapotokea mtu akadhani kurekodi kunapunguza gharama bila kujali nini kinaweza kupatikana kupitia njia nyingine , inafikirisha

2. Wameacha jukumu lao la asili na sasa wanatumika na CCM, ndio ukweli hata kama watu hawataki

3. Hawana ubunifu wa kuleta mvuto. Watu wanapotangaza harusi badala ya mambo yatakayovutia audience na kufanya biashara ni hali ya kusikitisha sana
 
mzee, tatizo ni kuwa vyombo vingine vya habari vinategemea 'feed' ya TBC ili warushe matangazo hayo. Hawana facilities zao wenyewe pale. Binafsi ningependa Bunge ndio liwe linatoa feed yake ili chombo chochote chenye uwezo wa kurusha live kinarusha na kama hakipo bado Bunge linarekodi kikao kizima "live" na vyombo vya habari vinaweza kuchukua na kuhariri kile wanachotaka kurusha.

Unajua kwa kadri ninavyozidi kulifikiria hili suala ndo ninavyozidi kushangaa kwa nini hata lipotezee watu muda.

Sasa labda ni mimi tu katika ujinga wangu ndo maana nashangaa.

Hapa nilipo najiuliza, hivi kuna hata mbunge mmoja huko nyuma aliyewahi kutoa hoja ya bunge kuwa na vyombo vyake vya habari/ mawasiliano?

Kama hakuna mbunge aliyewahi kuwasilisha hoja kuhusu hilo suala basi matatizo tuliyonayo ni makubwa mno pengine hata tunavyodhani.

Katika karne ya 21 suala kama hili kwenye taasisi muhimu kama bunge ni jambo ambalo halikupaswa kabisa kupotezea watu muda wao na kuleta vurugu bungeni.

Mimi naliona kama ni jambo ambalo lilipaswa kuwepo tokea mwanzo, hususan walipohamia kwenye huo mjengo mpya.

Walipaswa wawe na redio yao, runinga yao, tovuti yao ambayo pamoja na kuwa na taarifa za mambo mbalimbali ya bunge na wabunge ingekuwa pia inatoa live webcasts ya shughuli za bunge, ingependeza pia kama wangekuwa na YouTube channel yao, App yao ambayo watu wangeweza kui-download kwenye devices zao na kuweza kufuatilia mambo yanayojiri bungeni, na kadhalika.

Mimi wakati mwingine huwa nafuatilia sessions za Congress [chambers zote mbili] kwenye iPad nikiwa sipo nyumbani kuweza kuangalia C-SPAN.

Tukiachana na hayo makorokoro mengine ya kiteknolojia, kuendesha kituo cha runinga na redio ambacho kazi yake kuu ni kurusha matangazo ya shughuli za bunge, wala si gharama kubwa.

Na nasema hivyo nikiwa na ufahamu wa kiasi fulani juu ya nini kinachohitajika katika kufanikisha huo urushaji wa matangazo. Gharama zinaweza hata zisifikie hiyo bilioni 4 ya TBC.

Na kama nilivyosema hapo awali, hiyo bunge TV/ Radio inaweza hata kuchaji ada ndogo tu [itakayotumika kuchangia uendeshaji wake] kwa vyombo vya habari vitakavyotaka kurusha hizo shughuli za bunge.

Ambacho hata sielewi ni kwa nini taasisi kubwa na muhimu kama bunge haina hivyo vitu?
 
Cha msingi kuhoji hapo , Je ni kitu gani serikali inahofia kurusha matangazo ya bunge Live?

Hoja ya msingi siyo uLive au kutokuwepo uLive, Hoja ya msingi ukiingia deep ni the Motives behind this move ya serikali.

Motive ni ili wao kupata muda wa kuedit yale yote watawala wasiyoyataka, Ili wananchi tusipate taarifa sahihi!. This is the point Mr Mwanakijiji, mengine yote unayoyasema ni semantics
 
Nilitaka nifanye 'quote' kwa kupunguza mistari sikufanikiwa.
Kila mstari unajieleza kikamilifu. Ni hoja nzito zilizoshiba

Ukitembelea web ya bunge utashangaa na udhaifu utakaokutana, tume ya uchaguzi na vituko
Haya ni kwasababu ya kutotaka kutoa taarifa kikamilifu

Website ya tume ya Warioba ilifutwa haraka sana. Lengo likiwa kuzuia wananchi wasisome kilichomo

Bunge lhaliwezi kuwa na vyombo kwasababu litakuwa huru kujiendesha na udhibiti kutoka serikalini hautakuwepo. Hata kama wazo lipo ni wazi halifanyiwi kazi kwa hofu tu wananchi wataona madudu

Ni kasumba ya 'mazungumzo baada ya habari' Uhuru/Mzalendo na mkoa kwa mkoa

Yanayotokea ni matokeo ya nguvu mbili. Inayotaka habari wazi na inayohofia habari kuwekwa wazi

Live au recorded si tatizo kubwa, kinachosHtua ni jinsi suala linavyoendeshwa kiudanganyifu.
Bilioni 4 kweli! Leo wana uchungu na bilioni 4 wamesahau Bilioni Zaidi ya 100 za Bunge-katiba

Kuna kijana anaendesha webcast inayotoa matangazo live, bunge letu halina uwezo huo
Uwezo upo kinachohofiwa ni madudu, njia ya kuyaficha ni kutumia TBC na kulisha watu wanachotaka

Nipo against tabia ya kudanganya inayoonekana kufanikiwa sana. Tulidanganywa kuhusu sheria za mtandao kuwa ni za kulinda watu. Ukweli ni kuzuia mitandao kama hii kupashana habari. Walifanikiwa

Wanakwenda mbele baada ya vituko vya uchaguzi , umeme hakuna siku fulani, CCM wakiwa na shughuli umeme upo. Tbc ipo hewani CCM wakiwa na shughuli siku nyingine hakuna

Hakuna anayejua hujuma za mitandao wakati wa uchaguzi nani yupo nyuma yake.
Na wala serikali haikutumia sheria ya mitandao kubaini wahalifu. Serikali haikujua? Au kulikoni

Sasa wanataka ku 'insinuate' habari nyingine na kibaya ni kutumia chombo cha umma.

Wanataka watukaange kwa kodi zetu. Kwa bahati mbaya sana hatuelewi kwasababu tumelewa wimbo mtamu wa Hapakazi wakitugeuza mazezeta.
'
Hapana, Taifa letu ni bora Zaidi ya haya tunayoona.

Tukatae uhuni , ni afadhali watuambie ukweli hata kama hatukubaliani nao.

TBC iondolewe monopoly wamesema hawana uwezo, anayeweza kuweka mitambo aweke

Wanataka kuzuia uhuru wa habari kwa lengo moja , kuficha maovu wakitulaghai na majipu.
 
Itamsaidia nini mwananchi kuupokea mwenge wa uhuru, Itamsaidia nini mwananchi kutazama live wakati Rais wa nchi akiapishwa, Itamsaidia nini mwananchi kama wewe mwana kijiji kutazama mechi za ligi za ulaya live. Umejitetea na kujikanyaga. Kama ulivyoona kwa upande wako sio muhimu basi kumbuka kuna wenye kulichukulia hili jambo kwa umuhimu mkubwa. Tanzania ni yetu wote na maendeleo ya Mbeya ni manufaa ya wana Mtwara pia. Nitashangaa endapo atatokea mtu mwengine mwenye kuleta hoja za " Mbunge wa Lindi atakusaidia nini wewe Mwenyeji wa Kigoma. Na kusahau kwamba ndani ya Tanzania mtanzania unaweza kuhama na kuishi popote. Live itabaki kuwa live kwani ujumbe unaotolewa na mhusika unamfikia mpokeaji kama ulivyo moja kwa moja.
 
Live itabaki kuwa live kwani ujumbe unaotolewa na mhusika unamfikia mpokeaji kama ulivyo moja kwa moja.

This is just silly! kwani ili mtu upate ujumbe wa barua lazima umuone muandikaji wakati anaandika "live"?
 
Cha msingi kuhoji hapo , Je ni kitu gani serikali inahofia kurusha matangazo ya bunge Live?

Hoja ya msingi siyo uLive au kutokuwepo uLive, Hoja ya msingi ukiingia deep ni the Motives behind this move ya serikali.

Motive ni ili wao kupata muda wa kuedit yale yote watawala wasiyoyataka, Ili wananchi tusipate taarifa sahihi!. This is the point Mr Mwanakijiji, mengine yote unayoyasema ni semantics

Unajua wakati mwingine pia tuwe wakweli! Hivi waandishi wa habari wamekatazwa kuangalia Bunge live? Je, wageni wanakatazwa kuingia kuona Bunge linavyoendelea "live"? Hivi kweli kabisa tunaamini kwa vile tunaona habari "live" basi tunachoambiwa hakiwezi kuchakachuliwa? Kwa mfano wangesema "hakutaruhusiwa kuwepo waandishi wa habari" au "vyombo vya habari Bungeni" wakati Bunge linaendelea hata mimi ningeshtuka. Sasa tunataka tuaminishwe kuwa chombo pekee cha habari au waandishi wa habari wanaokuwepo Bungeni wakati Bunge linaendelea ni wa TBC peke yake. Hili ni kweli?

Au mnataka kusema kwa vile TBC haitaoonesha "live" basi waandishi wengine wa habari hawawezi kuripoti kilichotokea "live" Bungeni hata kama wataripoti baadaye. Si ndivyo habari nyingine nyingi tunazozipata na kuzikubali zinakuja hivi - kwamba waandishi wanaona live na baadaye wanatutumia ripoti. Sivyo?
 
huyu mzee na mzee mwenzie padri slaa tokea walambishwe hela za magamba na limbwata la kihaya wamekuwa kama mahayawani!we mzee usiyepiga hata kura hapa tanzania funga bakuli lako unatupigia kelele!hivi slaa bado analala sebleni kwako huko marekani?!!

uko sahihi sana kati ya watu ninaowadharau sana ni huyu mwanakijiji, evarist chahali na dr slaa. Wamekula fedha za watu sasa wanatafuta namna ya kulipa fadhila bila aibu
 
uko sahihi sana kati ya watu ninaowadharau sana ni huyu mwanakijiji, evarist chahali na dr slaa. Wamekula fedha za watu sasa wanatafuta namna ya kulipa fadhila bila aibu
Na hizi stori za kijiweni nazo zitafika mahali zitakwama tu; mmeingia mahaba ya mabadiliko feki kiasi kwamba hamtaki kuamini mmeuzwa wazima wazima. Kutoka hamtoki mmebakia kupinga tu mabadiliko ya kweli.
 
Duh! Haya bwana, yaani kila mwana CCM anatetea kufungiwa kwa Live stream, it means wana manufaa nayo.

Simple mathematics
 
TBccm leo imekua mali? Tumeaminishwa kwamba wenye akili waliacha kuangalia TV hii miaka mingi kumbe LAGHAI wakubwa. Aibu yao
 
Bungeni-Dodoma.jpg

Ugomvi wa Kifikra: Mojawapo ya upotoshaji mkubwa uliotokea ni kuwaaminisha watu kuwa ipo haki fulani inaitwa "ya kupata habari live". Kwamba, usipopata habari "live" basi haki yako hiyo imevunjwa. Haki hii haipo mahali popote duniani, na haijawahi kutambuliwa na serikali yoyote duniani! Hakuna haki ya kupata habari "live"!

Ipo haki ya kupata na kutoa habari. Haki hii ni miongoni mwa haki za msingi za binadamu. Haki hii imeanishwa katika Azimio la Wote la Umoja wa Mataifa juu ya Haki za Binadamu la 1948 (Kifungu cha 19) ambalo nchi nyingi duniani nazo zimeikubali.

Tanzania nayo inatambua haki hii na tumeiweka Katika Katiba yetu Ibara ya 18. Haki ya kupata habari ni haki ya msingi ya binadamu, kwamba huwezi kumnyima mtu habari. Ningekuwa miongoni mwa watu ambao wamekasirika na kuja kuu kama Serikali ya Magufuli ingedai au hata kupendekeza kuwa Watanzania wasiambiwe au wasisikie kinachotokea Bungeni. Ningeungana na wengine kupinga vikali endapo angesema kuwa Serikali imeamua kuwa kuanzia sasa habari za Bunge hazitawekwa wazi kwa wananchi. HIlo lingekuwa ni kuvunja Ibara ya 18 ya Katiba na kwenda kinyume na Azimio la Umoja wa Taifa la Haki za Binadamu ambayo Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoliridhia.

Kama Magufuli na Serikali yake wangekuja na pendekezo kama hilo nina uhakika kesi rahisi kabisa ya Kikatiba ingeweza kufunguliwa dhidi ya uamuzi huo na kwa asilimia 100 Serikali ingeshindwa.

Binafsi naamini ipo haki kubwa zaidi ambayo inatishia Watanzania kupata habari sahihi kutoka kwa wawakilishi wao Bungeni. Wabunge wamechaguliwa na wananchi kuwawakilisha Bungeni; nii ni pamoja na kushiriki mijadala, kutoa maoni, kusimamia serikali, lakini kubwa zaidi kutunga sheria na kubadilisha sheria mbalimbali. Mbunge ambaye haendi Bungeni, au ambaye anatoka Bungeni kwa sababu tu hajapenda uamuzi fulani wa Kiti cha Spika au kupinga maamuzi fulani ya kisiasa anawanyima wananchi waliomwakilisha kupata habari sahihi - kwani akija na kuulizwa kuhusu jambo ambalo yeye hakuwepo Bungeni hawezi kutoa habari sahihi na hivyo atakuwa anawanyima wananchi haki yao chini ya Ibara ya 18 ya Katiba na chini ya Azimio la UM la Haki za Binadamu.

Ndugu zangu, kama kuna sababu ya wabunge kulumbana na kucharuka ni kuhusiana na wao kutokuwepo “live” Bungeni wakati mijadala mbalimbali inafanyika na wao kutoa mawazo au kutoa hoja na kupendekeza Sheria au Mabadiliko ya Sheria mbalimbali Bungeni. Kuna faida gani kwa wananchi kuona kinachotokea Bungeni “live” kama wale waliowatuma huko Bungeni hawapo “Live”. Mwananchi wa jimbo fulani atafurahia nini kuona Bungeni kinachofanyika “live” wakati Mbunge wa jimbo lake hayupo “live” Bungeni?

Mwananchi ambaye anamuuliza Mbunge wake kuhusu suala fulani ambalo alitakiwa awe ametolea maoni nay eye hakuwepo “live” Bungeni atafaidika nini kuambiwa kuwa ameona jinsi watu walivyozungumza kwa ukali mambo ambayo yeye hayamgusi na mbunge wake hakuwepo Bungeni? Hili ndilo jambo hasa la kulizungumzia.

Binafsi, ningekuwa na uwezo nisingejali sana hili la kuona au kutoona “live”; ningejali zaidi kile kinachofanyika “live” Bungeni hata kama mimi mwenyewe sioni kwa macho! Kwa sababu macho siyo chombo cha kuaminiwa sana kwa kukupa taarifa sahihi; vinginevyo, mazingaombwe yangekuwa yanaamini ni ukweli. Kuona tu haitoshi; tunataka tujue nini kinafanywa na wabunge wetu Bungeni.

Lakini ningeenda mbali zaidi; na ninatumaini Serikali ya Mabadiliko ya J.P. Magufuli itakuja na mabadiliko ya sheria ambayo wabunge wote watafurahia ambayo yataweka adhabu kwa wabunge watoro Bungeni. Kama wafanyakazi wengine kwenye makampuni wanapewa kiasi tu (limited) cha siku ambazo anaweza kusema alikuwa mgonjwa wabunge nao wapewe siku (na zisizidi siku saba) kwa mwaka (ambapo kikao cha Bunge kinafanyika) ambapo ataweza kutoa udhuru kuwa hawezi kuwepo Bungeni. Isipokuwa kwa Mbunge ambaye yuko mahututi amelazwa au amepewa leave na Daktari kwa muda fulani. Wengine wote watatakiwa wawepo Bungeni au kwa kila siku, saa ambayo hawapo wakati vikao vya Bunge vinafanyika “live” watakatwa kwenye mishahara yao shilingi 50,000 kwa kila saa ambayo hawapo Bungeni au kwenye vikao ambavyo wanatakiwa wawepo. Hatutaki tuone Bunge “live” tunataka tujue wabunge wako “live” bungeni – mbele ya Luninga au hata nje ya luninga!

Nje ya hapo, ni lazima tukatae sanaa za maigizo ambazo zinajaribu kuwashikisha Watanzania wanasesere na kuwaambia waimbe “mtoto, mtoto!” na wengine kweli wanadakia “ni mtoto mtoto!” ati kwa vile mdoli huyo unafumba na kufumbua macho na unacheka kwa sauti zinazotokana na spika zinazoendeshwa na betri tumboni! Wakati wa kuwalazimisha Watanzania washike vipepeo na kuimba “uyoga uyoga” umepita! Tusiwafanye watu wetu waamini haki ambazo hazipo zipo na zile haki zenyewe za msingi wasijue kuwa zipo na wanatakiwa kuzidai!

Lakini kuna kubwa zaidi; kama kweli Wabunge wanataka kulazimisha kitu fulani kifanywe na chombo cha serikali ni wao wenye jukumu la kutunga sheria na kutenga fedha kwa chombo chochote cha serikali. Kama Nape ameona kuwa ni gharama kubwa kurusha vipindi “Live” badala ya kususa na kukasirika wabunge wanaweza hata kutoa hoja ya dharura ikajadiliwa Bungeni na kuamuliwa ili Serikali ipeleke fedha za ziada kwa TBC ili irushe Bunge live. Na hata Bunge likirushwa “live” masaa 24 – wabunge wawemo au viti tu vinavyozunguka zunguka – bado Watanzania watakuwa wanadai haki yao ya kuona wabunge wao wapo Bungeni “live” na wanashiriki ipasavyo kwenye mijadala muhimu na inayogusa maisha yao.

Mengine haya ni vipepeo na uyoga tu! Sidandii hata.

MMM
Pole sana mzee,ila ungejua tofauti iliyopo kati ya live na recorded usingeandika hayo maelezo mengi sana.Jiulize swali dogo tu,kwanini serikali haitaki kuonesha live mijadala? achana na sababu za Nape.Kuwa live kwa bunge nani ananufaika zaidi Kati ya ccm au upinzani mbele ya wananchi katika utatuzi wa matatizo yao?.Nakupa pole sana.
 
Sasa hizi ni hoja nyingine kabisa... kama suala ni kunufaika; utashangaa nani anaweza kunufaika. Hivi si Bunge limekuwa likionesha "live" miaka mitano iliyopita.. nani alinufaika zaidi?
 
Mkuu labda nikuulize, ni nchi gani duniani ambayo kikao cha Bunge kinaonyeshwa Live kwenye televisheni kwa zaidi ya nusu saa, achilia mbali masaa sita na wananchi wamekaa wanatazama?
House of Commons la Uingereza linaonyeshwa Live masaa yote. Wana Tv yao ya Bunge inaitwa(BBC Parliament TV) Vikao vyote vya Bunge vinaonyeshwa Live muda wote. Hiyo Stesheni ni Bunge tu 24/7.

Acha kudanganya Watu.

Mkuu labda nikuulize, ni nchi gani duniani ambayo kikao cha Bunge kinaonyeshwa Live kwenye televisheni kwa zaidi ya nusu saa, achilia mbali masaa sita na wananchi wamekaa wanatazama?
 
Uwa tunatune wakati was Bunge tu, na likiisha tunaondoa. Sasa kwa kuondoa live stream ndo TBC inakufa kabisa kama enzi za TVT

Kama ikifa hata mimi nitashukuru; na kama kwa kutorusha Bunge live TBC itakufa basi tuombee wasirushe kabisa kwa sababu ikifa labda tutapata akili ya kutafuta njia nyingine za uhakika zaidi za kupata taarifa live kutoka Bungeni.
 
Kuonesha bunge live kulikuwa kunasaidia sana usambazaji wa habari. Ilikuwa ni rahisi zaidi kwa habari za bunge (mbaya na nzuri) kusambaa mapema. Hata vyombo vingine vya habari pengine vilikuwa havina haja ya kwenda Dodoma au kuingia Bungeni ili kupata habari mbalimbali za Bunge letu na kuwasambazia wananchi au kufanya uchambuzi.Lakini lingine kubwa ni kuwa kuonesha live kunasaidia sana kuzuia upotoshaji/uchakachuaji (mzuri na mbaya) ambao ungeweza kufanywa na vyombo vya habari maana watu wengi wanakuwa wamejionea na kusikia wenyewe yaliyojiri bungeni.

Ukisema Bunge litarekodiwa na kuoneshwa jioni/usiku ni wazi haiwezekani bila ya kufanya editing (hasa kupunguza) maana bunge linaanza saa 3 asubuhi na mara nyingine linaisha saa tatu usiku (ukiacha muda mchache wa mapumziko)! Hiyo recorded version itaoneshwa usiku kucha? Kwa ajili ya nani na wengi wa walengwa wanakuwa wameshalala?
 
Na hizi stori za kijiweni nazo zitafika mahali zitakwama tu; mmeingia mahaba ya mabadiliko feki kiasi kwamba hamtaki kuamini mmeuzwa wazima wazima. Kutoka hamtoki mmebakia kupinga tu mabadiliko ya kweli.

Huna lolote acha kujipendekeza kwa CCM uliyoitukana kwa miaka zaidi ya 15 iliyopita, waongelea mabadiliko yapi akwa mfano? shame on you huna platform yeyote ya kusikilizwa labda ukaandike makala zako kwa gazeti la uhuru na jambo leo
 
Back
Top Bottom