YAH: Ukombozi wa Fikra Afrika (kitata)

Askarimtu

JF-Expert Member
Sep 7, 2019
277
185
Kwako Bwana/Bibi,

Husika na kichwa cha habari hapo juu! Mimi ni mtanzania wa kawaida sana niliyemaliza elimu yangu ya kunitosha tuu, ya kujua kusoma na kuandika.

Lengo la barua hii ni kutaka kukujulisha kuwa hapo zamani, Afrika ilikuwa na nchi kama Kaanani, Babiloni, Assyria, Sidoni, Tiro, Moabu, Ammoni, Edomu n.k
Lakini sasa ina nchi kama za (Kusini mwa jangwa la Sahara) na nyinginezo!!! Mjinga ni yule aliyesoma akaamua kusonya fysiuuuuu...!!!! Na mpumbavu ni yule aliyeona haimsaidii hata akijua au asipojua!!! Uzalendo unapatikana kwa kujua wewe ni nani, umetoka wapi na unaelekea wapi kwa lengo lipi na kwa faida ya nani!!! Sifa moja ya uzalendo ni kujua ukweli na kusimamia ukweli, ndio maana hata Biblia imesema mwenye upendo haogopi kufa!!! Ukiwa mzalendo una upendo!!! Japo upendo huanzia moyoni, kisha kwenye familia mpaka kitaifa... lakini wengi hawajui kupenda!! Wengi ni wazalendo lakini huishia kwenye ngazi za familia zao tu au koo zao...lakini hawafiki kwenye level za kijirani, kijiji hata kitaifa!!! Huwezi kukomboa fikra za watu bila kuwaonyesha uwezo wao kupitia historia yao, kukumbusha ukuu wao..kuwatetea bila maslahi binafsi bali ya kijumla.

Tufanye uchunguzi, elimu ya kisasa haijatusaidia sanaaa bali imetupumbaza sana ndio maana tunaona lakini hatutambui, tunasikia lakini hatuelewi! Kuna mtu akiambiwa kuwa mmea wa mzalia nyuma (phyllanthus) ni dawa ya homa ya ini atakataa na kusema ni ushamba, lakini babu zako walitumia na hawakufa kama ilivyo sasa na haikuwa uchawi bali ni kuchemsha tu majani na kunywa!!! Nikikwambia wewe mwanamke unayevaa uchi ndio unaosabibisha nguvu za kiume kuwa tatizo, utakataa pia!!! Nikikwambia usitafute Eden kule Iraq, ila njoo hapo Ngorongoro utakataa sana katakata!!! Utakubalije ukiambiwa katikati ya Jangwa la Kalahari kuna mji mkubwa sana chini ya mchanga?? Ni mji gani huo...?? Je, Capernaumu sio Cape Town?? Hujui kwa sababu huna evidence!!! Lake Tanganyika iliitwa Sea (bahari), hujui kwasababu HUJUI TU!!!

Unadhani waarabu walikuwa wajinga kuteka Kilwa?? Wareno walisema Sofala!!! Kwani vigezo walivyochorea mipaka ya nchi zetu ni vipi?
Jua vitu vingi kwanza, ndipo uje uweze kukomboa fikra ...uwe huru maana ukweli utakuweka huru, ukikuweka huru utakuwa mzalendo kwa watu wako, ukiwa mzalendo utakufa mapema ila utakufa kwa furaha tamuuu kabisa!!!

Kataa kupelekeshwa na stori za kigeni...!!!! Kinachouma ni kwamba, watu wabaya ndio waijuao siri, watu wazuri hawajui chochote na ndio ambao wako gizani.


Ni mimi ,

Muuza Sabuni za Kupikia.
 
Lengo la viongozi wetu ni kuwa elimu hii itupumbaze tuwe tunawasifu tuu kwa kila wanachokifanya. ukihoji wanazidi kutishia kuwa unahatarisha Amani. Kama ilivyokuwa wakati wa ukoloni ,dini zimekuwa vyombo vya kusadia serikali kutunyanyasa
 
Back
Top Bottom