YAH: Nyumbu - Mheshimiwa Pinda, huu sasa utani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

YAH: Nyumbu - Mheshimiwa Pinda, huu sasa utani!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Aug 12, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Aug 12, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  (Note: Kwa kweli nilitaka kuandika "huu sasa uhuni"!

  Kiwanda cha jeshi Nyumbu sasa kitaunda matrekta madogo
  Mwandishi Maalum, Kiteto

  WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amesema serikali imeamua Kiwanda cha Nyumbu cha Kibaha, mkoani Pwani, kianze kuunda matrekta madogo ya mkono, wakati maandalizi ya kukiwezesha kuyatengeneza hapa nchini, yakiendelea.

  Pinda amesema hatua hiyo inalenga katika kuyawezesha matrekta hayo kupatikana kwa wingi na kwa wakati mmoja, ili kufanikisha kaulimbiu ya 'Kilimo Kwanza'.

  Akizungumza na wananchi wa Kata ya Engusero, wilayani Kiteto juzi mara baada ya kuzindua ghala la mazao, waziri mkuu alisema serikali imeamua kuipa Nyumbu kazi hiyo, kwa sababu kimeonyesha uwezo wa kuifanya hivyo.

  Alisema tayari serikali imeshapata mkopo kutoka serikali ya India, ili kuiwezesha kiwanda hicho kufanya kazi hiyo na mafunzo kwa wafanyakazi.

  Akijibu maombi ya Mbunge wa Kiteto,Benedict Ole Nangoro, ambayo yaligusia tatizo la njaa, maji, umeme na minara ya simu, waziri mkuu alisema atawasiliana na Waziri wa Nishati na Madini, ili kujua hatua iliyofikiwa na mradi wa kuvuta umeme kutoka Olboloti unaofadhiliwa na MCC.

  Kwa mujibu wa Pinda, mratibu huo, umekwishatengewa fedha.
  "Kata hii ina wakazi zaidi ya 9,000, hiyo ni idadi tosha na kwa vile mna mazao ya kutosha ni dhahiri kuwa mtamudu gharama za kuweka umeme," alisema.

  Pia alitumia fursa hiyo kuwaeleza wananchi hao kuhusu Mfuko wa Kuendeleza Umeme Vijijini (REA), ambao kazi yake kubwa ni kutafuta mbinu mbadala za kufikisha umeme vijijini, kwa kutumia vyanzo vingine kama vile jua, upepo au kinyesi cha wanyama.

  Alisema yeye binafsi atasimamia ufuatiliaji wa minara ya simu ili awasaidie kuondoa adha ya kukosa mawasiliano.Kuhusu hifadhi ya mazao ghalani, Pinda alisema ataongea na viongozi wa Benki ya CRDB na wale wa Shirikisho la Vyama vidogo vya Ushirika (SCUULT) ambao wana uzoefu na uendeshaji wa AMCOS na SACCOS za mazao, ili wawasaidie wakazi hao kuziendesha vizuri zaidi.

  Maswali:
  a. Fedha za Meremeta/Buhemba zilienda wapi wakati tuliambiwa ni kwa ajili ya kusaidia kiwanda hicho cha Nyumbu?

  b. Kama kweli wana mpango wa kuiwezesha Nyumbu kwa nini zile fedha za EPA walizopeleka TIB zisingepelekwa huko Nyumbu?

  c. Kama kweli wao wanampango wa kuhakikisha Nyumbu inakuwa ni sehemu ya kuchochea haya maigizo ya "KILIMO KWANZA" (wazee kama mimi wanakumbuka "siasa ni kilimo", Azimio la Iringa, Kilimo uti wa mgongo, )kwanini wasitenge fedha za kutosha kwa hii bajeti yao iliyopita tu wiki chache zilizopita hadi waombe mkopo India?

  d. Kama kweli wanataka kuinua Nyumbu kwanini wasishirikiane na makampuni ya Kijapani au Kichina ili kutengeneza zana za kilimo hapo.. na kwanini wasiamue kufufua lile lijembe juu ya jengo pale Ubungo (UFI)? Sijui bado lipo?

  Hivi mtaanza kuwa serious lini?
   
  Last edited by a moderator: Aug 13, 2009
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Pinda hana majibu hadi arudi ofisini akaulize yeye anasema mambo kisiasa anafukia mashimo ili watu wajue CCM iko serius kaka .
   
 3. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  halafu finally maswali yanapokuwa magumu kwao wanatumika wakina TAMBWE-HIZA kucrush vitu ambavyo UNCRUSHABLE!.....................
   
 4. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hii nchi kweli inaongozwa na wenda wazimu..
   
 5. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  ................na asilimia kubwa ya wanaoongozwa huenda ni WENDAWAZIMU!
   
 6. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #6
  Aug 12, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Pinda is another useless git

  badala ya kutambia kwa nini Bandari ya Dar haifanyi kazi vilivyo anataka kuleta uhuni wa nyumbu

  Bandari na reli kama mbovu whats the point of hayo ma trekta ya Nyumbu?
   
 7. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #7
  Aug 12, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  mwalimu ndio alikuwa na vision ya vitu kama nyumbu,mzinga ,carmatec na taasisi nyingine za technolojia viwanda ....huyu anapiga siasa ...hali ya nyumbu tunaijuwa ...kuajiri wafanyakazi na kuwa retain kwenyewe wanashindwa tokana na ukata ..itakuwa hiyo....

  KILIMO KWANZA NI WIZI MTUPU!!!!......watuambie kilimo kwanza ....wametoa kwenye ilani gani???
   
 8. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #8
  Aug 12, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Top notch.
   
 9. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #9
  Aug 12, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nakumbuka alivyokuja UK alisema amejifunza mengi pale Durblin hivyo akirudi Tanzania ataenda kuboresha Bandali yetu pia. Watanzania waliokuwepo walikuwa wakimshangilia Yes we can. Msanii huyo nae
   
 10. H

  Hauxtable JF-Expert Member

  #10
  Aug 12, 2009
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 386
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Mkuu ni afadhali sasa hivi, kuna wakati hali ilikuwa mbaya kiasi kwamba walikuwa wanatengeneza Majiko/mashine za kufyatulia matofali ya udongo.
   

  Attached Files:

 11. T

  T_Tonga Member

  #11
  Aug 13, 2009
  Joined: Jul 24, 2007
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  si unajua tz inaongozwa na mfalme pweza na kundi lake la wajinga
   
 12. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #12
  Aug 13, 2009
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Yap Yap mkuu Tonga direct to the point!
   
 13. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #13
  Aug 13, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,844
  Likes Received: 1,110
  Trophy Points: 280
  wizi mtupu
   
 14. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #14
  Aug 13, 2009
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hizi kauli wanazoibuka nazo ni njia tu kuelekea 2010, wanatafuta njia ya kutolea hela kwa ajili ya kampeni chafu za uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani. Kinachowaumiza vichwa ni kuwa EPA ya iliyosaidia 2005 imebumburuka, walibuni Dirisha Dogo TIB lakini wamegundua kuwa macho ya wengi yako hapo, sasa wanakuja na wimbo wa Kilimo Kwanza, yote hii ni janja ya kuiba fedha za walipa kodi tu. Kauli hizi kwa nini hawakuanza nazo 2005 walipochaguliwa? Hiyo kampuni ya nyumbu imejiandaa vipi kufanya hiyo kazi ya kutengeneza matrekta kama sio baadae kuambiwa siri za jeshi kama Meremeta!
   
 15. B

  Bobby JF-Expert Member

  #15
  Aug 13, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,683
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Hili halina mjadala kwa kweli mimi sijuwi kitu gani kikubwa tulimkosea Mungu mpaka akaruhusu vichaa watuongoze. Kuna mjumbe mmoja Zanzibar aliomba kwamba huyu mzee akapimwe ubongo wake kama uko sawa. Mimi nadhani alikuwa na point kwa kweli akachekiwe huyu mzee si bure tena waende wote na boss wake maana wanayofanya I'm sure hata wale wagonjwa kule Mirembe wanawashangaa. Lakini kibaya zaidi wanadhani sisi wote ni wagonjwa kama wao otherwise wangeacha kutumia kodi zetu kutuambia pumba juu ya pumba.
   
 16. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #16
  Aug 13, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MKJJ,

  Wapo serious penye maslahi yao panapoguswa. Angalia akina Mama Kilango wakiguswa tu huko same, achilia mbali usimpe mkono wa asante kwenye kazi wanazaosimamia na mbali zaidi waalike kwako usiwape posho.
   
 17. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #17
  Aug 13, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  huyu pinda nae ni mtoto wa ''kufikia'' siku hizi sijui kawaje!
   
 18. Sura-ya-Kwanza

  Sura-ya-Kwanza JF-Expert Member

  #18
  Aug 13, 2009
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 561
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mh. Pinda hayaelewi haya ya maendeleo! Mwacheni kwenye deski lake na darubini achape kazi.

  Anawajibika.

  The buck stops with Mkuu, His SeXillency JK:D:D:eek:

  ...oops a typo
   
 19. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #19
  Aug 13, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Taffu,

  Hawa jamaa waacheni. Hayo ndiyo wanayoyaweza kwa sababu kwa kila kiongozi wa nchi hii kazi yake kubwa ni kuhakikisha CCM inabaki madarakani. Ndiyo maana hawaishi kueleta maagizo kwamba kila mfanyakazi wa serikali kuu, serikali za mtaa na mashirika ya umma aeleze ni kwa kiasi gani ametekeleza ilani ya CCM ya 2005, iwe ni ukweli au kwa kuigiza! Ili mradi wapate cha kusema ili wapete kura feki za maoni. Hawajuia hata kidogo wanachohitajika kufanya ili kutupeleka kwenye neema ambayo mwenyezi Mungu alishatupa siku nyingi. Wanabaki kuzunguka pale pala kwa sababu njia hawaijui. Watanzania wangewafanyia jambo jema kama wanegeweza kuwapatia likizo wakapumzike. Wamechoka sana hadi macho hayaoni, masikio hayasikii na pua hazinusi tena.
   
 20. K

  Kachero JF-Expert Member

  #20
  Aug 13, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizi kauli za kilimo kwanza na hii ya Waziri Mkuu ya Nyumbu zitawatokea puani kwa kuwa wanazitoa bila kuwa na uthibitisho wa kitafiti.Sina hakika kwamba utafiti umefanyika wa kutosha wa namna ya kukifanya Kilimo kiwe uti wa mgongo wa Taifa hili.

  Na kwa kuwa hakuna utafiti wa kutosha ni usanii mtupu ndio maana kila mwanasiasa anasimama na kusema cha kwake.Wakati Waziri Mkuu akisema kuhusiana na kutumia kampuni ya nyumbu kutengeneza matrekta, JK akiwa ziarani Ruvuma juzi alimuuliza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr.Ishengoma kuwa ni mkakati gani walionao kama mkoa kuhakikisha kuwa haya matrekta yanayonunuliwa kwa gharama kubwa na Serikali yanadumu na kufanyiwa matengenezo kila yanaopoharibika?

  Kwa bahati mbaya sana Mkuu wa Mkoa huyo hakuwa na jibu akabaki akimumunya maneno na kuamua kumtupia mpira Mkurugenzi wake wa Mkoa ambaye hata yeye alishikwa na kigugumizi.

  Sasa kama kweli Serikali inampango wa kutumia kampuni ya Nyumbu kwa nini Rais asiseme waziwazi juu ya mpango huo,kwa nini kuwe na kauli zinazotofautiana, je ina maana JK hajui maamuzi ya Serikali ni yapi au ni usanii mtupu unaoendelea.

  Hapa ndipo unapoona maswali ya Mzee MJJ yanaleta maana,na nafikiri serikali makini inapaswa itoe majibu sahihi ya maswahi aliyouliza MJJ.
   
Loading...