Ya zimbabwe - tutegemee hili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ya zimbabwe - tutegemee hili

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Wakwetu, Sep 16, 2008.

 1. W

  Wakwetu Senior Member

  #1
  Sep 16, 2008
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 157
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mchakato mzima wa uchaguzi wa Zimbabwe na kurudia kupiga kura ulimalizika kwa Rais Robert Mugabe kuibuka kidedea mara zote mbili. Kilichofuata ni malalamiko mengi sana juu ya vitendo vya wizi wa kura ambavyo hadi nchi ikawekewa vikwazo. Leo wamepaatana na kuungana na aliyekuwa anasema kura zake zimeibwa na sio akawa rais la hasha yupo chini ya rais.
  Hili lilianzia Kenya kama utani baadaye Kibaki akaungana na Raila na kumpa uwaziri, baadaye likafuata Zimbabwe mengi yakasemwa na viongozi (Marais) wetu kulaani wizi wa kura lakini cha ajabu kupongeze kuungana kwao. Hapa wanakubaliana na wizi wa kura. Kwa Tanzania 2010 ipo hapa karibu, Kesho 17/09/2008 J.K anaenda kushuhudia kuweka sahihi kwa Tsvangirai na Mugabe akiwa kama rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa AU. Tusitarajie tofauti na haya kwenye uchaguzi wake 2010 kwani hapo ni kubariki njia ya upatikanaji wa viongozo hao ndio anaendakuubariki.
  Kwa staili hii je MAFISADI WATAISHA????? Si watalindwa na mkuu wa kaya kwani hawa wanaoungana na kupewa uwaziri mkuu wapo chini yake???
  Hapa inabidi tuseme!!
   
 2. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2008
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,212
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  Tatizo la msingi Zimbabwe limebainika wakati Mugabe akitoa hotuba yake: Amesema "Afrika kuna tatizo la vyama vya upinzani kutaka kuwa vyama tawala".

  Moja: Mugabe anadhani chama chake (ZANU PF) bado ni chama tawala. Ukweli kwamba chama cha MDC ndicho chama kilicho na wabunge wengi zaidi hajautambua.

  Pili: Kwa nini iwe vibaya kwa vyama vya upinzani kutaka kuwa chama tawala? Kuna chama tawala cha kudumu?

  Tsvangirai kawaambia BBC he is watching his back. Yuko hatarini kweli kweli. Nimemwangalia Mugabe kwa karibu zamani nikiwa mwalimu wa Chuo Kikuu cha Zimbabwe. Ni mtu hatari sana. Inaaminika hata kina Tongogara ni yeye kawawahisha kwa Muumba wao.
   
 3. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wakwetu, mawazo yako ni mwanana kabisa.Wananchi tumeshatoa ushauri lakini hakuna anayetusikiliza.Ni ukweli kwamba Kikwete amekubaliana na uovu uliofanywa Kenya na Kibaki na sasa na Mugabe Zimbabwe.Lakini kwa vile wananchi wa Tanzania tumepigwa sindano ya ganzi,basi tusubiri mfalme wa anga(the abyss) achukue nchi.
   
Loading...