najiuliza hizi sattelite zote hapo hatuna hata moja?
najiuliza hizi sattelite zote hapo hatuna hata moja?
unajua kama kuna kitu kinachoniudhi TZ ni kwamba ni wachoyo sana yaani mtu anajua kuruka na ungo lakini ataruka nao usiku aje kwako kukufanya usilale vizuri asubuhi unamke umechoka ushindwe kwenda kujitafutia riziki.hahhahahahaha! halafu ile sayansi inatakiwa tuijue, maana nasikia wachawi husafiri kwa ungo na speed ya huo ungo ni 2000km/h
unajua nini mkuu! wachawi wana akili nyingi sana ila tatizo la wachawi wa tanzania ni wachoyo, halafu wanataka uchawi wao kuuendesha kwa kutumia viungo vya binadamu wenzao ila kiukweli tunapaswa tujue hiyo sayansi yao, mtu ndani ya dakika 1 yupo mwanza toka dar si mchezo, kinachonikera ni kule kutishana tu kuwa ooh ntakuua ntakuloga, badala ya kusema ntakujengea nyumba....unajua kama kuna kitu kinachoniudhi TZ ni kwamba ni wachoyo sana yaani mtu anajua kuruka na ungo lakini ataruka nao usiku aje kwako kukufanya usilale vizuri asubuhi unamke umechoka ushindwe kwenda kujitafutia riziki.
unajua hata wazungu ni wachawi sema sasa wanatumia uchawi wao vizuri yaani mzungu anaweza ruka na ungo akaja kwako usiku akapalilia bustani au anaruka na ungo anakuletea mawasiliano ya simu ndio unaona hata uko nagani kuna vitu wameziweka hata tunaweza kuandika huu ujumbe ujue unakufikia kuna mzungu mmoja anaruka na ungo kukuletea haya maandishi niliyoanika hapa nawewe ukiandika mwingie anaruka ananiletea.
kweli najitoa kwenye laana ya waafrika na kujiunganisha na mibaraka ya wazungu na kuanzia leo nami nitaruka na ungo wa kizungu na kuwaletea waafria wenzangu maendela mpaka uniite freemason
kwanza unaamini kuna uchawi au huamini?Kuona ndio mwanzo wa kuamini lisemwalo nyie hapo juu mmewahi kuona hizo nyungo zikisafiria angani au mnasimuliwa tu? Huo ni uzushi mtupu hakuna kitu kama hicho, ukiweza kunipa ushahidi usio na shaka labda nitaelewa mnachosema.
kwanza unaamini kuna uchawi au huamini?