Ya Ruto na Odinga Kuwagharimu Mbowe/Dr Slaa/Shibuda

Naona tunajaribu kufananisha vitu ambavyo havina hata chembe ya kufanana.
 

Nahisi kama unataka kutueleza kuwa katika siasa kuna siri nzito, Si kweli.Walichotofautiana na viongozi waCDM na Shibuda na kukataa kumsusa Kikwete wakati wabunge wa CDM walipotoka nje ya bunge. This is a very trivial matter ndio maana baadaye wote waliotoka nje ya bunge walienda Ikulu kwa Kikwete huyo huyo na baadaye wakamwagia sifa kemkem wakati wa uzinduzi wa barabara na miradi mingine ya maendeleo katika majimbo yao.

Ushauri wa mtoa mada ni muafaka sana.
 
Huko kanda ya Ziwa wameshasema asiposimama Zitto Chadema haipati kitu!

Nilikuwa Shinyanga juzi juzi naongea na wakereketwa wa Chadema mitaa ya majengo wamenipa hii habari.
 
Lakini swali langu linabaki pale pale: je, Shibuda anaweza kuvutia kura zote za Wasukuma ambao ni karibu 25% ya Watanzania? Jibu ni hapana. Kwa sababu Tanzania hatuchagui viongozi kufuatana na dini zao.

Umechanganya habari ya dini na kabila.
 
Sabau hatokei kaskazini ndio maana wanamtenga na pia wanahisi mbio za urais atawapita

----!!! Umetimiza wajibu wako kwa leo, wahi Lumumba ukavute mkwanja!!!!!

Tiba
 
Huko kanda ya Ziwa wameshasema asiposimama Zitto Chadema haipati kitu!

Nilikuwa Shinyanga juzi juzi naongea na wakereketwa wa Chadema mitaa ya majengo wamenipa hii habari.

Mkuu tumuombe mwenyezi Mungu muumba Mbingu na Nchi atupe uhai kwa ujumla wetu tushuhudie uchaguzi mkuu unao tarajiwa kufanyika nchini mwaka 2015.

Huwa napata taabu sana, je masalia mtachangia nini hapa JF mara tu baada ya uchaguzi wa 2015?
 
Hakuna chama kisicho na mamluki na dawa ya mamluki si kimfukuza na kulumbana nae bali kumnyima tu information muhimu za chama

Na ndiyo sababu ya Shibuda kulalamika kutengwa.Na hapohapo unashauri apewe uwaziri kivuli.Nikuulize bado huna uhakika kuwa Shibuda ni pandikizi na ana mkono wake mkubwa tu hata kwenye sakata la hawa watoto wanaopiga kelele kila siku gazeti la mtanzania?
 
 
Umechanganya habari ya dini na kabila.

Hivi hizi statistics za idadi ya makabila watu uwaga wanazitoa wapi? au sielewe wanakuwa wanamaanisha nini?, manake sijawahi kusikia watu wa kihesabiwa kwa makabila yao.
 
Hivi hizi statistics za idadi ya makabila watu uwaga wanazitoa wapi? au sielewe wanakuwa wanamaanisha nini?, manake sijawahi kusikia watu wa kihesabiwa kwa makabila yao.
Hizo statistics mbona zipo tangu enzi za ukoloni?
 
Japo mimi simpendi Shibuda ila analysis ya mtoa uzi naikubali. Huwezi ukatupa wavu baharini na ukavua samaki tu, never, lazima uvue na makokolo. Sasa Shibuda ni kokolo la lazima kwa idadi ya samaki tunaotakiwa kuwavua ndani ya usiku mmoja.
 

Moi ni kwasababu alikuwa Makamu wa RAIS... haukumbuki JINSI JOMO KENYATTA alivyosafirishwa Usiku usiku kufia MOMBASA, MOI alikuwa hakui isipokuwa Wakikuyu kina SAITOTI na JAJI MKUU walikuwa upande wake... Walikuwa hawamtaki CHARLES NJONJO awe Rais wa KENYA... ndipo hapo MOI akasalimika lakini angalia Makamu wake wote ni Wakikuyu na alimpa kanu UHURU KENYATTA... ndio yeye aliyemuingiza kwenye SIASA akiwa na Miaka 32... PAY BACK is HEALTHY eh!!!
 
Ni bora kuzikosa kura za mtu huyu kwani ni msaliti.Cdm songa mbele usirudi nyuma.
 
Japo mimi simpendi Shibuda ila analysis ya mtoa uzi naikubali. Huwezi ukatupa wavu baharini na ukavua samaki tu, never, lazima uvue na makokolo. Sasa Shibuda ni kokolo la lazima kwa idadi ya samaki tunaotakiwa kuwavua ndani ya usiku mmoja.
Yeah,hata ukiangalia USA, POWEL ALIMUUNGA MKONO OBOMA REP HAWAKUMKEMEA. TUKUBALI WATU KAMA SHIBUDA WAPO TUWAVUMILIE
 

hapo red panaonesha jinsi ulivyo popo, kimsingi uko too low, hakuna namna ambapo siasa za kenya zinaendana na za bongo, kenya ni ukabila na umaskini wa kutupwa wa watu wa kawaida
 
Shibuda haaminiki na anafahamu hilo . Ukiona kansa mkononi dawa ni kukata mkono mapema ukifikiria faida ya mkono baadaye utajuta kansa itakapoenea . Shibuda ni mjanja lakini cdm ni wajanja zaidi ndo maana hawana haraka na shibuda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…