Ya Ombeni Sefue kumkuta Kinana?!

Ya Ombeni Sefue kumkuta Kinana?!

BEHOLD

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2013
Posts
5,056
Reaction score
10,729
Kwa silka na hulka ya utendaji wa Mwenyekiti mpya wa CCM, Dkt Magufuli, na hasa kwa kutowakubali, (yawezekana kwa kutowaamini), wateule na watendaji wakuu wa Mtangulizi wake, sioni dalili za Uteuzi wa Ndg Kinana kuwa Katibu Mkuu Mpya wa CCM, kudumu kwa muda hata wa siku 100.

Licha ya sifa kemkem alizopewa Dodoma, kuna uwezekano mkubwa yale yaliyomkuta aliyekuwa katibu mkuu kiongozi Ndg Sefuwe, yakamkuta Kinana, tukaishia kuambiwa, "ATAPANGIWA KAZI NYINGINE"

Muda haudaganyi Tusubiri.
 
Kinana ataendelea sana kudumu hadi 2017. Ila wasaidizi wake akina Nape, Luhwavi, Asha Rose na Zakhia Meghji hawana muda kwenye sekretarieti mpya
 
Huyu jamaa bana yaani hujui kazi ya kinana ndani ya chama nje ya chama ndani ya umma nje ya nchi?, hujui hata mambo ya mbuga za wanyama
 
KINANA! MTU WA KAZI NA ANAIWEZA SPEED YA MSUKUMA! ALIASHIRIA TANGU 2015 MWANZONI KUWA NI MWANAMABADILIKO, SINA HOFU JUU YA KINANA! ILA WENZIO. WATATAFUTIWA KAZI INGINE!
 
Mungu akikujaalia maarifa ni rahisi saana kukaa na mazuzu-Rais ana PHd ya kusotea
 
Muda ni mwalimu mzuri wa kujifunza. Tusubiri nini kitakachojiri wakati utakapowadia.
 
Mleta uzi mimi pia niliwaza kama wewe, Magu siyo mtu wa kuamini sana. Nadhani kuna uzoefu kidogo anahitaji toka kwa Kinana then amteme
 
Kinana ni kama Yohana mbatizaji,alitengeneza mapito ya Jamaa.
 
kwa speed ya magu,akimtema kinana;ccm itakumbana na dhoroba kubwa sana 2020! kinana ni dk.slaa wa CCM,chadema chali kifo cha mende baada ya kumtema slaa.
 
Kwa silka na hulka ya utendaji wa Mwenyekiti mpya wa CCM, Dkt Magufuli, na hasa kwa kutowakubali, (yawezekana kwa kutowaamini), wateule na watendaji wakuu wa Mtangulizi wake, sioni dalili za Uteuzi wa Ndg Kinana kuwa Katibu Mkuu Mpya wa CCM, kudumu kwa muda hata wa siku 100.

Licha ya sifa kemkem alizopewa Dodoma, kuna uwezekano mkubwa yale yaliyomkuta aliyekuwa katibu mkuu kiongozi Ndg Sefuwe, yakamkuta Kinana, tukaishia kuambiwa, "ATAPANGIWA KAZI NYINGINE"

Muda haudaganyi Tusubiri.
Na mimi niliwaza hivyo hivyo
 
By the way huwezi kumlinganisha Ombeni na Kinana. Kinana ni namba nyingine
Jembe sana huyu mtu..sina shaka akitoka hapo atakwenda TANAPA ili tupae na UJANGILI utakoma kabisa!
 
Nape yupo saana tu.Kazi aliyoifanya wakati ule wa kampeni ilikuwa kubwa sana.
 
Nape yupo saana tu.Kazi aliyoifanya wakati ule wa kampeni ilikuwa kubwa sana.
 
jana kikwete alimwambia magufuli "ukipata watendaji wazuri katka chama, utafanya kazi zako kwa raha mustarehe, kwa maana ww utakuwa unadeal na upande wa serikali tu huku chama kinaendelea vizuri bila shida yoyote" kinana ni katbu mkuu bora kabisa kuwahi kutokea katka vyama vyote vya siasa hapa tz, tena ninamshauri magufuli ambakize na mzee mangula katka nafasi yake maana ngoma ya mangula nayo si yakitoto.
 
Back
Top Bottom