Ya Mbwana Samatta yatufunze

FATHER OF REALITY

Senior Member
Nov 3, 2014
123
100
Kwa kifupi ninaungana na Watanzania au Manaafrika Mashariki wengi wanaompongeza mcheza kandanda Mbwana Samatta kwa mafanikio aliyoyafikia na kumuombea apate zaidi ya hayo.

Langu kubwa ni hili; Watanzania au kwa upana Wanafrika Mashariki ni kama watu wengine duniani au kama Waafrika wengine kama Wanigeria, Wakameruni au hata Waghana wenye mafanikio makubwa katika medani ya soka. Hivyo tuanzishe moyo wa kujituma kwa dhati ili kufanikiwa zaidi yani wanakandanda wawaze nje ya Simba, Yanga, Sports Villa, URA, Express, Ghormahia, Fc Leopards, Sofapaka, MPRA nk. Hii yote nahimiza kwa sababu wanaocheza TP Mazembe au Barcelona au Man U nk, ni kama wachezaji wetu, tofauti ni kujitambua na kuwa na malengo binafsi yenye chachu ya mafanikio makubwa katika soka na si kama ilivyo sasa mchezaji wa Afrika Mashariki ambao wakipata uwezo wa kubadilisha mboga basi wamemaliza, na hasa wakifikia kiwango cha kucheza vilabu vyetu viitwavyo vilabu vikubwa Afrika Mashariki basi wamefika mbingu ya kandanda.

Najua twaweza jitetea na mambo mengi sana kama vile umaskini, elimu ndogo, viwanja vibovu, kukosekana dhamilra ya dhati ya serikali zetu katika kuinua michezo, ujinga tuu wa mtu mmojammoja na mengine mwengi. Kuna ukweli kiasi kikubwa tuu, lakini niulizev swali hili , sasa tufanyeje, vipaji vife kwa sababu ya hayo, mbona tumeweza kupambana mpaka tukaweza kuchezea timu zetu kubwa, hayo je hayakuwa vikwazo, ahaaa, kumbe tatizo ni kubweteka baada ya kupata maendeleo kidogo, daaa, watz, mmmh wakipata kahela ka kununua satarlet na bia mbili tatu, basi habari yote kwisha kabisa matajiri wao.

Binafsi ni mwanasports, hasa football, sijui niwaambie vp wachezaji wetu ili waelewe, tafadhali mnaosoma habari hii hebu kawapeni habari hii. Kwanza watambue hali za kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiutendeji katika nchi za Afrika zinafanana mno, na kwa nyongeza nchi za Amerika ya Kusini bara lenye magwiji wa soka. Kwa Afrika ni tofauti kidogo na mataifa mengine, huku kwetu mafanikio ya mtu ndio yanachochea juhudi za serikali zetu na si serikali kuchochea mafanikio ya wanamichezo.

Maana yake ni nini, yaani lazima wachezaji wetu wajitume katika hali hii hii mbovu ili walete chachu kwa serikali kuanza mikakati baada ya kuona wachezaji wa Afrika Mashariki wanarudi na tuzo mbalimbali za mkafanikio ya kisoka.

lingine la kuwashirikisha wachezaji wetu huko mitaani, ni kwamba, kama nilivosema mwaqnzo mi ni mwanamichezo, hasa soka, hivyo nimefuatilia historia mbalimbali za magwiji wa soka, daaa, aisee wengi wametoka katika umasikini wa ajabu, kwa mfano, Ronaldo De Lima mama yake hakuwa hata na uwezo wa kumnunulia viatu vya kuchezea soka, ilibidi afanye kazi hotelini kwa muda mrefu akitafuta pesa hiyo, maana baba Ronaldo aliiterekeza familia yake.
Ronaldinho alikulia katika umaskini, na familia yao ilikuwa ikimtegemea kaka yake ambaye alikuwa na kipaji cha mpira blakini kutokana na majukumu ya kuitegemeza familia kwa ukaribu na hasa kusubiri kidogo wadogo zake wakue kue ilikosa nafasi kucheza soka ulaya vilabu vilipomuhitaji, baadaye dunia ikashuhudia ufalme wa Ronadinho Gaucho.
Wachezaji kama Denilson, yeye alikuwa anakosa hata nauli ya kwenda mazoezini, angesema umasikini ni kikwazo tusingemjua, alikuwa akiwalilia makondakta ili kumpa lifti kila siku, masikini engine, George weah, aliishi katika nyumba iliyozungukwa na uchafu mwingi na ni miongoni mwa familia zilizokuwa na njaa na kipindupindu kila wakati, aliishi na shangazi yake, shaababani nonda papii, rivaldo, etoo, Arantes Nasimento (PELE WA BRAZIL), Gilbeto silva yeye alikuwa muuza machungwa, Child Boy, na wengine wengi.

Rai yangu, si upande wa mpira tuu au michezop peke yake, Samatta na Oligi wa nchini Kenya, Asha Rose Migiro, Profesa Boaz mwalimu chuo kikuu marekani zaidi ya miaka 25 mtz au Obama rais wa marekani, na wasanii kama Bob Marley toka jamika katikati ya umasikini na yeye akiwa maqsikini, wawe chachu juu ya Wanaafrika Mashariki, Wanadunia ya tatu kama tuitwavyo au ngozi hii nyeusi kwamba tunaweza sawasawa na wengine, tujitahidi, katika michezo, elimu na ugunduzi, uongozi, muziki n.k.
nawasilisha.
 
Cha msingi huyu dogo asijihusishe kabisa na mademu hawa vinuka mkojo wa kibongo muvi.....asije kujidanganya kupenda bongo kwani hapa bongo hakuna mapenzi ila bongo muvi tu mtindo mmoja. Akiendekeza tu mademu basi atakuwa amekwisha na kubakia kama kale kajamaa Hasheem Thabeet. Kalikuwa kanachezea mademu wa bongo muvi na kujifanya hajuwi kiswahili wakati mtoto wa porini tu, ulizeni kaishia wapi.
 
Back
Top Bottom