Mkuu wangu nakubaliana na wewe 100% na kama ulinisoma vizuri nilisema pia kwamba yule kijana ni Victim wa system ya maisha tunayoishi na hata wale wajinga walokwenda kuchoma makanisa ni matokeo ya sisi wenyewe tulowafunda na kuujenga uhasama huo. Hawa ni watu wanaosubiri tu cheche ziwashwe halafu wafanyize maana maisha tayari yameisha washinda. Tumeshindwa kuwapa elimu bora tumeshindwa kuwapa mtaji wa maisha hivyo watu kama hawa hukimbilia last option ya kimaisha - IMANI ya dini na ndio mwokozi wao wa MAISHA na sio kiroho alobakia..Mkandara, Jasusi, maggid,
..sasa nikirudi kwenye hii mada husika, naomba nigusie hoja moja ambayo uliitoa.
..nakumbuka ulisema kwamba kijana wa miaka 14 au 16 anajua nini anafanya.
..mimi nakubaliana na hoja yako, lakini nadhani pia vijana wa umri huo mara nyingi hawana busara ya kujua madhara ya kitu wanachofanya.
..kwa uelewa wangu ktk umri huo vijana huwa very defiant, na watu wa kupenda kujiona wamekuwa, na hupenda kujaribu vitu mbalimbali.
..nikikumbuka ni katika umri huohuo ambapo vijana huanza mambo kama uvutaji sigara[kubwa na ndogo], hujaribu pombe, wasichana, na kwenye nchi za wenzetu ndiyo unakuta mambo kama gangs, guns, etc etc.
..kwa maoni yangu huu mgogoro ulipaswa kushughulikiwa kwa mtizamo huo. kwamba hawa ni vijana wawili vichwa maji waliokuwa ktk mabishano.
..pia tunapaswa kuhoji wazazi wa vijana wote wawili walishughulikia tatizo hili namna gani. kwanza ni huyo aliyefanya kosa kubwa na kukojolea msahafu. pili ni aliyefanya kosa dogo kwa kuchukua msahafu na kuutumia ktk mabishano yasiyofaa.
..mwisho, mabishano ya hao mabwana wadogo ni reflection ya mambo tunayoyafanya watu wazima siku hizi. wakati mimi na wewe tunakuwa sidhani kama mabishano ya Uislamu vs Ukristo yangeweza kutokea.
Mkuu Joka kuu, unajua kujenga hoja kwa kulazimisha na si mantiki huzua maswali magumu kujibika. Kwa hili nitakwambia wazi kuwa hutasikia Kawawa akitajwa popote katika historia ya Mohamed Said. Niliwahi kumuuliza na jibu ni kuwa 'huyo tumwache kwanza'. Kwahiyo Mwinyi na JK hutawasikia sana kwasababu hoja za wale wanaolazimisha haziruhusu kutwajwa kwao ili zisimame 'katika ukweli'.Mkandara, Jasusi, Nguruvi3,
..but can u tell me kwanini Raisi Alhaj Alli Mwinyi hatajwi kabisa kwenye hili suala la MOU? Badala yake anayetajwa ni Lowassa kana kwamba he was some rogue Minister acting on his own??
..mwisho, kwanini mpaka leo basi hatumjui waziri aliyehusika na suala la utaifishaji wa shule na hospitali wakati wa utawala wa Raisi Nyerere. Mimi ningependa kumjua Waziri huyo ili tumpe sifa au lawama zake.
Mkuu Joka kuu, unajua kujenga hoja kwa kulazimisha na si mantiki huzua maswali magumu kujibika. Kwa hili nitakwambia wazi kuwa hutasikia Kawawa akitajwa popote katika historia ya Mohamed Said. Niliwahi kumuuliza na jibu ni kuwa 'huyo tumwache kwanza'. Kwahiyo Mwinyi na JK hutawasikia sana kwasababu hoja za wale wanaolazimisha haziruhusu kutwajwa kwao ili zisimame 'katika ukweli'.
Mfano wa pili, utasikia kadhia ya mabucha ikimhusisha Mwinyi kwa neno serikali hata Mohamed Said ndivyo alivyoandika. Maana nzima si kusema ukweli kama ulivyo ni kuunga unga habari ili zi-fit hoja tarajiwa.
Miezi michache iliyopita Kadhi wa Yemeni alikamatwa na Polisi Bagamoyo. Mada nzima juu ya kadhia ni kuhusu Polisi na serikali, cha ajabu, kwa upuuzi wa Mohamed Said Nyerere alishirikishwa! Ilitungwa hadithi ili kumtaja Nyerere.
Miaka 14 tangu afariki na 25 tangu aondoke madarakani, bado kunwa watu ambao akili zao zinawatuma Nyerere anafanya kazi kutokea kaburini Mwitongo.
Tulipomuuliza Mohamed Said kwanini Nyerere na si JK, alikimbia hakurudi tena. Anajua kuwa ni uchochezi tu uliotamalaki katika nafsi yake, kiu ya vurugu na umwagaikaji wa damu ili apate kuuza vitabu.
Ukisikia mtu anajenga hoja na kuhusisha vitu vingine maana yake ni kuwa hoja yake haisimami yenyewe hadi iwekewe uzio wa mabua.
Mwinyi hawezi kukwepa lawama za MoU na hapo ndipo wanaodhani ni kitu kibaya walipaswa waanzie.
Mwinyi alikuwa Rais aliyeunda serikali kwahiyo dhamana ya kila jambo ipo mikononi mwake.
Alijua hilo na hakufanya kitu! Kwahiyo kumsota kidole Lowasa ni yale yale ya kutafuta mahali laini pa kupiga na kukwepa ukweli.
Kuhusu waziri aliyehusika katika utaifishaji wa shule, hilo hutaweza kuambiwa. Sababu kubwa ni kuwa waziri husika alifanya kazi chini ya Waziri mkuu Marehemu Kawawa. Hapo utagusa ukweli ambao usiowalazima.
Mkuu Mkandara,
Labda nikuulize kuwa kwanini sheria nyingi duniani zinawalinda watoto 1-14 hata wanapokuwa na makosa?
Pili,Endapo kitabu kitakatifu cha Korani kingenajisiwa(hilo lisitokee, huu ni mfano tu) na mtu aliyeitwa Mchamboa Semangube Zomboka, unadhani busara ipi ingetumika kufikia suluhisho? Naomba busara zako as always
Tatu,je, kuchoma nyumba za ibada kunaweza kutoa suluhu ya kudumu ya tatizo, na je ni njia muafaka kwa busara za kidini na kidunia.
Hii nimeipenda sana kwa nini ufundishe neno la mungu kwa kudanganya?inakuwaje watu wa mungu wanakuwa waongo,huko si kumtendea dhambi Mungu,dini ifundishwe kwa kuelewa na sio kwa kutishia kuwa eti ukifanya hivi ,kutatiokea mlima wa moto,hayo mambo ndio yanatupa shaka ya hao wanaojiita waalimu wa dini kama kweli wanaelewa wanachokifanya au ndio kufanya kwa mazoea,kwa ufundishaji huu si ajabu Al Shaababu inapata vijana wengi kwa kudanganya kuwa wataenda peponi kwa kujilipua ,naamini yyule kijana angefundishwa kuwa kile ni kitabu kitakatifu tu na kiheshimiwe asingemtisha mwenzake kuwa atageuka nyoka.na mimi nashauri tuwalee watoto wetu kwa kuwaambia ukweli,waislamu kwa wakristo.
watoto wa siku hizi ni wadadisi na akili zao hazikubaliani na vitu vya kufikirika.
ukimwambia mtoto kuwa mtoto ananunuliwa hospitalini ujue akili yake haitatulia mpaka amedhibitisha.
ukimwambia ukichana biblia utakuwa wa bluu na kwa sababu hajawahi kusikia wala kuona mtu wa bluu atajaribu.
TUWE MAKINI NA WATOTO.
Kwa hiyo dawa ni kwenda mitaani na kuchoma makanisa sio,na je wakristo nao wachome misikiti pale wanapoambiwa Yesu si mwana wa Mungu,ugomvi wa watoto unaingiaje kwa waislamu wote ,mbona tumeona mengi wanayofanya waislamu dhidi ya wakiristo na hatujaona wakiristo wakiingia mitaani na kufanya vurugu?dini yenye vurugu si dini bali ni kufuru kwa Mungu!shauri yenu mnaoshabikia ujinga siku ya siku kutakuwa hakuna cha mwislamu wala mkiristo vita haichagui diniMtoi na kundi lako, nadhani umemezeshwa propaganda zinazoenezwa na maadui juu ya lile tukio. Waislamu si wajinga kama mnavyotaka watu wafikri. Issue ni kuwa baada ya mama mmoja wa kiislamu kuripoti hii habari ya kokojelea masahafu kwa mama wa ' bedui'. Yule mama alijibu kwa jeuri 'si makaratasi tu hayo'
Hiki ndicho chanzo cha kadhia nzima ambacho watu hawataki kukizungumza badala yake wanalilia guitar na 'whisky' zilizomwagwa altereni!
Dharau za hawa ndugu zako hazivumiliki, hata humu JF unaona mwenyewe, wako hivyo!
Endelea nao, lakini ufahamu walivyo!
Wewe nawe ndio kweli endeleeni kushabikia huu upuuzi. watakaoumia ni watu wa dini zote atakuwepo mama yako dada yako shangazi yako mjomba wako etc. sisi sote ni ndugu nani alikuja akasema dini fulani ndio ya kweli..UPENDO ndio dini za madhehebu yote..wewe unashabikia kama vile si Mtanzania angalia Middle East kinachowakuta kwa nini tunashindwa kujifunza na hii mifano. Ndugu zetu waislamu msidanganyike.Mtoi na kundi lako, nadhani umemezeshwa propaganda zinazoenezwa na maadui juu ya lile tukio. Waislamu si wajinga kama mnavyotaka watu wafikri. Issue ni kuwa baada ya mama mmoja wa kiislamu kuripoti hii habari ya kokojelea masahafu kwa mama wa ' bedui'. Yule mama alijibu kwa jeuri 'si makaratasi tu hayo'
Hiki ndicho chanzo cha kadhia nzima ambacho watu hawataki kukizungumza badala yake wanalilia guitar na 'whisky' zilizomwagwa altereni!
Dharau za hawa ndugu zako hazivumiliki, hata humu JF unaona mwenyewe, wako hivyo!
Endelea nao, lakini ufahamu walivyo!
Ningependa nikusahihishe kama ifuatavyo;
*Kijana aliyekojolea Quran tukufu inaelezwa alikuwa ana umri wa miaka 12 kwa mujibu wa report ya polisi, vyombo vya habari na mahakama.
*Hakuna mahali popote kwenye uislam panapofundisha kuwa mtu akiidhalilisha Quran tukufu atageuka mnyama, kufa au kuwa kichaa.(Yule mtoto wa kiislam alikuwa anapotosha na kusema uongo kwa kumuhusisha Mwenyezi Mungu na jambo ambalo Mwenyezi Mungu hajalisema, kiislam huu ni sawa na ushirikina)
*Uislam haufundishi watu kufanya mizaha, kuthubutisha au kufanya majaribio kwenye Quran tukufu.
(Yule mtoto wa kiislam alipaswa kuadhibiwa kisawasawa na waislam kwani tunaamini anayajua hayo na alipaswa kuepusha yasitokee, na yule kijana wa kikristo alipaswa kufundishwa na kuonywa maana tunajua hajui nini maana ya Quran tukufu na mafundisho ya uislam kwa usahihi wake)
*Si sahihi kabisa kabisa kwa waislam kutaka kuamsha ghasia siku za leo kupitia matukio yoyote kwa kisa cha kudai waliwahi kuonewa siku za nyuma.(Kufanya hivyo hakuwezi hata sikumoja kuujenga uislam wa kweli, zaidi kutaleta uadui mkubwa na visasi)
MY TAKE
1/Wale watu wote waliofanya ghasia mbagala sio waislam sahihi, kwa kuwa uislam ni dini ya amani na masikilizano.
2/Hakuna mahali popote kwenye uislam panapotamka kuwa maadui wa waislam ni wakristo.[/QUOTE]
Concrete: Umetoa ufafanuzi mzuri sana wenye hekima. Maelezo yako ni ya kujenga watanzania. UBARIKIWE
TUngekuwa na Waislamu japo 10 ya Mjengwa hapa Tanzania, hakika nchi ingekuwa ya maana sana. Huyu ana akili. Si hawa wanaoleta vurugu. Swali kwa Mjengwa: Yule aliyekojolea Kuran kafikishwa mahakamani, je, yule aliyempelekea Kuran mbona kaachwa?
Nicholas,Wasomi wa Tanzani walianza tuangusha kihistoria kwa mara ya kwanza walipochanganywa na pesa za mwarabu ,huku wakiwa desperate kutafuta hero wa kiafrica aliyepiga West.Walijikuta wakifanya kazi mbaya na ya kijinga ya kuwaiata akina Mkwawa, mirambo baadaye Mirambo, Kinjekitile Ngwale kuwa mashujaa.Kilichofichwa hapo ni majina kamili ya hao watu na imani zao hadi wanakufa.Hii ndio dhambi ya kwanza na inayowapoa kiburi waislam kuwa hao watu walikuwa mashujaa.Ila hao watu walipigana na kuwaua wamissionary na si hata wazungu mabepari.Sasa wanakwenda kwa Nyerere,na wataendelea sana kadiri wanavyoweza manipulate media na historia na wasomi hewa wetuw anaochanganyiw ambona,kwa mgongo wa ubepari, sijui n aubaguzi wa palestina.
Niliweka article JF kueleze wapi saikubaliani na ushujaa wa mkwawa na fikra za mwambao,Ilifutwa fasta na ban juu.
Nicholas,
..Mkwawa, Mirambo, na Kinjeketile, walianza kutambuliswa zamani sana kama mashujaa wa Tanganyika.
..kumbuka kwamba kuna shule, vyuo vya elimu, viwanja vya michezo, etc vilivyopewa majina ya baadhi ya viongozi hao.
..hivi karibuni, tena hapahapa JF, kuna hint fulani ililetwa ambayo inanifanya mimi niamini kwamba historia ya Mkwawa, Mirambo, Kinjeketile, etc inapaswa kufanyiwa uhakiki.
..kwa upande mwingine, kuna maandiko mengi sana yanayowahusu watawala hao yako ktk mataifa ya nje na sisi wa-Tanganyika hatuna habari nayo.
Mtoi na kundi lako, nadhani umemezeshwa propaganda zinazoenezwa na maadui juu ya lile tukio. Waislamu si wajinga kama mnavyotaka watu wafikri. Issue ni kuwa baada ya mama mmoja wa kiislamu kuripoti hii habari ya kokojelea masahafu kwa mama wa ' bedui'. Yule mama alijibu kwa jeuri 'si makaratasi tu hayo'
Hiki ndicho chanzo cha kadhia nzima ambacho watu hawataki kukizungumza badala yake wanalilia guitar na 'whisky' zilizomwagwa altereni!
Dharau za hawa ndugu zako hazivumiliki, hata humu JF unaona mwenyewe, wako hivyo!
Endelea nao, lakini ufahamu walivyo!