Ya Kikwete yanafurahisha

babu seya kukaa segerea[emoji57] [emoji57] [emoji57]
 
Tanzania tuitoeni ccm madarakani hata term moja tu, watakapo rudi watakuwa wamejifunza mengi sana.
Hii ya kusema Jakaya sijui Magu tuna potea.
Tukiweza kuitoa CCM madarakani tutatengeneza upinzani wa kweli Tanzania
Sio kuitoa tu madarakani kama fashion bila kujua kwanini tunaitoa na nani tutamkabidhi kwa sababu gani. Uganda, Kenya, DRC, Malawi, Zambia walifanikiwa kuwatoa lakini hadi sasa hatupishani. China hawajawahi kubadilisha chama lakini mambo yao yanaenda sawa, shida sio chama bali wanaokiongoza chama na Katiba mbovu.
 
JK alikuwa akisafiri mara kwa mara kwenda nje ya nchi kuimarisha mahusiano na nchi mbalimbali.Huyu wa sasa amekuwa akisafiri mara kwa mara kuzungunguka mikoani kwa ajili ya kuligawa taifa kikanda,kikabila na kichama pia kufanya matumizi haramu ya kununua wapinzani na kuwatisha au kuwapoteza kabisa.
 
JK hakuwa manager alikuwa ni Leader.
 
Mkuu Kenya wanajitahidi sana, lkn kwanini nasema tuwatoe ni kwasababu watanzania wengi wanaamini kujipendekeza kwa viongozi wa CCM na serikali ndio kutoka kimaisha.
Pia CCM wakitoka watu wengi wataacha kuchagua kwa mazoea zaidi
 
Namkumbuka kwa kukumbatia majizi,wauza madawa ya kulevya,matapeli,uwajibikaji duni wa Watumishi wa Serikali
 
Mkuu Kenya wanajitahidi sana, lkn kwanini nasema tuwatoe ni kwasababu watanzania wengi wanaamini kujipendekeza kwa viongozi wa CCM na serikali ndio kutoka kimaisha.
Pia CCM wakitoka watu wengi wataacha kuchagua kwa mazoea zaidi
Kama ninakuelewa kwa mbaaali vilee!!. Kama mtawala akijua kuwa kuna uwezekano wa yeye na chama chake kushindwa uchaguzi siku moja anaweza kufanya yafuayayo:

1. Ama kujilimbikizia mali zaidi, au
2. Kufanya mazuri na kutimiza ahadi zake ili yeye au chama chake kisiadhibiwe
 
Pamoja mkuu
 
Pia ukumbuke hapa katiba itawekwa vzr sana ili kuwe na fair play kwa kuhofia mpinzani alieingia asing'ang'anje madaraka
 
Mimi nakumbuka chai ya Ikulu.
 
Mkuu Kenya wanajitahidi sana, lkn kwanini nasema tuwatoe ni kwasababu watanzania wengi wanaamini kujipendekeza kwa viongozi wa CCM na serikali ndio kutoka kimaisha.
Pia CCM wakitoka watu wengi wataacha kuchagua kwa mazoea zaidi
CCM haitatoka kwa kura..itatolewa na dola
 
babu seya kukaa segerea[emoji57] [emoji57] [emoji57]

Hili halikutokea kipindi cha JK, jaribu kufanya uchunguzi vizuri.. Kesi ya Babu Seya ilianza kuuguruma kabla ya 2005..JK aliingia madarakani 2005-2015.
 
Kwa hiyo huyu aliyepo atafanikiwa katika miaka yake kumi kufikisha maji vijiji vyote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…