Ya Kibiti ni uhuni usiokubalika

Ya Kibiti ni uhuni usiokubalika

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,345
Reaction score
17,584
Siku zote na mara zote watu wanaofanya mauaji kama yanayofanywa kule Mkurunga, Kibiti na Rufiji huwa wanaweka madai yao hadharani ili wahususika ndani na nje ya nchi wayajue kama yanavyofanya makundi mengine duniani kote.

Sasa hawa wa Kibiti hawana wanachoeleza wala kudai hadharani kwa kutuma ujumbe popote pale duniani ili dunia iyafahamu madai yao.

Hawa ni watu ambao wanastahili kusiginwa hadi tone lao la mwisho kama ikiwezekana. Hakuna mtu hata mmoja wa habari anayefahamu hasa nini chanzo cha mauaji yao ili ama waungwe mkono au walaumie na jamii ya kitaifa na kimataifa.

Wanachofanya wao ni uharibifu wa rasilimali zetu (watu, pesa, muda na vitu) k..ipu..mbavu tu. Pesa zinazotumika kulitatua tatizo zingesaidia kulipia mikopo ya shule ya watoto wetu, lakini ona, zinatumika kijinga kabisa. Sio wa Kibiti tu wanaoathirika bali nchi nzima.
 
Mkuu fika MKIRU uyaongee hayo kwenye jukwaa, waambie waje mzungumze kisha utatupa mrejesho..
sihitaji kwenda kule ili niyajue, msemaji wao aende basi hata BBC, DW, Al Jazeera, CNN, n.k. akaseme nini ndiyo madai yao kule. Lakini kuua kimyakimya haitawasaidia hata kidogo. Hata Wataliban, ISIS, Al shabab, Tamil Tigers, Hamas, n.k dunia inafahamu wanataka nini. Hata wapiganaji wa Maji Maji na MAU MAU waliweka wazi malengo yao, hawa ni wahuni tu.
 
Tanzania sio salama saaana kama unavyodhani mkuu.
Angalia wasije wakakutimbia na wewe,
 
sihitaji kwenda kule ili niyajue, msemaji wao aende basi hata BBC, DW, Al Jazeera, CNN, n.k. akaseme nini ndiyo madai yao kule. Lakini kuua kimyakimya haitawasaidia hata kidogo.
Sasa wakiua waziwazi ndio itawasaidia nini?
 
sihitaji kwenda kule ili niyajue, msemaji wao aende basi hata BBC, DW, Al Jazeera, CNN, n.k. akaseme nini ndiyo madai yao kule. Lakini kuua kimyakimya haitawasaidia hata kidogo.
Hujui lengo lao usiseme kuwa haiwasaidii huwezi kujua labda kuuua ndio malengo yako

Polis wameenda wapi !!?
 
Pombe ameshatangaza kuwa wanaofanya hayo mauaji ya Kibiti ni Masheikh wa Uamsho.
Hao Masheikh wamesema hivyo? wapi? wanadai nini? Kwani Masheikh wako Kibiti tu? Unatafuta kupoteza dira na mwelekeo kuhusu haya mauaji.
 
Hawana nguvu mkuu ndio maana hawasemi hadharani. Waseme ili wakamatwe.

Hayo makundi mengine tayari yananguvu na majeshi yakueleweka. Ndio maana hao tunaita ni kama majambazi tuu
 
MKIRU na habari nyingine hayo matamko yenu endeleeni kuyatolea huko chini ya uvungu wa Lumumba
 
sihitaji kwenda kule ili niyajue, msemaji wao aende basi hata BBC, DW, Al Jazeera, CNN, n.k. akaseme nini ndiyo madai yao kule. Lakini kuua kimyakimya haitawasaidia hata kidogo. Hata Wataliban, ISIS, Al shabab, Tamil Tigers, Hamas, n.k dunia inafahamu wanataka nini. Hata wapiganaji wa Maji Maji na MAU MAU waliweka wazi malengo yao, hawa ni wahuni tu.
Jamaa wanaenda staili za kichawi, ila nahisi kuna kitu nyuma ya pazia, jamaa huenda wanatarget yao na pia wahusika labda wanafaham, badala ya wao kutamka wanasubiri wahusika wajiseme wenyewe..
 
Back
Top Bottom