Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,694
- 149,920
Huko Kenya watu wa fani fulani baada ya kupuuzwa kwa muda mrefu na wanasiasa hatimae uvumilivu ukawaishi na wakaamua kuungana na sasa hivi huko kuna wako moto huku kukiwa teyari na madhara makubwa mpaka sasa.
Na huku kwetu kuna mtu mmoja anadhani ukimya na uvumilivu wa watu ni kumuogopa hajui kuwa shida na mateso vikizidi watu huishiwa uvumilivu na kuamua liwalo na liwe.
Yeye aendelee kupuuza tu manung'uniko ya watu akidhani kijiji chote kakiweka mfukoni mwake lakini ajue ipo siku watu watasema basi na akumbuke kabla yake kuliwahi kuwa na mbabe mmoja ambae nae kwa kiburi alipuuza madai ya watu na uvumilivu ulipowaishi kilichotokea kila mtu anakijua.
Uvumilivu una mwisho.
"Mwenzako akinyolewa,wewe tia maji"