Ya Jide, Ally Choki na Kinachoitwa kuzikana!!!


tindikalikali

tindikalikali

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2011
Messages
4,876
Likes
115
Points
135
tindikalikali

tindikalikali

JF-Expert Member
Joined Jan 14, 2011
4,876 115 135
Naomba nianze kwa kusema, binadamu tumeletwa duniani si kwa ajiri ya kuleta matatizo, bali tupo kwa ajiri ya kutatua matatizo. Kuyakimbia matatizo hakujawahi kuwa suluhisho la matatizo hata siku moja.

Katika siku za hivi karibuni nimeshuhudia kauli za kushangaza toka kwa watu ambao mwanzo nilikuwa nikiwaheshimu katika kazi zao.

Mwanzo alianza Jay Dee ambaye sasa anajiita Anaconda kwamba pindi atakapofariki, Ruge na Kusaga wasije kumzika. Na hivi majuzi Ally Choki naye kaibuka na kudai siku akifa, Asha Baraka ambaye ni bosi wake wa zamani asije kumzika.

Wote wawili wameniacha na maswali mengi. Kikubwa nimejiuliza hivi kuzikana ni nini? Hivi mtu akija au kutokuja msibani marehemu itamwongezea ama kumpunguzia nini?
Hii inaleta picha gani katika jamii? Je ni kushindwa kutatua matatizo ama ni kufikia ukomo wa kufikiri?
Hivi kumwambia mtu asije msibani kwako ni kumkomoa ama?

Hawa wasanii kwanini wasikae kimya kama wameshindwa kutatua matatizo yao wakiwa hai? Kutishiana kutozikana kuna tija gani kwao na pengine kwa watoto wao kama siyo mashabiki?

Mwisho niseme huu mtindo unaohasisiwa na hawa wanaojiita kioo cha jamii unapaswa kukataliwa kwa namna moja au nyingine.
 

Forum statistics

Threads 1,272,335
Members 489,924
Posts 30,448,060