Ya Dr Shein na Al Bawardi wa Kempisky | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ya Dr Shein na Al Bawardi wa Kempisky

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Game Theory, May 3, 2011.

 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Kuna news nimeiona Michuzi (siku hizi anabania huwezi ku copy text from his blog), ambazo zinaonyesha how bold huyu Dr Shein is.

  Anasema kuwa hoteli itajengwa Stone Town na asiyetaka akashtaki!

  Sina uhakika na legalities na siwezi kutetea upande wowote kwani sina facts in hand ila one thing is for sure. Dr Shein sio mpole mpole kama ambavyo we were led to believe.

  If only JK would make bold moves kama Shein sasa hivi yafuatayo yangekuwa yanaendelea:

  International Airport ingekunguwa ishaanza kujengwa Bagamoyo

  Port ya Bagamoyo ingekuwa ishakamilika

  Oil pipeline from Dar, Tanga & Mtwara to interior na great lakes region ingekuwa inafikia ukingoni

  Mtwara port ingekuwa ishamalizwa kuwa upgraded na inashindana na Beira

  Serengeti Highway ingekuwa ishaanza kunjengwa mithili ya interstate za kule USA au M1 highway in UK

  Iringa, Mbeya, Tanga, na Mwanza zingekuwa zinapata portion kubwa zaidi kutokana revenues zinazoingia kwao ambazo wangeendelea kujenga airports na infrastructures zinginezo

  Kigamboni Satellite town watu wangekuwa washalipwa na phase 1 ingekuwa imekwisha

  Inshort mambo mengi yangekuwa yanaendelea kama vile serikali ya China inavyofanya.

  Hawa ma eco imperialists na fascists hawawezi kuendelea kui-hold nchi hostage kwa sababu tuu lobby zao ziko headquatered in Nairobi, London na New York.
   
 2. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #2
  May 4, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Rais kaingiwa kiwewe. Barua ya madai juu ya ujenzi wa five star hotel ameandikiwa Mkurugenzi Mamlaka ya Uhifadhi wa Mji Mkongwe na Rais kapelekewa nakala tu. Kwanini asimuache Mkurugenzi kujibu barua kimaandishi kama sheria zinavyoelekeza.

  Kuna taratibu zinazolinda zoezi zima la uhifadhi hivyo ni mapema Rais kucharukia maamuzi ambayo kwao wao wameshafikia na kutoa vibali vya ujenzi kabla ya kukamilisha taratibu za kisheria. Kwanini visiachiwe vyombo vya Sheria.
   
 3. J

  JokaKuu Platinum Member

  #3
  May 4, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,751
  Likes Received: 4,975
  Trophy Points: 280
  ..mbona JK naye yuko bold sana tu?

  ..JK yuko bold na amefanya maamuzi mazito kama kusaini mikataba ya Buzwagi,Richmond, na Dowans.
   
 4. Tumaini Jipya

  Tumaini Jipya JF-Expert Member

  #4
  May 4, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ha ha ha ha ha ha ha ha, We Utazitegua Mbavu zangu!!!
   
 5. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #5
  May 4, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Infact Shein angenyamaza kimya halafu hao watu wa chini yake wakayamaliza kwa kufuata sheria

  haikuwa na haja ya kuzungumza hili in public kwa sababu ina hatari ya kufanya sheria ikapindwa kwa sababu rais kasema

  yale yaleee ya JK kupanga bei za korosho ili hali bodi ndio yenye mamlaka hayo jambo lililoleta huge conflict kati ya serikali na bodi ya korosho
   
 6. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  kwani ni nani aliyesamehe wezi wa EPA mchana kweupe? sio jk kweli!!!!!!
   
 7. k

  kayumba JF-Expert Member

  #7
  May 4, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mkuu nilimuona Dr. Shein jana na kweli sikuamini kama ni yule tuliyekuwa tumemzoea! Japo nimetofautiana sana na jinsi alivyojaribu kuonyesha ujasiri. Aliseama hivi " Pale mji mkongwe zile ni nyumba za serikali, na serikali imetaka kuziuza sasa nani huyo aje kutuuliza kwanini tunauza? Eti mnauliza kwanini hazikufuata utaratibu wa kutangazwa tenda?!!" Huku akionekana kuwashangaa wanaohoji.

  Akasisitiza "Nyumba ni zetu hatutakiwi kutangaza tenda na tukiamua kuuza tunauza, mbona hamkusema tulivyowauzia wengine bila kutangaza tenda?" Ukiangalia kwa makini hapa utagundua ujasiri wake ni kama ule wa Mkapa. Wote mnakumbuka Mkapa alivyosema mtake msitake NMB itauzwa hapo akipuuza madai ya wananchi kuwa ile benki ilikuwa inapata faida.

  Je wale waliomsifu eti ni Bold kwa wakati ule bado wanamsifu kwa maamuzi yale? Kuwa Bold kwa masuala ambayo ni ya msingi kwa jamii huku ukijifanya wewe ndiye mmiliki wa nchi ni ishara mbaya. Asiyejua hilo akajifunze Arabuni, hii tabia ya viongozi kudhani wana haki ya kufanya lolote bila kuhojiwa na wananchi ni kosa kubwa na mara nyingi usababishwa na ulevi wa madaraka.

  Kwa aliyeangalia mahojiano hayo atakubaliana na mimi kuwa Dr. Shein alichokuwa anatetea si sahihi kwa sababu kusema eti mali ya serikali ikitaka kuuzwa hakuna haja ya kufuata sheria za manunuzi ni tabia itakayoturudisha kule kwenye ufisadi mkubwa. Je baadaye ikijagundulika kuna watu wamenufaika na hiyo deal ya kuuza majumba kwa matajiri yeye atasimama kuwatetea?. TAFAKARI
   
 8. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #8
  May 4, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mali ya serikali inapouzwa inatakiwa ifuate sheria ya manunuzi kama ingekuwa mali yake binafsi hapo hakuna mtu wa kuhoji na kumuuliza ila kwa mali ya serikali hapo Dr. Shein amechemsha na anaonekana tayari kilevi cha madaraka kilishapanda kichwani
   
 9. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #9
  May 4, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mie nadhani Rais huwa anakuwa briefed juu ya kila kinachoendelea. Na Rais ambaye yupo makini hapati news kutoka magazetini au watendaji tu bali pia kutoka kwa watu wa usalama. Kwahiyo hata hiyo bei ya korosho huenda anajua ni nini alichofanya.
  Shein yeye aliulizwa msimamo wa serikali, na huenda yale maelekezo yanayotekelezwa na yule mkurugenzi ndiyo maelekezo yale. Kwahiyo alikuwa anajibu la moja kwa moja na hakuwa na haja ya kusubiri. Hii inawasaidia wale wanaotaka kwenda mahakamani wawahi zaidi.
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  May 4, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  inawezekana nchi hii ukiwa rais lazima ufanye madudu!! si bara wala si visiwani
   
 11. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #11
  May 4, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  hiki kiti hakikuwa chake ni cha bilali, ila chakachua ya ccm ndio matokeo yake hayo,
  tatizo ni ccm viti maalumu mkapa kwenye urais,
  nyie subilini hiyo 2015 yakwamba rais anatakiwa kutoka zanzabar,
  kama hawajaweka mwinyi mzee wa milipuko ya mabomu
  sijui lini watanzania tutaondokana na mawazo mgando ili hawa viongozi wasifanye nchi kama mali yao.

   
 12. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #12
  May 5, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,381
  Likes Received: 5,665
  Trophy Points: 280
  Mmh sio mimi
  jamani kwa walioona taarufa ya habari itv na channel ten na star tv walishangaa sana binafsi nimeamini huu ufisadi ni zaidi ya sumu ile inayonyunyuziwa kwenye mahindi wadudu wafe..yaani imesambaa haraka kupita kiasi

  wakati mh huyu akishuka toka turkish watu walijazana kumuuliza wakati akiondoka ameacha makaratasi ya kukabidhiwa jengo moja wallaaahiiii kubwaaa nyiee ati wamemuuzia mfanyabiaashara aka mwekezaji..jengo nila serikali akaulizwa mbona liko kwenye list ya makumbusho....,wazanzibari wamepanga maandamano hivi karibuni ..jamaa alipoulizwa walahi niliona kama sura ya osama yaani alivyobadilika uwiiii

  mh embu tueleze imekuwaje mmeuza lile jengo la serikali ..na mbaya mfanyabiashara huyu anajulikana si mwaminifu kwenye makodi yenu..na mbaya zaidi iweje mmeuza bila kufwata sheria za mauzo kuweka tenda na mengineyo

  dk shein

  nani kakwambia hii mali ya serikali tunauza saa yoyote akuna wa kutuuliza nakwambia kawajibu hivyo tenda tenda mbona huko nyuma zingine azikuuzwa na tenda amsemi

  yesuuuu nipeleekeee kule kwa baba nikaishi nae kule mbinguni kwenye mji wa......
   
 13. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #13
  May 5, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ufisadi Zanzibar ni bomu ambalo siku likilipuka hasalimiki hata kiongozi mmoja, sema sasa wako bize kuzungumzia Muungano.
   
 14. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #14
  May 5, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na Mwajuma Juma, Zanzibar

  VYAMA vitatu vya upinzani vimesema Rais Dkt. Shein anawalinda mafisadi wanaotuhumiwa kuuza majengo yaliyomo katika hifadhi ya Mjikongwe kinyume na
  sheria.

  Tamko hilo wamelitowa kufuatia kauli ya Rais Dkt. Shein kudai serikali haikuwa na ulazima wa kutangaza zabuni katika uuzwaji wa majengo hayo, kwa sababu imeuza mali yake.

  Wakizungumza katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo viongozi wa vyama hivyo TADEA, NCCR-Mageuzi na Chama cha Wakulima (AFP), wamesema mkataba huo uvunjwe ili kulinda sheria namba 9 ya mwaka 2005 ya ununuzi wa Mali za Serikali.

  Katibu Mkuu wa TADEA, Bw. Juma Ali Khatib alisema kwamba Serikali ni ya wananchi na mali inayouzwa ni ya Wazanzibari wote na haikuwa muafaka kukodishwa miaka 99 bila kutangazwa zabuni, kama masharti ya sheria yanavyoelekeza.

  “Rais alikula kiapo kuwa atalinda katiba na sheria, na mawaziri wake pia walikula kiapo inakuaje serikali inashindwa kuheshimu sheria za nchi,” alisema Katibu huyo.

  Alisema kwamba nchi inaendeshwa kwa kuzingatia katiba na sheria na majengo hayo yalistahili kutangazwa zabuni badala ya kuuzwa kienyeji kwa vile sio majengo ya mtu au Ikulu, ni mali ya Wazanzibari wote.

  Hata hivyo, alisema kwamba imefika wakati Wazanzibari wakafahamu haki zao za msingi za kikatiba ili kuepusha tabia ya mali za serikali kuuzwa bila ya kuzingatiwa taratibu za sheria.

  Naye Mwenyekiti wa AFP, Bw. Said Soud alisema inashangaza Serikali ya Umoja wa Kitaifa imeshindwa kusimamia misingi ya utawala bora kwa vitendo tangu kuundwa kwake Novemba mwaka jana.

  Alitoa mfano alisema sheria za kazi zinasema mtu atastaafu kwa lazima baada ya kufikisha umri wa kati ya miaka 50 na 60, lakini badala yake watu waliostaafu na kulipwa mafao yao wamerejeshwa tena katika utumishi wa umma.

  Aidha alisema kwamba hivi karibuni Chama cha Wanasheria Zanzibar, kimekuwa kikilalamika kuhusu uteuzi wa majaji uliofanywa bila ya kuzingatia maamuzi ya tume ya utumishi na maadili.

  Alisema kwamba kwa kuwa serikali imeshindwa kuzingatia utawala wa sheria hakuna sababu ya kuwa na Baraza la Wawakilishi na badala yake livunjwe kutokana na serikali kushinda kuzingatia sheria zinazotungwa na baraza hilo.

  “Katiba ya nchi inasema mamlaka ya kuendesha nchi ya wananchi wenyewe, tunashauri rais avunje Baraza la Wawakilishi badala ya kupoteza fedha kwa kutunga sheria zisizozingatiwa na serikali,” alisema.

  Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Dkt. Shein katika Uwanja wa Ndege wa Zanzibar juzi baada ya ziara yake ya Uturuki, alisema kuwa serikali haikufanya makosa kuuzwa majengo hayo bila kutangaza zabuni kwa vile mali iliyouzwa ni ya serikali.

  “Serikali haifanyi makosa, ina uamuzi wake hasa kwa mali zake hakuna anayeweza kuhoji, tukiamua kuuza jengo tutauza, Mambo Msiige ni ya Serikali hatujauza mali ya mtu,” alisema Dkt. Shein.

  Tangu kuuzwa kwa majengo hayo Oktoba mwaka jana na Serikali ya Awamu ya Sita wanaharakati na wanasheria Zanzibar, wamekuwa wakidai majengo hayo yameuzwa kinyemela kwa dola za Marekani milioni 1.5, bila ya kutangazwa zabuni.
   
 15. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #15
  May 5, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu, sio kuwa ameanza, anaendeleza
   
 16. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #16
  May 5, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kama ni yule Dr Shein ninayemfahamu mimi, hata siku moja yule baba hawezi kumlinda mtu FISADI. Nadhani humjui Dr Shein, hebu jaribu kwingineko siasa hizi.
   
 17. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #17
  May 5, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Chanzo cha habari hii???????????
   
 18. a

  aziz_ally Member

  #18
  May 5, 2011
  Joined: Dec 20, 2008
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Pengine ameingia system mpya
   
 19. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #19
  May 5, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Nadhani umekusudia Zanzibar Mkuu. Au sio?
   
 20. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #20
  May 5, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Huyo unaemjua wewe ni wa 'before madaraka' na huyu anaejibu majibu ya aina ile tuliyoyaona kwenye vyombo vya habari ni wa 'after madaraka'.
   
Loading...