Ya Dangote na aibu ya pande 3: Wanahabari, wapiga dili na mabazazi

Waandishi wa habari kwa sasa wanashindana kwa hali na Mali ili kila mmoja awe wa kwanza kutoa taarifa Fulani ili wapate umaarufu, maskini wamesahau kuwa taarifa tatu safi hufutwa na taarifa moja chafu. Wamekuwa wazembe wa kufanya utafiti wa kina juu ya habar Fulani.
 
yani me kinachonishangaza eti kuna watu hawalali wao wanapenda tu wasikie mabaya kwa serikali ili wapate cha kusema.

uchawi si hadi uruke na ungo hata kutopenda maendeleo ni ushirikina tosha.
Kazi mojawapo ua upinzani and kufichuwa mabaya Na kama wapinzani na waandishi wangekaa kimya nani angepeleka suhala hili kwa rais hivi mfano and leo rais angemtaja muhsika wa kampun ya aqua mnahisi angetoka upande gani upinzani au tawala
 
Siku hizi kila siku issue ikazingua na mpiga deal tu analaumiwa hawa wapiga deal hawajulikani ??mbona hamna hata mmoja amewah kutajwa?
Hawa wapiga deal ni majini au vibwengo kulikoni!!
 
kuna watu hawaitakii mema hii nchi kabisa unaweza kudhani watu hawa ni raia wa nchi jirani labda conflict of interest ndio inaleta hizi chuki za wazi!cha ajabu ni wazawa wa tanzania wenyewe
 
Ni suala la muda tu, hata hii Thread yako utakuja kuikana hapa hapa.

Suala la Dangote ni suala nyeti na tata sana, alichokifanya Rais ni "kupunguza Kelele za ndani ya chumba zisitoke nje kwa kuweka Sound Proof".

Kama unabisha, jaribu kujiuliza swali hili, Mpaka sasa serikali imeshatoa kauli nzito kama Tano kuhusiana na issue ya Dangote, na kauli zote zinatofautiana. Kwanini?
Kuna selikari zaidi ya Magufuli au Rais? Fikiria mara mbili. Hapo ndiyo mwisho wa reli ndugu yangu. Ama uifuate na kama huko tayari kuifuata basi unaachia iende na wengine. Nadhani umenielewa.
 
Ni suala la muda tu, hata hii Thread yako utakuja kuikana hapa hapa.

Suala la Dangote ni suala nyeti na tata sana, alichokifanya Rais ni "kupunguza Kelele za ndani ya chumba zisitoke nje kwa kuweka Sound Proof".

Kama unabisha, jaribu kujiuliza swali hili, Mpaka sasa serikali imeshatoa kauli nzito kama Tano kuhusiana na issue ya Dangote, na kauli zote zinatofautiana. Kwanini?
Endelea kuzungusha mikono wakati mwenzako anashusha magari 650 Bandari ya Mtwara sasahivi
 
Endelea kuzungusha mikono wakati mwenzako anashusha magari 650 Bandari ya Mtwara sasahivi
Na atahitaji madereva maelfu na mafundi magari. Wacha Dangote atuonyeshe jinsi viwanda vinavyofanya kazi. Tuige mfano kwake kama role model wetu. Big up Alhaj Dangote
 
Rais ameshatoa kauli na Kauli ya Rais ni ya Mwisho kwa upande wa Serikali.
Second Aliko Dangote ameshatoa kauli na kauli yake ni ya Mwisho kwa upande wa Kiwanda. Sasa unasubiri nini tena wewe? Kiwanda hakiondoki na malighafi zitanunuliwa hapa hapa. Full stop
Bavicha huyo roho inamuuma sana baada ya Magufuli na Dangote kumaliza issue hii, sasa wanakula na uzushi mpya kwa kuyaponda magari ya Dangote
 
Siku hizi kila siku issue ikazingua na mpiga deal tu analaumiwa hawa wapiga deal hawajulikani ??mbona hamna hata mmoja amewah kutajwa?
Hawa wapiga deal ni majini au vibwengo kulikoni!!
Jaman iyo misemo anapataka huku jamiiforum sasa anaitumia bila kudhani ye ndo mnene bongo
 
Ni suala la muda tu, hata hii Thread yako utakuja kuikana hapa hapa.

Suala la Dangote ni suala nyeti na tata sana, alichokifanya Rais ni "kupunguza Kelele za ndani ya chumba zisitoke nje kwa kuweka Sound Proof".

Kama unabisha, jaribu kujiuliza swali hili, Mpaka sasa serikali imeshatoa kauli nzito kama Tano kuhusiana na issue ya Dangote, na kauli zote zinatofautiana. Kwanini?
Acha papara we bazazi...upinzani jipangeni upya..hapa ni kazi juu ya kazi yani bamba to bamba...
 
Sakata la Dangote limekwisha katika staili ninayoweza kuifananisha na fasihi moja isemayo "Zama Zimebadilika."

Na sasa kilichobaki ni aibu kwetu-tena aibu ya pande tatu.

Ukilitazama sakata hili utakubaliana nami kuwa Watanzania kwa sasa ama tubadilike na wakati au tusubiri wakati uendelee kutubadilisha.

*Waandishi wa Habari*

Katika sakata hili ndugu zetu hawa walionekana kubeba maslahi ya kizani badala ya usahihi.Hawakutaka kusaka ukweli na kamwe kusaka ukweli kwao haikuwa ajenda.

Walikuwa tayari kumhoji na hata kuitaka jamii imuamini machinga aliyeko Kilwa anapozungumzia sakata la Dangote kuliko kuwapa nafasi wataalam wanaojua kiini cha tatizo

Ndo maana, kwa wanahabari hawa ambao juzi tu wametoka kukataa sheria inayowataka wakasome, siku alipozungumza mhandisi mmoja makini wa TPDC kuhusu uwepo wa gesi ya kutosha na kwamba ni "watu" wa Dangote ndio wanakwepakwepa kukubali bei waanze kununua wanahabari wetu walimpa nafasi zaidi Machinga mmoja wa Mtwara aliyekuwa anaropoka tu‍♂‍♂‍♂

Yani kabisaaa mwandishi wa habari unampa mtu ukurasa wa mbele kisa kasema eti Dangote atahamishia kiwanda Kenya??Umeshatembelea kiwanda cha Dangote kweli?Mnajua sababu za kistratejia za kujengwa Tanzania na si popote ktk EAC?Kama haya si maswali muhimu kwenu tena basi fani hii imevamiwa.

Kama tuna waandishi wasiojua kuhoji haya basi kwa leo hawa jamaa acha niwaachie moja tu la mwisho; kwa uandishi huu sasa mmeanza kuihama wenyewe fani yenu na mnakuwa *wahandisi* badala ya *waandishi* wa habari.

Lakini moja tu mlijue: kama mnataka kuhamia huku nako basi mjue kama mliikimbia dhana ya elimu kule basi mjue katika huku katika uhandisi nako ndio kabidaaa kuna vigezo vikali vya elimu. Muwe tayari.

*Wapiga Dili*

Hawa walizoea.Mazoea yanatabu kwao Bwana.Waliingia kati na kuwachanganya au kupiga dili na "watu" wa Dangote.

Hawa hawakujua kisa cha nyakati.Waliendelea kuamini katika uwezo wao wa kuruka vihunzi wakiwa na briefcase zao bila kujua nyakati zimrbadilika.

Kumbe zama zile zilikwisha kitambo wakafika walipofika sasa wameparaganyika sawa na yaliyomkuta yule Diwani mashuhuri wa viunga flani Dar es Salaam.

*Mabazazi*

Hawa nao labda kama wale wenzangu wa kundi la kwanza hapo juu wameamua kuuza Utanzania wao.

Hawa kila wakiamka asubuhi wanazua jipya na kutafuta jipya jingine la kuzua jioni.

Utawakutana asubuhi wanamwaga povu kwenye vijiwe vyao kuwa nchi gani haina hata shirika la ndege; zikinunuliwa jioni utawasikia ndege gani zile!

Utawasikia asubuhi wanalalamika nchi haina ajira kwa vijana lakini waliposikia uzushi kutoka kwa jamaa zao wawili hapo juu kuwa eti Dangote atahamishia kiwanda Kenya wakaruka juu wakishangilia: "Afadhali acha aende kule tu."

Sasa ukitaka kujua ubazazi ni ugonjwa mbaya labda kuliko ule wa jamaa zetu wawili hapo juu ni hili:

Alhaji Dangote mwenyewe kaja nchini kasema haendi kokote, ndio kwanza jana hiyo hiyo kashusha malori 600+ na atajenga kiwanda kingine Tanzania, nimepita jana kijiweni mabazazi wamenuna balaa

Nimepita tena leo kijiwe kimekufa kabisaaa.Watu wamenuna na hawajaja kijiweni.Labda wanatafuta jingine tena

*By Political Jurist, UDOM*

Copy and Paste wandugu.Nimeikuta mahali hii
Wewe ndio mpiga dili mkubwa unaandika pumba tupu. Issue ya Dangote bado mbichi, utakuja kuona. Pale Rais amefunika kombe mwanaharamu apite.
 
Ila Waandishi wa habari wa Tanzania ni janga jingine la Kitaifa.

Tuna waandishi bomu hakunah! hasa waandishi wa magazeti. Wamekuwa washabiki, watu watetesi na wana kiherehere cha kuandika badala kutulia, wakafanya utafiti ili kuufahamu ukweli halisi.
 
Niliona uzi humu wiki iliyopita ukihoji uzito wa Dangote katika uchumi wa TZ. Mpaka Rais amekubali kukutana na Dangote mwenyewe itoshe tuu kuonyesha umuhim wa Dangote..
Mi naomba niseme hivi,
Sio umuhimu wa Dangote bali ni umuhimu wa viwanda ama uwekezaji.
Nisinge penda ionekane kama Rais kaingia kwasababu ya Dangote.
Hapana awe amefanya kwa maslahi ya Taifa kwa upande wa uwekezaji na hasa foreigners investors.
Kujenga picha nzuri ya Nchi yetu kwa wawekezaji.
 
Back
Top Bottom