Ya BASATA na Shilole

Ya BASATA na Shilole

Ngwananzengo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2012
Posts
1,911
Reaction score
1,320
Tumesikia na kuona kupitia vyombo vya habari kile alichofanya msanii Shilole a.k.a Shishi baby kwenye onyesha alilofanya nchini Ubelgiji. Baada ya taarifa na picha za tukio Hilo kusambaa BASATA ilimuita Shilole kwa mahojiano zaidi. Binafsi Sijui alivyojenga hoja zake katika kujitetea lakini nalaani adhabu iliyotolewa kwa msanii huyu na BASATA.

Mosi kwa sababu adhabu hii imejaa unafiki mwingi ndani yake. Kwa wale wanaoishi miji mikubwa ndani ya nchi yetu watakubaliana nami kuwa hakuna cha ajabu alichofanya. Pili adhabu hii si adhabu bali ni aina fulani ya kukomoana. Najiuliza ni adhabu ya aina gani inayoenda kuua ustawi wa mtu na familia yake.

Mwaka 1bila ya kufanya Sanaa akale wapi binti wa watu. Tatu hii inadhihirisha ile hali ya watendaji wengi ktk taasisi za umma kutokufikiri kwa mantiki. Kwa masikitiko makubwa nakupa pole sana Shilole kwa adhabu hii ya kijinga.

Wito wangu waone wanasheria wakupe ushauri wa kisheria
 
Wakati mwingine huwa natafakari na kujiuliza, hivi kweli tumejitahidi vya kutosha kufikiri na kupambanua mambo. Mungu yupi unaemsema? Je, kile unachokiamini wewe ni lazima wengine pia wakiamini?
 
Shilole ameitwa jumla mara tatu kuhusiana na uvaaji wake na uchezaji wake usio na maadili na BASATA

Mara mbili amekua akionywa abadilike na kujihrshimu lakini akawa anachukulia poa tu
Sasa hii mara ya mwisho aliitwa akajitetee kwa yaliotokea ubelgiji na baada ya maelezo yake basata wakajiridhisha huyu shishi ndio zake na hana sababu za msingi wakampiga ban

Kiukweli adhabu ipi very harsh and unfair

Wajinga wajinga kama hawa unatwanga faini tu ya kutosha na atanyooka mwenyewe
 
Unapoambiwa usivae ovyo.. Wewe ukavaa ovyo.. Ukajifanya wewe ni mjuaji zaidi.. Wewe imara zaidi.. Utafungiwa tu, eeeh maana lazima tukubaliane BASATA itaongozwa kwa misingi ya sheria ( in Pinda's voice)
 
mhhhhhhhhhhhhhhh
 
Nuh Mziwanda mbona unalalamika sana?
 
Kwanini wasingefanya faini badala ya kumfungia ??????????????
 
Unapoambiwa usivae ovyo.. Wewe ukavaa ovyo.. Ukajifanya wewe ni mjuaji zaidi.. Wewe imara zaidi.. Utafungiwa tu, eeeh maana lazima tukubaliane BASATA itaongozwa kwa misingi ya sheria ( in Pinda's voice)

Nakubaliana na wewe kweli alivaa Hovyo, hebu tujiulize kuvaa huku Hovyo kumemuumiza nani ktk jamii na Taifa? Maana tumekuwa tukilinda maadili yasiyokuwepo na Mfano mzuri ni kitendo cha wale tunaowaita waheshimiwa (Mh Job & Mh Wasira) kupigana hadharani na kutoa lugha ya matusi, kama kweli Sheria ni msumeno mbona hawa hauwakati? Au nchi hii sheria ni kwa wanyonge tu kina "Shishi baby".
 
Pindi alivyoitwa na BASATA kujieleza ,mngempa ushauri wa kwenda kujitetea.Alipoitwa mkakaa kimya bila kumshauri aende kwenye baraza ,leo baraza limefata kanuni zake ndio mnajitokeza kumuonea huruma.Usivunje sheria ya nchi kisa mwingine mbona anavunja.
 
Ni kweli kosa halihalalishi kosa. Lakini jamii kuwa na watu walio juu ya sheria na wengine walio chini ya sheria si jambo lenye afya kwa jamii husika. Kikubwa ninachojiuliza hivi kile alichofanya "Shishi baby" kimemuumiza nani ktk jamii na Taifa kwa ujumla? Au ndio kuua mbu kwa gobole.?
 
Mkuu naamini angeenda pale alivyoitwa ,adhabu isingekuwa kubwa hivyo maana angeweza kujitetea na wao pengine wangeelewa baada ya kupata ufafanuzi kutoka kwake.Hii adhabu waliyompa nadhani imeongezeka kwa kudharau chombo ambacho kipo kwa mujibu wa sheria.Siku zote uitwapo kwenye shauri unatakiwa utekeleze wito wao.
 
Back
Top Bottom