Xiomi Redmi note 12 4G Vs Samsung Galaxy note 9

Hivi hii Redmi note 10pro napata Kwa Bei Gani mkuu, nkaitafute huku najua Bei yake
Kama una 560,000 hakikisha unapata 6GB RAM 128 GB
Kama una laki 6 hadi 7 hakikisha unapata yenye 8GB RAM 128GB ROM
 
Kununua iphone, Samsung, matoleo ya 2019, huo ni ulimbukeni, mahitaji Yako yatakupa simu sahihi, , Mimi natumia Tecno common 19, full unyama.
Nenda gsm arena ukacheki specification na kucompare simu mbili .
 
chukua redmi note 12
 
Kaka naomba abc za Samsung A54 nataka nijilipue next month
Samsung Galaxy A54 ni simu nzuri sana. Hapa Bongo ukiwa na laki 9 ukipata yenye 8GB RAM 256GB ROM sio mbaya

Uzuri wake
*Design iko poa, inafanana na Galaxy S23+
*Utapata kamera poa sana, hata selfie camera inarekodi 4K videos.
*OLED display, 1000nits, 120Hz na rangi ziko accurate sana
*Unapata Android 13 na One UI 5.1
*Utapata 4 years of major Android updates na 5 years One UI updates. Hii iko mbele kuliko wapinzani kwa mfano kwenye Google Pixel 7A unaweza kupata 3 years of software support, au kwenye Xiaomi Poco F5 utapata 3 major Android updates na 4 years MIUI updates, kwa hiyo tunaona Pixel 7A itakuwa supported hadi 2026, Poco F5 itakuwa supported hadi 2027 Ila hii A54 itakuwa supported hadi 2028.
*Utapata sehemu ya kuweka memory card
*Ina IP67 rating na stereo speakers pia
*Inatunza Sana chaji

Ubaya wake
*Ila chipset yake ni Samsung Exynos 1380 kwa hiyo performance yake ipo chini kuliko wapinzani wake kama Google Pixel 7A ambayo ina Google Tensor G2 na Xiaomi Poco F5 ambayo ina Qualcomm Snapdragon 7+ Gen 2. Kwa hiyo note down, kama wewe sio heavy gamer basi A54 itakutosha, ila kama unataka performance kubwa ni heri uchukue Pixel 7A au Poco F5
*Slow charging, actually charging ni slow kuliko wapinzani. A54 ina 25W charger kwa hiyo kuichaji itachukua zaidi ya saa moja. Ila A54 inatunza sana chaji kwa hiyo sidhani kama 25W haitoshi ila wapinzani wako faster zaidi. Akina Xiaomi ambao wanatumia dakika 30 hadi 45 kujaza simu kutoka asilimia 0 hadi 100
*Kwenye box kuna simu na waya tu. Hakuna charger, kwa hiyo unapaswa kutafuta charger mwenyewe.


Samsung Galaxy A54 ni chaguo bora sana na ni ngumu kutokushawishi ununue simu hiyo. Licha ya kuwa A54 ni midrange bado unapata long software support, design nzuri kama S23+, kamera bora kuliko washindani wenzake wa bei hiyo, software yake in features nyingi kama S23 series tu kasoro feature ya Samsung DeX, ina IP67 rating kwa hiyo ni water resistance, ina sehemu ya kuweka memory card, kamera ya mbele inarekodi video nzuri sana. Kwa nini usinunue simu kama hiyo. Nunua tu usifikirie mara mbili mbili

Binafsi ningechukua Poco F5 kwa sababu ni bora kuliko A54 kwenye sehemu nyingi, ukianza na Qualcomm Snapdragon 7+ Gen 2 ambayo ni SoC bora kuliko hata Snapdragon 8 Gen 1. Pia inakuja na 8GB/12GB RAM badala ya 6/8 GB RAM ya kwenye A54, Poco F5 haiji na storage ya 128GB bali zote zina 256GB tu tofauti na A54 ambayo ina hadi 128GB version, pia inakuja na 3.5mm jack.
Ila sasa Poco F5 ni mpaka uagize kutoka China kupitia AliExpress.
 
Sasa laki 4 ulitaka simu gani? Ongeza hela. Hiyo ulinganishe na Redmi?
Ndio ukubali kuwa kwa laki 4 simu bora ni Redmi Note 12
Sasa hiyo A04s ndio ufananishe na Redmi Note 12?
Kwa laki 4 kama shida yako ni Samsung tafuta Samsung Galaxy A14 5G, ingawa sio bora kushinda Redmi Note 12 ila at least ina make sense kuliko hiyo A04s ulioitaja
 
mkuu upo vzuri
 
Hivi mkuu Xiaomi kwa sasa nikitaka simu nzuri kwa budget ya 850K utanishauri nichukue simu gani?

Currently natumia Poco F3 ila nimeichoka nataka nibadilishe,naomba niambie ipi unahisi itaizidi hii.

Shukrani!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…