Xiaomi 13 pro: Simu bora ya Xiaomi 2022

Niko na Note 13pro nimeilaza charge mpaka asubui hafi hivi navyoandika hapa imegoma kuwaka leo wiki sasa. Ukiweka charge inavibrate tu
Kiukweli hiyo Note 13 Pro, sijajua ni simu gani
Ila jaribu njia mojawapo
  • Bonyeza Power button kwa sekunde 10 hadi 30 hivi, halafu tulia kama itakubali kuwaka. Ikishindikana jaribu njia nyingine
  • Au, press hiyo power button kwa muda na usiiachie. Hivyohivyo ukiwa umeihold chomeka chaja na endelea kuhold hivyohivyo hadi iwake. Ikikubali kuwaka irestart
  • Au kama betri yake inatoka basi itoe na uirudishe tena
  • Au iconnect simu yako na kompyuta kwa kutumia waya wa USB, acha ichaji kwa dakika 15. Halafu chomoa waya kutoka kwenye simu (sio kutoka kwenye kompyuta) hakikisha waya wa USB unabaki palepale kwenye kompyuta, we chomoa simu tu waya uache.
Baada ya kuichomoa simu, tulia kwa sekunde kumi na uichomeke tena kwenye chaji. Ichaji tena kwa dakika 30. Baada ya hapo press power button kwa sekunde 5 halafu tap restart. Kama hujaiona restar, endelea kupress na kuhold power button kwa sekunde nyingine 30.
* Ukishindwa njia hiyo jaribu kupress button ya volume down na power button kwa pamoja kwa sekunde 10 hadi 30
Njia zote hapo zikigoma tafuta msaada kwingine, mfano peleka simu kwa fundi au mconsult CHIEF MKWAWA
 
Ni 13 pro.

Nimejaribu njia zote hizo imegoma kabisa Mkuu, mpaka nimefikia uamuzi wa kuifungua nika disconnect betri labda itakubali, imegoma kabisa. Simu hii niliagiza, na ni mwezi wa 12 mwishoni ndio ikafika yaani sijaitumia hata mwezi. Hata pesa sijamaliza kumlipa aliyeileta imeniletea mapicha haya Mkuu. Mimi mwenyewe ni Fundi, wa Software ( Mobile Software ) hardware si sana. Sasa nilikuwa naomba muongozo je hizi zina sensor kwamba iko overcharge inakata ama inaua Display? Kwa sababu nikiichomeka ktk PC inaonekana kisha inatoka, force restart inagoma pia. Nashindwa kusambua mkuu sababu daah hela kibao halaf nimetumia nusu mwezi tu, nimenunua mpya kabisaa
 
Hiyo 13 pro ni Xiaomi au iPhone?
Halafu kama nilivyokuambia hapo mfuate Chief Mkwawa, hata pm. Mambo kama haya yeye ndo anajua shida ni nini anaweza kukusaidia. Hapo ukute simu ni nzima kabisa halafu unaifungia ndani wiki nzima kumbe solution ni simple tu.
So.. tafuta humu JF kuna watu ni maexpert na wengine ni mafundi simu, mimi haya mambo siyajui sana aisee.
Consult experts
 
Nilitaka kuchukua oppo a17 kwa 370k
 
Nilitaka kuchukua oppo a17 kwa 370k
Hiyo bei ni ya wapi?
Kama shida yako ni Oppo, hiyo chukua tu kwa bei hiyo, nimeangalia hapa kuna mambo kadhaa yamenivutia kulingana na hiyo bei ( Oppo A17 sio Oppo A17K)
  • Kwanza, ina option moja tu 4GB RAM na 64GB ROM haitamchanganya mnunuaji
  • Halafu kamera yake ni nzuri kuliko simu nyingi za bei hiyo
  • Brightness ya display yake inafikia 480nits
  • Ina fingerprint pembeni (sio nyuma)
  • Muonekano wake kiujumla unavutia
  • Inatumia Android 12
Japokuwa ichukue kama perfomance kwako sio kipaumbele, inatumia chipset ya MediaTek Helio G35, hii ni weak chipset ila kuna option ya kuexpand RAM mpaka 4GB zaidi. Kwa hiyo unaweza kuexpand RAM kutoka 4GB hadi 8GB na kuexpand ni rahisi tu[emoji28][emoji28]. Ukiexpand RAM haitoweza kuboost perfomance sanasana itasaidia multitasking
Ila amezingua kutumia storage ya eMMC 5.1, bora angetumia UFS 2.2. Ila pia anatumia microUSB charger ila ingependeza kama angetumia USB Type C 2.0.
Hakuna simu iliyokamilika kila kona[emoji28][emoji28] kama unataka Oppo, chukua tu hiyohiyo ( kwa 370,000Tsh)
 
Same here, Nilianza na Redmi Note 5 pro yangu naipenda sana, nikaenda redmi Note 8 kisha note 8 pro, Kisha Note 10 pro 5G kisha nikashuka ghafla mpaka Redmi 9A [emoji3][emoji3] hiki chuma kinakaa na chaji siku mbili plus na data on... Baadae Nikarudi kwenye Redmi note 5 pro yangu ya awali niliyonunua 2018 ikarudi mikononi mwangu [emoji3][emoji3][emoji3] what a Joke! Ndio niko nayo mpaka sasa ..... Imepita Mikononi mwa watumiaji wawili na sasa imenirudia ni bado chuma kinapiga kazi haswa... Battery tu ndio limekua dhaifu ila nina mpango wa kulibadilisha... Ni gb 4/64 hivyo inakidhi kabisa mahitaji yangu ya storage.


Kuna wale wanataka simu GB 256 sijui wanajaza mashetani.? [emoji3][emoji3]

Sent from my Redmi Note 5 using JamiiForums mobile app
 
Sasa hiyo Note 10 Pro ilipotelea wapi[emoji23][emoji23]
 
Naona kioo chake kizuri kushinda washindani wake wa bei hiyo
 
Nina bajeti ya laki tano na nusu simu gani nzuri ya redmi naweza kupata?
 
Nina bajeti ya laki tano na nusu simu gani nzuri ya redmi naweza kupata?
Laki 5 na nusu unapata "Xiaomi Redmi Note 10 Pro" yenye 4GB RAM na 128GB ROM. Angalia specifications zake hapa Xiaomi Redmi Note 10 Pro: specs, benchmarks, and user reviews

Au ingia Mlimani City, nenda kwenye office za Tigo shop. Nunua "Xiaomi Redmi Note 11" yenye 6GB RAM na 128GB ROM. Bei yake ni exactly 550,000/= fixed ukinunua Tigoshop. Angalia specifications za Redmi Note 11 hapa Xiaomi Redmi Note 11: specs, benchmarks, and user reviews
 
Mkuu nisaidie Mwanza nipate Redmi 11 lite.
 
Mkuu nisaidie Mwanza nipate Redmi 11 lite.
Redmi 11 Lite siijui. Lakini Redmi Note 11 ndio naijua. Kwa kuwa sipo Mwanza siwezi kujua ni wapi utazipata.
Jaribu kwenda Tigoshop ya Mwanza. Wanauza simu bei sawa mikoa yote. Xiaomi Redmi Note 11 ya 4GB RAM 128GB ni 530,000/= na Xiaomi Mi 11 Lite ya 8GB RAM na 128GB ROM inauzwa kwa TSh 850,000/=
 
Simu zao nzuri, tatizo ni hiyo MIUI ina mauzi ya hapa na pale kama ku crush, kuwa slow nk. Mi nawahama sasa, tukutane oppo
Mimi ni mtumiaji wa MI 11 5G. Mwaka pili huu sijawahi pata hizo changamoto unazosema. Kikubwa kinachokera ni matangazo. Software zao nyingi zinakuwa na matangazo ya biashara. Mchina bwana.

Otherwise, ni simu bomba sana kwa hili toleo nililonalo.
 
Nina MI 11 5G mwaka pili huu sasa. Sijawahi jutia.
 
Bado nina imani na Xiaomi. Hata hivyo, ili kuepuka stress ninanunulia soko la nje,Ulaya. Mwaka wa pili huu MI 11 5G utasema inetoka dukani leo. Chuma ya ukweli 👏👌
 


Unatumia Oppo Gani Mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…