Xiaomi 13 pro: Simu bora ya Xiaomi 2022

High end gani isiyokaa na chaji
Mi natumia S20 iko vizuri tu, tofauti na REDMI note 10 ni fast charging
 
Aisee wapi nitapata mix fold 2 kwa Dar?
Duh...hiyo agiza tu AliExpress, tumia DHL mzigo ukufikie
Bongo kupata ni ngumu sana, agiza kupitia AliExpress, Amazon au eBay
 
One plus alishapoteza identity yake ya zamani.

Asus Zenfone ndo simu zimeanza kuwa nzuri na bora almost kwenye kila department.

Sema ni brand mpya haina jina sana sokoni.
 
One plus alishapoteza identity yake ya zamani.

Asus Zenfone ndo simu zimeanza kuwa nzuri na bora almost kwenye kila department.

Sema ni brand mpya haina jina sana sokoni.
Ni kweli Asus ni simu nzuri, ninazijua ila sizifuatiliagi
 
Mkuu nataka kuhamia oppo, nitegemee nini hasa mimi napenda kioo kizuri na chaji ikae kutwa nzima
 
300k - 400k
Mkuu Oppo ni simu nzuri sana lakini kwa bajeti hiyo hapa Bongo sio simu nzuri. Labda uagize nje au ununue used. Ngoja nikupe mifano kulingana na bei za hapa Tanzania (za madukani)
  • Kwa TSh 340,000/= unapata Oppo A16K ya (3GB RAM 32GB ROM) ambayo kwa hii bei umepigwa sana. Simu hii ina chipset ya MediaTek Helio G35, hii chipset ni mbaya na kama una matumizi mazito haitakufaa, pia chipset hii inatumiwa kwenye simu nyingi za Infinix au hata Redmi 9C. Hivyo usitegemee perfomance nzuri. Ukiachana na hapo pia storage yake ni eMMC na bado charger yake ni microUSB. Kamera haina maajabu ni ya kawaida sana. Ukinunua hii simu utakuwa disappointed
  • Lakini kwa TSh 340,000/= hiyohiyo hapa Bongo unaweza kupata Oppo A17K ya (3GB RAM 64GB ROM) hii simu siyo nzuri nayo, inatumia chipset ileile ya Helio G35 ambayo ni weak, kamera yake ya nyuma ni 8MP na haifai hata kwa matumizi ya picha za kila siku, RAM ipo moja tu, ya 3GB RAM hakuna option nyingine. Sasa kwa chipset weak kama hii 3GB RAM ni ndogo sana tena kwa bei hiyo umepigwa. Kikubwa tu ni kwamba display yake inafikia brightness ya 600nits ila hii simu haifai kabisa, tena inatumia microUSB charger, binafsi sikushauri ununue hii.
  • Kwa TSh 440,000/= unapata Oppo A55 5G, yenye (4GB RAM 128GB) kama lilivyo jina lake hii simu inakuja na 5G.Inatumia chipset nzuri ya MediaTek Dimensity 700 na storage ni 128GB. Charger yake ni USB Type C na kamera yake ni ya kawaida sana kwa bei hii. Kwa kuwa bei imefika laki nne na kitu bora ununue Redmi Note 10 (plain) ambayo inarekodi 4K videos hii Oppo inarekodi mwisho 1080p, Redmi Note 10 ina SoC nzuri ya Snapdragon 678, ina kamera kali, display yake ni AMOLED hii Oppo ina LCD, Redmi Note 10 display yake inafikia brightness ya 1100nits, hii OPPO inaishia 480nits, Display ya hiyo Oppo ina resolution ya 720p wakati Redmi ina 1080p, kikubwa tu Oppo ni 5G.
Nisikuchoshe, najua unataka kuihama Xiaomi, ila ni ukweli usiopingika kwa sasa Bongo hii, kwa shilingi 350,000/= hakuna simu nzuri kama Xiaomi Redmi 10C, kwa sababu zifuatazo
  • Redmi 10C inatumia chipset ya Qualcomm Snapdragon 680, ambayo hii ni gaming chipset kabisa. Ni strong kwa hiyo kama una matumizi mazito itakufaa hii. Simu nyingine za bei hii zina MediaTek Helio G25, G35, P22, P35, A25 na kadhalika, hizi zote ni mbaya hazifai kutumika kabisa, unaweza kuexperience laggs, apps kufunguka taratibu n.k. Redmi 10C inafungua applications kwa haraka zaidi kuliko hata simu nyingi tu za laki nne na nusu hadi laki 5.
  • Redmi 10C inatumia storage ya UFS na sio eMMC kama ilivyo kwa simu nyingi za laki tatu
  • Kwa 350,000/= unapata Redmi 10C ya (4GB RAM 64GB ROM) na 380,000/= unapata yenye (4GB RAM 128GB ROM) Tanzania hapahapa.
  • Redmi 10C inatumia charger ya USB Type C 2.0 wakati simu nyingi za laki 3 zinatumia microUSB charger
  • Redmi 10C inasupport GCAM, simu nyingi za laki 3 hazisupport hii kitu. GCAM itakusaidia kuongeza ubora wa picha utakazopiga
  • Redmi 10C ina kamera nzuri kuliko wapinzani wake wa bei hiyohiyo
  • Redmi 10C ina AnTuTu score kubwa, zaidi ya 240,000, simu nyingi za laki tatu score zake zinarange 140,000
  • Redmi 10C ina display kubwa 6.71inch, simu nyingi za laki 3 zina 6.5inches
Ila ukinunua Redmi 10C usithubutu ku-update software, usije ukaja kutukana Xiaomi zote humu ndani[emoji23][emoji23]
Maamuzi ni yako tu. Labda umuulize CHIEF MKWAWA akushauri simu kali ya Oppo kwa bei hiyo, na wapi unaweza kupata kwa bei hiyo.
Oppo ni tamu sana kama ukitumia hizi Reno Series kama aliyopost huyo jamaa The Monk ila bei yake iko juu kidogo, zenyewe ni midrange. Pia Oppo tamu zaidi ni Oppo Find X-series ila bei zimechangamka sana[emoji28][emoji28]
 

Ahsante Kwa uchambuzi murua mkuu, hii waliniuzia pale City Mall wakati zinaingia ingia. Ilienda Kwa 1.2M ikiwa na warrant ya mwaka 1. Inafanya updates vizuri tu. Kiufupi Hadi Sasa sijutii maamuzi yangu.

Kitu ambacho sikielewi vizuri ni hapo kwenye RAM 8+8
 
Hiyo inamaanisha unaweza kuexpand RAM kutoka 8GB na kuongeza 8GB RAM nyingine kufikia 16GB RAM na inaweza kusaidia kuongeza perfomance. Hii ipo kwenye simu nyingi kutoka China kwa sasa, zinaprovide RAM Expansion. Sijui unaexpand vipi. Again kuhusu RAM expansion, muulize huyohuyo CHIEF MKWAWA.
Huwa napenda kuwaambia watu wamconsult huyu jamaa, maana hii ndio fani yake, Lazima atakuwa tu anajua haya mambo ya RAM Expansion[emoji41][emoji41]
 

Namie naelewa kwamba unaweza kufanya expansion, ila unafanyaje ndio mtihani ulipo. Ila naamini nikitulia, nikitu naweza kukielewa na kufanya.

Mkwawa inabidi tu apewe tuzo kwenye uwanja wa tech. Hivi hakupendekezwa kwenye zile awards?
 
Namie naelewa kwamba unaweza kufanya expansion, ila unafanyaje ndio mtihani ulipo. Ila naamini nikitulia, nikitu naweza kukielewa na kufanya.

Mkwawa inabidi tu apewe tuzo kwenye uwanja wa tech. Hivi hakupendekezwa kwenye zile awards?
Mkuu jaribu kwenda Settings then About phone, then RAM Menu. Ingia kwenye RAM Menu halafu chagua kiasi cha RAM unachotaka kuexpand, ila hakikisha kuna storage imebaki itakayotosha kumudu hiyo expansion yako. Ukishachagua hiyo RAM then Restart simu hapohapo. Mpaka simu ikijiwasha tena tayari unakuwa ume-expand RAM.
Hapo maana yake unasacrifice storage ili kuruhusu expansion ya RAM.
Ikishindikana basi endelea kutafuta njia nyingine ya kuexpand RAM
 

Kumbe hapo ilipo ndio tayari ipo kwenye hiyo state ya ku expand. Ila unachagua u expand Kwa 4GB, 6GB au 8GB.

Inamaana hapo Cha msingi ni hapo kwenye kuchagua option ya kuruhusu RAM expansion na kiasi unataka.



 
Niko na Note 13pro nimeilaza charge mpaka asubui hafi hivi navyoandika hapa imegoma kuwaka leo wiki sasa. Ukiweka charge inavibrate tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…